Labda hatuelewani! Matokeo ya wanafunzi bora kwa madarasa yote kuanzia darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita yameanza kutangazwa rasmi mwaka 2016.
Sasa kama hizo orodha zipo naomba utuoneshe! Tayari umetuonesha za mwaka 2012, matokeo ya kidato cha sita. Mengine yako wapi? Matokeo ya kidato cha nne na darasa la saba?
Nadhani naelewaka, kwa mtindo unaotumika sasa hivi, naomba na wewe uwasilishe matokeo ya wanafunzi bora vivyo hivyo.
Hayapo! Eeh!
Wekeni hizo orodha hapa! Hata PDF hamna? Mimi nataka niwaoneshe kitu fulani ambacho ni tofauti na matokeo ya wanafunzi husika.Jamaa chenga sana wewe' wanafunzi bora kitaifa wanatangazwa tangu kitambo sana
Wekeni hizo orodha hapa! Hata PDF hamna? Mimi nataka niwaoneshe kitu fulani ambacho ni tofauti na matokeo ya wanafunzi husika.
Kwa mfano, aliyeongoza kidato cha nne mwaka 2008 kwenye cheti chake ameandikiwa amepata division one ya point 13 lakini kwenye orodha ya wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa yumo na anaonekana ameongoza na alipata division one ya point 7.
Vile vile aliyeongoza kidato cha nne mwaka 2007 kwenye cheti chake ameandikiwa amepata division one ya point 17 lakini kwenye orodha ya waliofanya vizuri kitaifa yumo na anaonekana ameongoza na alipata division one ya point 7.
Tena, aliyeongoza kidato cha nne mwaka 2006 kwenye cheti chake ameandikiwa amepata division one ya point 11 lakini kwenye orodha ya waliofanya vizuri kitaifa yumo na anaonekana ameongoza na alipata division one ya point 7.
Tena na tena, aliyeongoza kidato cha sita mwaka 2010 kwenye cheti chake ameandikiwa amepata division one ya point 6 lakini kwenye orodha ya waliofanya vizuri kitaifa yumo na anaonekana ameongoza na alipata division one ya point 3.
Sasa tatizo linakuja wapi? Matokeo ya kwenye cheti yakiwa tofauti na yale matokeo yanayosoma kwenye fomu ya maendeleo ya mwanafunzi [ TSM9 ], hupati kazi popote pale duniani au kwa lugha nyingine wanasema "vetting disclosure" yaani vetting imegoma.
Ikitokea umepata bahati utaishia kuajiriwa kupitia halmashauri au kupitia wizara kwa wale wa sekta ya afya na kilimo. Na ukiwa na bahati zaidi utaishia kuajiriwa kupitia serikali kuu.
Lakini sahau kuajiriwa nje ya nchi au kwenye taasisi za kimataifa kwa sababu ya "vetting disclosure" na hii ndio sababu inayopelekea watanzania wengi kutokuwepo kwenye soko la ajira la kimataifa.
Hii fomu ya [ TSM9 ] ndio inayoeleza taarifa za mwanafunzi husika tangu chekechea mpaka chuo kikuu. Yaani ni kivuli cha mwanafunzi husika, popote pale utakapoenda hili faili litakufuata mpaka sehemu yako ya ajira.
Sasa hakuna wa kukuajiri kama hii fomu ya [ TSM9 ] ni tofauti na matokeo yaliyopo kwenye vyeti.
Ndio maana ninasema hizo orodha tunaomba zitangazwe ili wale wanafunzi waliongoza wajitambue na wapewe vyeti vyao kulingana na ufaulu wao ili kuondoa hii tofauti.
[emoji23][emoji23][emoji23]nadhani ni mtu mmoja ila id mbili tofautMkuu una undugu na Deo Kisandu?
Engineer anafundisha??..... hii kweli tz ya vi-wonder.....poor utilization of scare resources
Kwanini mkuu 😂😂? Mbona simfahamu huyo mtu!Mkuu una undugu na Deo Kisandu?
Kwanini mkuu [emoji23][emoji23]? Mbona simfahamu huyo mtu!
Imepita miaka takribani 12 sasa, tangia Tanzania ilipapata kumshuhudia mwanafunzi aliyeshindikana katika maswala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's
Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama kibaha, ilboru, mzumbe, kilakala, Tabora boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.
Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga secondary kuendelea na masomo yake ya Advance level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)
Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A
October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.
Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania hasa shule za Advance.
Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo. (tetesi [emoji6] [emoji6]).
Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tuu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.
Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011,2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"
Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake nyumbu na kuwa na jeuri zaidi ya akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amedhamiria kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.
Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.
Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania na kuwaonesha wengine uwezo wake katika nyanja nzima ya Elimu.
Wapo wengi wanaojiuliza Eng Elias Kihombo yupo wapi kwa sasa, Lakini mpaka sasa Kihombo yupo chini ya Himaya ya Mkoa wa Geita Nyumbani kwa Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuri, huku akiendeleza harakati zake na akiwa na vitabu vyake vingi alivyoviandika kuwasaidia vijana wa Tanzania ikiwa pamoja na Physics Books na Chemistry Books.
Written by Eng EVANS RICHARD.
*We Always Live To Fight Another Day*
View attachment 818214View attachment 818215View attachment 818222
Hata kuandika sentensi ya kiingereza inakushinda! Ilikuaje ukapata shahada yako?
Ndio haya tunayosema, elimu ya Tanzania ilikuwa ni soko huria.
Pesa ilikuwa inamaliza kila kitu, na sio uwezo wa mwanafunzi husika. Ndio maana hata kimataifa watanzania hawapo!
Nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Msumbiji na hata Malawi zimetupita mbali sana kielimu.
[/QUOTE
Umekosea mkuu, nimesoma na haya mataifa yote na hawana chochote cha ajabu, mbona tumewaburuza sana chuo.
Usishuhudie usichojua.
Hapana aisee![emoji23][emoji23][emoji23]nadhani ni mtu mmoja ila id mbili tofaut
Basi acha hizo mambo za don nalimison aka deo kisanduHapana aisee!
sifa zinazomiminika kwa huyu kiumbe wengine zinawauma wanatamani wangekua wanasifiwa wao, tuache roho za chuki zisizo na msingi hasa kwa watu tusiowajua, ukisoma hii thread kuanzia mwanzo lazima ukubali uwezo wa huyu mtu na ukiendelea kubisha basi ni roho mbaya na chuki ya asili tu itakua inakusumbua na utakua unahitaji Tiba ya kiroho.Nasema hivyo nikiwa na maana ya kuwa kupata division one ya point III siyo kigezo cha kuwa mwanafunzi bora kitaifa. Kama hiyo orodha ipo, naomba utuoneshe.
Kuna Civil Engineer kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam [UDSM] anachonga madirisha.Mbona Engineer Manyanya anauza mbaazi
Hmm! Mimi binafsi namfahamu kwa sababu alinifundisha masomo ya dhiada [ tuition ] ya Physics na Mathematics mwaka 2009.sifa zinazomiminika kwa huyu kiumbe wengine zinawauma wanatamani wangekua wanasifiwa wao, tuache roho za chuki zisizo na msingi hasa kwa watu tusiowajua, ukisoma hii thread kuanzia mwanzo lazima ukubali uwezo wa huyu mtu na ukiendelea kubisha basi ni roho mbaya na chuki ya asili tu itakua inakusumbua na utakua unahitaji Tiba ya kiroho.
We fala hujui hafu unakera hfu mbishi kama shipaMatokeo ya wanafunzi bora, yaani kumi bora [ 10 ] - kuanzia darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita yameanza kutangazwa rasmi mwaka 2016, kipindi cha rais John Pombe Magufuli.
Kabla ya hapo, yaani tangu kuundwa kwa Baraza la mitihani [ NECTA ], mwaka 1964 hadi mwaka 2015. Matokeo ya wanafunzi bora kwa hatua zote yalikuwa hayatangazwi.
Hivyo basi, huyu mwanafunzi anayetambulika kwa jina la Elias Kihombo, anayejinadi kama mwanafunzi aliyeongoza kidato cha sita mwaka 2006 sio yeye na ni tapeli kama walivyo matapeli wengine.
Ili kuondoa sintofahamu na kuzuia watu wa aina hii kwenye jamii na hata kutambua wale wanafunzi bora walioongoza kihalali tangu mwaka 1964 hadi mwaka 2015 kupewa haki zao kama wasifu wa kitaaluma.
Kama ilivyofanyika kwa mwaka wa 2016, 2017, 2018 na 2019 chini ya mamlaka ya rais yaani "Presidential Decree Order" au maarufu kama "OPD" tungeomba ifanyike vivyo hivyo kwa matokeo ya wanafunzi bora kwa miaka iliyopita, yaani kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 2015.
Hii itasaidia kuondoa makandokando yaliyokuwepo na yanayoendelea kuwepo kwenye baraza la mitihani [ NECTA ]. Kwani matokeo ya shule katika hatua zote - yaani darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita yamekuwa yakikumbwa na udanganyifu na ulaghai wa kutisha!
Ukanda! Ukabila! Udini! Na hata rushwa zimekuwa ni nyenzo katika upangaji wa matokeo ya wanafunzi kwa hatua zote za elimu.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kipindi cha mwaka wa 2005 hadi mwaka 2015, ambapo elimu ya Tanzania ilikuwa ni kama soko huria "Tanzania Education System was a form of a modernised market - the more you pay, the higher you score". Yaani anayelipa pesa nyingi ndiye anayepata matokeo mazuri bila ya kujali uwezo wa mwanafunzi husika.
Kwahiyo kutangaza matokeo ya wanafunzi bora kwa miaka ya nyuma itasaidia sana wahitimu waliopita kufahamu wasifu wao wa kitaaluma.
We fala tu mmoja eti umekuwa wa kwnza 2007 labda umewaongoza CCM.Weka hiyo orodha, hata ya 2015! Jamiiforums sio kijiwe, tuna watu wa kila aina humu!
Mimi mwenywe nimemaliza kidato cha nne mwaka 2007 na kidato cha sita mwaka 2010.
Ninachokueleza ninauhakika nacho, kwa sababu hata mimi niliongoza kidato cha nne, mwaka 2007.
Lakini nimekuja kufahamu baada ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi, mwaka 2017 kama mhandisi.
Baada ya muajili wangu kuomba taarifa zangu za kitaaluma [ TSM9 ] kutoka baraza la mitihani [ NECTA ].
Sasa kama unasema unawajua baadhi ya watu walioingia kumi bora, naomba utuwekee hiyo orodha hapa. Jamiiforums ni jukwaa huru [emoji23][emoji23][emoji23]