Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

mkuu unatufikirisha vizuri lakini neno "kama" mbona ni ufananisho sidhani ni uhalisia.

Mfano:
Tulikiwa machoni pao kama nzige.???
Shetani ni kama simba aungurumaye?
Yesu kama mwanakondoo asubiriye kuchinjwa??
Zaburi 1:3 naye atakuwa kama mti uliopandwa kati ya maji.

Isaya 40:31 wamngojea bwana watapaa juu kama mbawa za tai.

mkuu binafsi bibilia naipa Highest authorty kuliko vitabu vingine, lkn pia nakubali kujifunza kutoka katika vitabu vingine lakini sio kama vyenye msawazo sawa na bibilia. naamini maneno ya agano la kale aloyotumia yesu ndiyo tunayotumia sisi kujenga hoja licha ya uwepo wa mavitabu mengi enzi hivyo ambavyo havikuwa endorsed na mwokozi.


bibilia imejaa ufananisho wa watu na viumbe vya asili katika mantiki mbalimbali, tunajifunza kwa urahisi lwa kuangalia viumbe asili zaidi ya masomo dhaania.

maoni na mtazamo juunya comment yako mkuu.
 
Mkuu wanaposema KAMA ni kweli haimaanishi ndio uhalisia ila ni ULINGANISHO kuwa kitu kitakuwa kwa mithili hiyo huwezi ukaniambia mtu akimuelezea magufuli atasema MREFU KAMA MNAZI haiwezekani sababu hata haikaribii nusu ya ukweli ila kwa mtu kama Hasheem thabeet kidogo inaweza onekana kuna kamfananisho kwa mbali

Hivyo hapa muandishi hata kma hamaanishi kuwa ogu alikuwa mrefu kama huo mti ila anajaribu kutuonyesha kuwa alikuwa MREFU SANA na MWENYE NGUVU SANA bila kujalisha ni kama hiyo miti au mbao ila ndio alichotaka tuelewe hivyo kwa mstari huu mtu akisoma atajua jamaa alikuwa na NGUVU SANA bila kujalisha kuwa alifikia hiyo mierezi na mialoni.

Na ndio maana hata mwandishi wa zaburi anatoa mfano kuwa wenye haki Watastawi na kuwa kama MIEREZI ya lebanon.... Akimaanisha watakuwa IMARA bila kujalisha utafikia uimara wa huo mti au lah.

Che mittoga SALA NA KAZI Malcom Lumumba
 
napata mawazo kadhaa...
1:ni vizuri tujue kusudi la Mungu kumuacha makusudi wakati Lengo lilikuwa ni Kuangamiza dunia yote kwa Maji. Waliopona walipata neema kwa Mungu na Mungu akawaweka wazi. Ingekuwa kuna Mwovu mwingine anapata rehema tungefahamishwa. Na kujua kama hakuwepo, mara baada ya gharika uendelezo wa vizazi haumuonyeshi wala uzao wake.

2:Rahabu alipata rehema, alafu ile adhabu ilikuwa ni regional sio grobal hata ile ya wakaanani. Lengo na hili la nuhu ni tofauti. Mwanzo Mungu anataka kufuta wanadamu wote, hapo case nyingine anataka kufuta baadhi ya watu waovu katika eneo flani tu, huku maeneo mengine ya dunia uovu unaendelea kama kawaida, hivyo muovu mmoja au wachache kupata rehema, au wajumbe wa Mungu kukengeuka na kitotimiza agizo walilopewa kukomesha regional uovu ni tofauti na sidhani kama ni sawa kutumia mifano hiyo.

3: Rahabu ulikuwa mpango wa Mungu. Na kupitia rahabu na Malaya wengine kama Tamari Yesu alizaliwa. na kuna typology nyingi tunapata kwa rahabu na wokovu wa mwanadamu, pamoja na ile kamba nyekundu iliyowaokoa wanadamu. Assumption Mungu aruhusu hybrid ya uovu, ambayo ndiyo ilikuwa lengo lake kuiangamiza hicho kizazi ambacho wewe unataka kiokolewe.

4:Watu sabini kuingia kwenye safina hiyo assumption ni sahihi kwa vitabu na maarifa nje ya bibilia. lkn hiyo hoja tukiijenga kwenye bibilia inaleta ukakasi mwingi.

*Mwanzo 7:7 wanaoingia wanatajwa. Nuhu, wanawe, mke wa nuhu na wake za wanawe. Mungu anawafahamu wana wa wana na huko nyuma kwenye geneology wametajwa lkn hapa hawakutajwa, na imerudiwa zaidi ya mara moja bila kutajwa, sidhani kama kunausahaulifu ila yawezekana ndivyo ilivykuwa.

*Mwanzo 7:13 Wanatajwa hado majina Shemu,hamu na yafethi na wake zao. Nuhu na Mke waku.

*Mwanzo 8:15,16
Wanatoka kwenye safina, Nuhu, mkewe, wanawe na wake za wanawe.

*Mwanzo 9:1 Mungu anawapa amri kama aliyowapa adamu na hawa kabla hawajapata watoto. Zaeni mkaongezeka mkaijaze nchi. Maana yake walikuwa hawana watoto.

*Mwanzo 9:18,19 wanatajwa wana wa nuhu hao watatu, na anapigilia msurmari mstari wa 19, "HAWA WATATU WALIKUWA WANA WA NUHU NA KWA HAWA WATATU NCHI YOTE IKAENEA WATU"

* Mwanzo 10:1 watoto wa hawa jamaa wanaozungumziwa ni Baada ya Gharika, baada ya kuambiwa na Mungu zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi.

5:Katika gharika Umesema Shem Alikuwa na miaka 100. hivyo anatakiwa awe ameshapata watoto.
Mwanzo 7:6, wakati mtoto wa kwanza anaingia na miaka 100, Baba mtu alikiwa na miaka 900.
hapo utaona Nuhu alipata mtoto akiwa na Miaka 800. kwa ratio hiyo tukiihamishia kwenye kizazi chetu au ukitoa sufuri Nuhu aliingia anamiaka 90, mtoto wake akiwa na Miaka 10.
kwa umri wa kabla ya gharika miaka mia ni kama teeneger. Ila kwa ukomavu wao walikuwa wameoa. yawezekana walikiwa hawajaoana muda mrefu au kwa ratio ya baba na watoto, watoto hawakuwa tayari wameshapata watoto.


mkuu nafikili kibibiliabibilia zaidi.
 

nimekupata mkuu.
ila inaonekana katika kila kizazi cha mwanadamu baada ya gharika hadi kesho kumekuwepo na watu ambao ni Extreme outlier kwa maana ya ulefu na ufupi.

kuhusu utofauti huu kuhusiana na unefili au ant-nephili DNA hapo mjadala uendelee mkuu.
 
Mkuu ukiwa msomaji wa biblia utaelewa hoja yangu kivipi Mungu anaweza toa hukumu ila akaruhusu masalia wabaki na amefanya hivyo hata kwa wanefili wa baada ya gharika (Waamori)ambayo ni familia ya mfalme Ogu

Twende taratibu

1. Mungu anamuamuru waisraeli waue wakaanani WOTE wasibakize kitu

Kumbukumbu la torati 20
16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;
17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru BWANA, Mungu wako
;

2.Tukisoma kwenye joshua baada ya kuwa wameikamata canaani waliweka makubaliano na hawa wanefili ya kuwaacha hai!!

Joshua 9:15
15 Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia

3.Kinyume kabisa na maagizo ya Mungu ya kwanza tunaona wagibeoni wakiachwa hai na waliingia agano ambalo Mungu alisupport

Kumbukumbu 7
1 BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang?oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;
2 wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao


4.mpaka hapa unaweza kufikiri waliamua wenyewe waisrael lahasha..... Huko mbeleni tutaona MUNGU akiwaadhibu waisraeli kwa kuvunja agano hilo la kuwaacha waamori/wagieboni hai

2 samuel 21
1 Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.

Je unataka kusema Mungu ni kigeugeu au utakubaliana na mimi kuwa Mungu aliamua kuwaacha hao wagibeoni kwa kusudi lake???

Na je kama tunaona hapa Mungu aliamrisha waue waamori WOTE ila baadae Mungu alitaka wengine wabakizwe je huoni hoja ya kusema Ogu kuwa mnefili pekee kuachwa kwenye gharika kuwa ina mashiko maana tumeona kumbe Mungu akitoa hukumu ya WOTE huwa anaacha exceptions!!!

Karibu tuelimishane mkuu wangu
Cc SALA NA KAZI Malcom Lumumba Eiyer popbwinyo Kudo900
 
Sasa kwann aliwaaacha wasaidizi wake ,wakafa kwa gharika? walikua wana msaidia bila kujua kuwa jamaa atawaacha au ? Maelekezo aliyopewa hayakuhusu kubeba wasaidizi ( km walikuwepo)
 
Nachanganyikiwa kabisa na habari hizi,mnaojua hivyo vitabu vingine tufahamisheni na tusiojua tuelimike
 
Nachanganyikiwa kabisa na habari hizi,mnaojua hivyo vitabu vingine tufahamisheni na tusiojua tuelimike
Mkuu hii ni biblia mbona ndio nmeongelea kwenye hii post na hata mfalme Ogu pia biblia inamtaja so hatupo mbali sana na vitabu vya dini

Labda udadavue kipi kimekuchanganya ili wajuvi watiririke
 
Hahahhaa, eti Gharika1...kwahiyo gharika ilifunika kila kitu "Duniani"?!!
Ushahidi wa canopy theory na ice age unasuggest kuwa dunia at some point ilifunikwa na maji.... Kuna ushahidi pia wa baadhi ya specie za baharini kukutwa katikati ya nchi kavu na majangwani hivyo kuthibitisha huko nyuma kulikuwa na tukio lililofanya bahari ihamie nchi kavu

So sio nadharia za kiimani tu ila hta wanasayansi wachache wamekuja na nadharia kuprove uwepo wa gharika zamani hta kma sio la Nuhu
 

Hakuna nadharia inayosuport dunia YOTE kufunikwa na maji katika wakati fulani!
 
Kuna na miji pia youtube ,ambayo ilimezwa na bahari
 
kuna movie fulani niliiona kuwa kuna tetemeko litaikumba dunia, volcano na aina zote za natural disaster.. halafu kuna jamaa alikua anahubiri kwisha kwa dunia watu wakawa hawamwelewi....

mwisho wa siku yakatokea kweli na huyo star wa hio movie.. atapewa ramani na huyo jamaa ambayo inaonesha mahala ambapo hapatakumbwa na hayo matatizo...

wakati huo madon wa dunia washatengeneza manyambizi ambazo zina kila huduma ndani yake.. ya kukimbilia kiama.. mwisho wa siku zile nyambizi baada ya kupata misuko suko siku nyingi zitafika South Africa Good hope.. Kwa maana kuwa Africa haitazama.


Hata sikuelewaga maana yake.
Na jina lake silijui wakuu nadhani wengi wetu tumeionaga
 
Kuna na miji pia youtube ,ambayo ilimezwa na bahari
Sehem ya ardhi kuzama inatokea mara nyingi tu, hata kuna mabara mazima yaliyowahi kuzama, lakin siyo dunia nzima izame chini ya maji, ukitazama vizuri muundo wa nchi na ukatazama kwa uangalifu mzunguko wa maji ni suala ambalo haliwezekani kutokea!
 
Hakuna nadharia inayosuport dunia YOTE kufunikwa na maji katika wakati fulani!
Canopy theory mkuu inaelezea ivo na bado tafiti zinafanywa kuipa nguvu zaidi

Na kuna nyingine inaelezea kuhusu kukutwa kwa mali kale za baharini juu ya milima huko Caucasus ambayo imewabakiza na maswali kivp maji ya baharini yafike juu ya mlima hadi yaache mabaki ya vitu vya baharini na sio caucasus tu ila milima karibu kila bara ina hiyo tendency je bado haiwezi kueleza uwepo wa gharika kuu
 
Na tena, kwa uelewa wangu mdogo tu nilionao nikitafakari nagundua kwamba Biblia inamfanya msomaji aushughulishe ufahamu wake apate kutambua vile wanefili wanavyo fanania.

Sababu inatoa baadhi ya sifa za wanefili waliokuwepo zamani zile, tena ukiendelea zaidi kuwatafuta wanafananaje utaona Biblia inakupeleka kwa Goliath angalau upate picha japo kwa sehemu tu wanefili wanataswira ya namna gani mbele ya mwanadamu wa kawaida.

Kiukweli ili kuelewa Maandiko Mtakatifu inahitajia msaada wa ziada nje ya akili ya kawaida ya kibinadamu na si kufanya uchambuzi wa kutengeneza historia yenye kuleta maneno kama vile, "Inasemekana", "Huenda ilikuwa hivi", Utafiti unaonesha hivi" nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…