Mfalme aliyekuwa wa Zanziba, Sultan Sayyid Jamshid ni mzawa mzaliwa wa Zanzibar hakuja kama Mgeni

Mfalme aliyekuwa wa Zanziba, Sultan Sayyid Jamshid ni mzawa mzaliwa wa Zanzibar hakuja kama Mgeni

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
hqdefault-480x272.jpg

MFALME ALOPINDULIWA SAYYID JAMSHID

Nyerere alikua na lake moyoni (agenda ya siri)alishiriki kumtorosha huyu ili apate kui Koloni Zanzibar kwa Kisingizio cha Ubaguzi wa Kiarabu na Sultani.

Sayyid Jamshid hakuja Zanzibar kama mgeni kutoka Arabuni, Sayyid Jamshid Kazaliwa Zanzibar na kasoma Zanzibar mpaka kamaliza na kaondoka Zanzibar baada ya kupinduliwa na Kapitia Bandari ya Dar es Salaama kuelekea Uengereza (Portsmouth)alikokwenda kuomba Ukimbizi , kwahio Jamshid ni Mzanzibar kama wengine walozaliwa Zanzibar na kuwa na haki ya Uzaliwa.

Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliupindua utawala wa kiarabu tu ,lakini sio kupindua haki ya Wazaliwa wenye asili za Kiarabu, kihindi, kingazija , generation yote ya vizazi hivyo sasa ni Wazaliwa wa Zanzibar na wana haki kama wale wazaliwa wa Tanganyika akina Nyerere, na Ali Hassan Mwinyi na Mpaka Kikwete mwenyewe.

Sasa ukisema watu hawa wenye asili za kiarabu ,kihindi na kingazija Unawabagua haliyakua ni Wazaliwa wa Zanzibar na huwataki unataka Wahame Kikwete na ccm yako, jee tukikuliza utawapeleka wapi?

Wewe Mwenyewe Kikwete uko tayari kuhamishwa Bwagamoyo Tanganyika?

Wznz tumechoka na ubaguzi wa ccm wakutugawa kwa misingi ya hii ya Uarabu(Usultan ) Uhindi ,Ungazija,Upemba na kubwa zaidi sasa ni karata ya Undini ambayo ni kuomba huruma kwa mataifa ya Magharibi kuja Zanzibar ku deal na Waislamu wa Zanzibar ? maskini ccm Smz kupoteza muelekeo hata wa Dini yao kwa TONGE, Waislamu wa Zanzibar si 0% ni %99 sasa unapo tumia U-dini kwa kukiimarisha chama Basi utafeli tu .

Makabila yote hayo nilioyataja hapo juu hakuna alokaribishwa Zanzibar wote ni Wazaliwa wa Zanzibar kulikoni hata Ali Hassan mwinyi na Wenzake walokuja Zanzibar kwa kukaribishwa sio Uzawa, katu huwezi kumlinganisha U-Zanzibar wa Ismail Jusssa, Eddy Riam , Maalim Seif ,Maalim Haroun, Salim Dimani na wengine kua ni sawa na Ali Hassan Mwinyi ambaye sio Mzaliwa wa Zanzibar .

Mwinyi hana sifa ya Uzawa wa Zanzibar lakini hao wote wana sifa ya uzaliwa wa Zanzibar na si watu walozaliwa nje ya Zanzibar wamezaliwa Zanzibar na kusoma na kumaliza Zanzibar hata huyo munaye mwita Sultan Jamshid , kwa hio ccm wacheni karata ya kubagua jamii ya Wananchi wa Zanzibar kwa misingi ya Ubaguzi wa rangi .

Visiwa vyetu viwili vya Zanzibar vina mchanganyiko wa makabila na wa rangi , kama badhi ya visiwa vingi ulimwenguni vina sifa hio.

Sasa ccm Munapo tumia siasa kwa kubagua jamii hili hatutolivumilia hususan hapa kwetu Zanzibar, ccm Smz tutapambana na nyiyi kwa jambo hili mpaka kiama na ni haki yetu.

Unapoleta kuwagawa Wazawa wa Zanzibar kwa misingi ya rangi zao na asili zao, hii itawa-cost sana ccm na mwicho wa hayo ni kufilisika kisiasa na chama chenu kukosa Dira na muelekeo na kuachiwa wenyewe munaojita WAHADIMU mukiongoze chama chenu cha Ubaguzi?.

Hivi sasa Takriban Wananchi wa Zanzibar wamechuhudia mengi yalokuwemo kwenye nyoyo zenu , juu yakua Bunge la katiba halijulikani kua litaendelea au vipi ? lakini tunamshukuru Allah kuona yale muliokua nayo katika Nyoyo zenu.

Mzalendo.net - Zanzibar na zama za ukweli na uwazi

M/mungu ibariki Zanzibar na watu wake wote.
 
Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana. Alichofanyiwa Mh. Dr. Salim Ahmed Salim kipindi kile nadhani kila mmoja anakikumbuka. Sijui hawa jamaa wanavyosema wanamuenzi Nyerere wanamaanisha nini haswa!

Kuna haja ya Katiba Mpya kueleza kinagaubaga maana na mipaka ya propaganda na ni wakati gani mipaka hii ikivukwa inakuwa ni uvunjaji wa Katiba vinginevyo tunaelekea kuzalisha Interahamwe hatari sana siku za usoni kwa tunachodhani tunapiga propaganda. Warioba ni mtu wa kutukanwa nchi hii kweli? Dr. Salim ni mtu wa kubaguliwa nchi hii hadi na watoto wasiojua hata kuchamba vizuri?
 
Alipateje ufalme? kwa mila za Kiafrica mfalme anawakilisha wananchi wake sasa ufalme aliupata wapi wakati wazazi wake ni wahamiaji?
 
Alipateje ufalme? kwa mila za Kiafrica mfalme anawakilisha wananchi wake sasa ufalme aliupata wapi wakati wazazi wake ni wahamiaji?

Karume wazazi wake wahamiaji histori iko wazi nenda kwenye mtandao utapata historia yote ya Karume na wazazi wake wamehamia lini zanzibar.

ukitafuta vizazi vya karume hakuna zanzibar,Karume hana hata generation moja ya vizazi vyake zanzibar,aliekuwa Sultan wa zanzibar unaweza kwenda nyuma geration 8 au zaidi nyuma,,,,ya wazazi wake wametokea zanzibar,sasa nani ni mzanzibari nani anafaa kutawala nchi ya zanzibarar kati ya Karume na aliekuwa Sultan wa zanzibar

siko upande wa Sultan lakini huo ndio ukweli,msema kweli hutunzwa,msema kweli ni mpenzi wa mungu
 
Siku zanzibar ikiwa na wananchi 20% wakristo hakika nitafurahi sana.
 
Karume hakuwa mfalme Je ufalme wa hao waliutoa wapi kwa wananchi wa Zanzibar?
 
Alipateje ufalme? kwa mila za Kiafrica mfalme anawakilisha wananchi wake sasa ufalme aliupata wapi wakati wazazi wake ni wahamiaji?

Kamundu,
Ili uweze kujua ilikuwaje hata usultani ukaingia Zanzibar inabidi wewe mwenyewe
usome historia ya Zanzibar.

Ukiuliza maswali haya hapa JF hutopata historia itakayokusaidia.
Ingia google utapata mengi ya manufaa.

Lakini kwa kuanzia kitafute kitabu, ''Omani Sultans in Zanzibar,''
(1988) kimeandikwa na Ahmed Hamoud Al-Maamiry.

Kitabu hiki kina sura 12 na ya sura ya 12 ndipo utakuta habari
za Sayyid Jamshid Bin Abdulla Bin Khalifa 1963 - January 1964.

Kwa taarifa yako tu mwandishi wa kitabu hiki alipata kuwa
mwakilishi wa Oman katika Umoja wa Mataifa na ni Mzanzibari
na akisema Kiswahili kama sisi.

Hivi sasa Al-Maamiry ni marehemu.
 
zanzibar yenyewe jina lake limetokana na muarabu kupaita zenji, yaani nchi ya watu weusi, hivyo muarabu hawezi kuwa mwenyeji wa zanzibar zaidi ya mtu mweusi kwa kuwa yeye mwenyewe alipotoka zake arabuni aliwakuta.
 
Kakke,

..JAMSHID arudi, ajiunge na CCM, mambo yake yatakuwa mazuri.

..kinyume cha hivyo ataendelea kupigwa na baridi huko Uingereza.

cc gombesugu, Mohamed Said, Nguruvi3, Barubaru

Nikuulize JE MMESHAPATA UFUMBUZI NANI ANA HAKI YA KUCHINJA?

Vipi na nchi kuongozwa na mfumo KRISTU, si umeusoma WARAKA WA KICHUNGAJI WA KIKATOLIKI uliosainiwa na maaskofu 21 na kusomwa katika makanisa yote katoliki wakti wa pasaka?

Jiangalie kabla kumwangalia mwenzako.

..Jamshid afungue tawi la CCM hapo Portsmouth mambo yatamnyookea tu.

..wanakwambia if u cant fight them, join them.
 
Kakke,

..JAMSHID arudi, ajiunge na CCM, mambo yake yatakuwa mazuri.

..kinyume cha hivyo ataendelea kupigwa na baridi huko Uingereza.

cc gombesugu, Mohamed Said, Nguruvi3, Barubaru

Dole mjomba.
Na akisema anarudi na kujiunga ccm atakaribishwa na watampa jimbo la mji mkongwe kugombea.hao ndio ccm ..kwani si huko wapo mahizbu wengine kama salim ahmed
Mohamed aboud
Salmin amour
Seif khatib
Raza
Asingie cuf bi asha bakari atamwambia ana busha buree
 
Last edited by a moderator:
..Jamshid afungue tawi la CCM hapo Portsmouth mambo yatamnyookea tu.

..wanakwambia if u cant fight them, join them.

Je umeshawahi kumuona mtu anatoroka peponi na kukimbilia motoni?

Ana shida gani Jamshid mpaka arudie uraia wa Tz. Kwani akitaka kwenda ni kama kumsukuma mlevi tu ni kuchukua viza na kwenda popote Tz bila kipinganizi.

LAKIN NIMEKUULIZA HUKO TGK MMESHAPATA UFUMBUZI NANI ANA MAMLAKA YA KUCHINJA? NA VIPI MMEKUMBUKA KULIWEKA KATIKA KATIBA YENU YA TGK?
 
..mkataa kwao mtumwa.

..Jamshid atakuwa sawa na mtumwa kwa kuikana Zanzibar na kuendelea kuishi ukimbizini Uingereza.

..mimi nimeshauri tu kuwa aanzishe tawi la CCM hapo Portsmouth kama maandalizi ya kurejea Zanzibar.

NB:

..suala la kuchinja limekwisha, na sasa tunaendelea na utaratibu ambapo Waislamu ndiyo wanachinja wanyama.
 
Jamshid ni raia halali wa Oman na anaishi UK kwa kufuata taratibu zote za kiuhamiaji kama ilivyo kwa waTZ lukuki waliopo huko ambao wengi wao wanakuwa wanabeba mabox kupata pesa za kujikimu.

Sasa na nyie mnaokataa UTANGANYIKA wenu ina maana ni watumwa?

Je umewasikia wenzako wanasema MBILI ZATOSHA YA TATU YA NINI? je wanaogopa nini kuanzishwa kwa Taifa lenu huru?

Sasa vipi hilo la uchinjaji mumeliweka katika katiba yenu ili lisije zua rabsha na mapigano hapo siku za usoni?

..mimi sijasema Jamshid yuko UK kinyume cha taratibu.

..nilichoshauri mimi ni jinsi gani huyu bwana arudi Zanzibar nchi yake alikozaliwa na kulelewa.

..namshauri aanzishe tawi la CCM huko Portsmouth, wakina Ali Karume watamkubali.
 
Je u,eshawahi kumuona mtu makini kabisa na akili zake timamu ANATEMA ASALI NA KUTAMANI PILIPILI? Je mtu huyo atakuwa tamamu kiakili?

Pole sana
 
Zanzibar katika kila kundi lazima atafutwe mtu mwenye rangi nyeupe kidogo japo kama ya kina Lowassa au Kikwete ili waonekane waupe au wenye asili ya mbali na sio Africa, wengine wanaitwa makusudi kama kuwakodi na kuwekwa mbele ili wajione na uhindi au uarabu hivi, kuna majimbo pale yanawagongea wahindi au waarabu wasiojua chochote zaidi ya kupanda minazi na kuwaomba wawe wawakilishi wao serikalini ili lionekane jimbo la weupe.
wazima hawa?
 
Je u,eshawahi kumuona mtu makini kabisa na akili zake timamu ANATEMA ASALI NA KUTAMANI PILIPILI? Je mtu huyo atakuwa tamamu kiakili?

Pole sana

..winter haizoeleki hata ukae miaka mingapi huko ulaya.

..kwa umri wake Sultani anatakiwa apumzike mahali penye hali ya hewa ambayo ni rafiki kwa watu wa makamo yake.

..Jamshid kuendelea kuteseka na winter ukimbizini Portsmouth, wakati anaweza kurudi kwao Zanzibar, ni mfano dhahiri wa mtu anayetema asali na kufakamia pilipili.

..SULTANI asiendelee kukataa kwao, na kuwa sawa na MTUMWA.
 
Back
Top Bottom