Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 761
- 1,464
Huyu alikuwa ni sister wa kanisa Katoliki, anaelezwa kuwa wakati wa uhudumu wake alihofiwa kuwa alikuwa anamilikiwa na nguvu za giza. Jina lake kamili anaitwa Sister Josephine Rosenthal.
Mwaka 1742 sister Rose alipata ujauzito kimaajabu kwani hakuwa amewahi kushiriki tendo la ndoa na mwanaume yeyote tangu azaliwe, alipata ujauzito kwa njia iliyoleta utata, alikuwa anaishi na masister wenzake katika eneo la siri ambako hakuna mwanaume aliyeruhusiwa kuingia.
Ilikuwa ni ajabu mno, masister wenzake walibaki kushangaa kwani habari za kupata ujauzito bila kushiriki ngono walikuwa wakizisoma kwenye kitabu kitakatifu cha Bibilia pekee, wakabaki flummoxed, midomo wazi.
Hilo pekee halikutosha kuwashangaza kwani mbali na kuwa alikuwa bikra lakini pia baadaye iligundulika kuwa hata uwezo wa kushika mimba Rose hakuwa nao, alikuwa mgumba, iweje sasa ajikute mjamzito?.
Hali hii ilitosha kuwaaminisha watu kuwa Sister Rose alikuwa na pepo, kwasababu kuna muda mwingine pia hata tabia zake hazikuwa za kawaida.
Mimba yake ilipofikisha miezi 6 akachukuliwa na kutengewa sehemu maalumu ya kuombewa muda mwingi hadi mtoto alipofikisha umri wa miezi 8 na kisha kuzaliwa.
Kutokana na kupoteza damu nyingi Rose alifariki siku hiyo anazaa na kumuacha mtoto wa kike aliyemzaa akiwa na afya dhoofu ilihali, lakini licha ya haya yote mtoto alilelewa na kuja kufariki baadaye akiwa na umri wa miaka 33, mtoto huyu alipewa jina la Maria.
Baada ya sister Rose kufariki alikatwa kichwa chake na kikahifadhiwa katika makumbusho ya Merrylin Cryptid Museum London kwa imani ya kuwa mapemo hayataendelea kumsumbua yeye wala waliobaki, waliamini pia kuwa hata ujauzito alioupata kimaajabu ulisababishwa na pepo.
Historia imeandika kuwa baadaye iligundulika kuwa Rose pamoja na mwanaye Maria ni binadamu wa ajabu waliowahi kuishi ambao damu zao zilikuwa na uwezo wa kutunga ujauzito zenyewe ndani ya mwili bila kufanya ngono.
Mtoto anapozaliwa basi mama lazima anafariki, ndivyo ilivyotokea pia kwa Maria japo yeye na mtoto wote walifariki.View attachment 1495294