Mfahamu "Victor DJ Rule Bongo UK" Promoter- Tapeli wa Diamond

Winnie227

Member
Joined
Jun 21, 2013
Posts
86
Reaction score
41
Victor hafai- kabisa,Kwa wasiomjua- huyu jamaa ameanza- hizi vurugu- kitambo.

Ameshawatapeli kina Ay birmigham Ay alienda clouds akachafua ila nadhani watu wakawa hawajajua kiundani ni nani mwaribifu,Tena akarudia akamfanyia tena Mr blue,tena Ali kiba ndo husiseme huyu huwa halipwi kabisa na uambulia mademu na kukaa kwa victor.

Matonya na Nonini nao,Chege na Temba pia sanaa kibao.Victor yeye huwa anaharibu halafu anakimbia na kutupia lawama watu wasio husika. Kwamfano latest tweet yake ya insta inasema "tatizo sio promota au Diamond bali ni club licence"Huu ni wizi mtupu,huyu jamaa analeta urafiki na wasanii na kusahau hii ni biashara.

Huyu mtu anatakiwa kufunguliwa mashtaka kwasababu hii sio mara ya kwaza wala ya nne na hatua zisipochuliwa huyu mtu ataendelea.bila kumsahau TID,last shown TId aliongea kwenye page yake victor kamtapeli,naona watu walidhani ni bangi za Tid ila sio mara ya kwanza kwa Tid kuzinguana na victor
 
Haya sasa na movie lianze...

Wasanii wetu mbona wamelizwa sana hii alikutana na kigingi uyo mchizi. Wamezoea mtu akisha tua London basi kwa roho zetu peace za kibongo mtu anaona fans watanionaje anapiga show kisha anapelekwa shopping anarudi bongo kimyaaa. Mimi uwa nashangaa kwa nini mtu unamwamini mbongo kisa yupo Europe wakati kakimbia rhumba uku, we toka lini mbongo akawa promota nchi za watu kwa mtonyo upi kama sio janjajanja .
 
Za mwizi arobaini..Huyu victor machota a.k.a Victor djrule ndo promota anayemleta Ali kiba uingereza kila siku.Ali kiba mpaka kamzalisha dada mmoja birmigham kwa kuendekeza ufuksa..huyu victor anachojua ni wanawake,pombe na utapeli..Waulizeni offside trick,mr blue Na Tid hawa wachache..jamaa ni mwizi..Kiba ndo kama dem wa jamaa..maana yeye huwa upewa sanaa tu na jamaa na shopping.akija anakaa kwa Victor halafu ni starehe kwenda mbele ..Kiba kashadhurumiwa sana na victor sema ndo hasemi yeye analia kimya kimya tu..
 
Hata Domo kasisitiza watu wa UK ukiona Victor anaandaa show basi maraia wa uk wawe makini jamaa ni namba chafu.
 
Wanalizwa kwasababu hawaendi na kwa mikataba wanaenda kishamba shamba,na elimu nayo pia inachangia kwenye mambo mengine jamani..............yani ushamuona mwenzio kanyolewa bila kutiwa maji kwanini na wewe usikitie chako maji kabisa?
 
Haya ni matatizo ya ubinafsi na kila mtu akienda nje kufanya show anachukulia ujiko.iweje watu kibao walizwe na wote wanatoka hapahapa.Maana yake wasanii awana pool ya kudiscuss mambo mbalimbali kila mtu akiibiwa anarudi na jeans na raba na maumivu kichwani.

Watalii wa ulaya wana pool za kujadili kila nchi na jinsi walivyotendewa kana kwamba record mbaya aiwezi jirudia kwa mteja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…