hypothalamus
Senior Member
- Feb 19, 2018
- 126
- 153
Sadhu Amar Bharati wa India amenyoosha mkono wake wa kulia juu kwa miaka 47 bila ya kuushusha chini kama alama ya Utukufu wa Mungu wa kihindu ‘Shiva’
Mwaka 1973 aliamua kunyoosha mkono wake wa kulia kwa nyuzi 90 hewani,kufikia 2020 vidole vyake vimejishikiza kwenye kiganja cha mkono,kucha zake ni ndefu sana na zimejikunja kunja mithili ya nyuzi zilizo chunwa chunwa kutoka kwenye mti. Mkono huo unaonekana kama kipande cha mbao na hauwezi kutumika tena hata akitaka kuutumia
Mwaka 1970 aliacha kazi,mke wake na watoto watatu ili kujisalimisha kwa Mungu ‘Shiva. Miaka mitatu baadae aliona bado hajajisalimisha vya kutosha na bado hajajitenganisha na maisha ya anasa ya kidunia hivyo akaamua kuinua mkono wake wa kulia ili kujitenga na maisha yote ya anasa’ yanayoletwa na maisha ya kawaida ya dunia.