Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Si wanasema malaika hawana jinsia
Ni kweli hawana mkuu ila wanauwezo wa kujibadilisha na kuwa wanadamu au angalau kuvaa mwili wa kibinadamu na kuweza kuzalisha..... Hata Mshana Jr aliwahi tupa incident ya wanawake kulalwa na majini na wengine kupewa mimba labda aje atusaidie na hili swali pia kwa upande wa ''malaika''.
 
M kuna kitu najiuliza /nauliza pia kama kweli hiyo Ogu ndio pekee aliyesalimika kwenye hilo gharika vipi kuhusu Unju bin Unuq..MTU aliyeishi Tanganyika kipindi n kwenye baadhi ya vitabu arabuni ameandikwa ambaye kabuli la kidole chake chenye urefu wa kilometa 1 kasoro kimezikwa bagamoyo kwenye makumbusho....ameandikwa kwenye historia ya kale ya kiarabu ambao walimuhusisha kabisa na Ogu kuwa ni MTU mmoja,...unju bin unuq wanasema alikuwa na uwezo wa kutembea baharini miguu yake ikagusa chini ya bahari na urefu kufika mawinguni ..chakula chake nyangumi anamkausha na jua kama kumchoma ..na huyu unju ndio inasemekana alibeba mlima kwa nia ya kuangamiza kambi ya musa na wanaisrael Mungu akamzuia(historia inapatikana katika vitabu vya historia uarabuni/wayahudi kama Ogu) ukisoma kumb 3,11 wanasema Ogu pekee ndio aliyesalia katika mabaki ya warefai ...na naamini mifano mengine iko mingi inayofanana na hiyo ogu/unju bin unuq aliyeweza kusafiri nchi moja kwenda nyengine kwa hatua tu!..ni kujaribu kutafuta historia za jamii za kale naamini utakuta nilikuwa na 'majitu' pia mfano Jamuhuri ya Congo kulikuw na jitu pia kwenye nimesahau jina lake na kitabu chake kipo / tukiachana na hayo tuje hapa;
Je kama Ogu ndio pekee aliyesalimika kwenye gharika vipi na huyu Unju bin Unuq !? Au Ogu na Unju bin Unuq ni MTU mmoja!?...bado nami natafakari na kuchunguza pia!
 
Mkuu mmangO sorry to say this....hivi vitabu vya dini tukividadisi sana utakuta kuna kasoro nyingi za kiuandishi sababu unakuta story moja ilioongelewa kwenye biblia imewahi ongelewa nje ya biblia kwa miaka maelfu nyuma mfano huyu mfalme OGU kihistoria yeye na UNJU BIN UNUQ ama UJ IBN ANAQ ni mtu mmoja sasa unju anaongelewa Tanzania ilihali OGU anaongelewa Israel hapo unapata maswali mengi sana kwamba kuna either moja alicopy na kupaste ama kuna historia inafichwa kwa makusudi kabisa ili kuwapa umaarufu watu fulani kuwa wao ndio walimuua OGU hivyo wana uwezo wa kitofauti!!!!

Nasema hivi sababu hata issue ya gharika kwa ancient texts za sumeria ilishaongelewa miaka 1000 hata kabla Nuhu wa biblia hajazaliwa lakini ukisoma jinsi biblia ilivyoelezea utaona story hizo mbili zinafanana kila kitu kuanzia ukubwa wa meli,number ya survivors, siku mvua ilinyesha n.k utagundua mmoja wao lazima amecopy na kupaste kama story hii ya OGU ni lazima alikuwa mmoja tu ila kama wa kweli ndio huyo wa bagamoyo au wa israel hapo ndipo changamoto ilipo!!
 
Ugumu unakuja kwamba dunia INA muda gani yaani huu Mwaka wa ngapi toka kuumbwa kwake hilo ni gumu sana ila kuna nakala /artcles mbili tatu nimezisoma bado sijapata chanzo halisi cha hizo story kufanana pengine labda(kutokana na hizo nakala nilizopitia /mtazamo wangu sisi (binadamu) sio viumbe wa kwanza kuishi duniani kulikuwa viumbe tofauti tofauti muumbaji alitengeneza viumbe kila kiumbe na wakati wake mwisho wa Siku akakiangamiza ila mpangilio wa maisha ukawa na mtiririko ule ule , maana ye ndo muweza wa yote anafanya atakalo....sasa basi kwenye Kitabu cha Mwanzo kuna mistari inasema "26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1 :26 yaani mtu kwa mfano wake (hii ni mistari migumu sana kuilewa) INA maana Adam alikuwa na mfanano na Mungu na kwa namna gani hasa..tafakari!
Kwenye kipindi cha uumbaji hicho hicho ukikaa chini ukifikiria kipindi viumbe viliumbwa kabla ya Binadamu/(kumbuka Mwaka 1 kwa Muumbaji/(Mungu sawasawa na miaka 1000) na kuna uzi wako mmoja kuna andiko uliandika kuhusu viumbe wa ajabu waliokuwepo duniani kwa mujibu wa biblia nadhani kabla ya binadamu kuumbwa kulikwepo na jamii ya viumbe hivyo vilivyoishi pamoja ikaanzisha utaratibu wao wa maisha binadamu tukaja kuiga tu...kufundishwa huko tukawaona hao viumbe kama miungu yetu mfano kwenye pyramids za Misri kuna mchoro kama huu chini nimezungushia duara LA kijani nacho ni kiumbe cha ajabu na kwa jinsi alivyo alikuwa ni kitu kichwa sio cha binadamu lakini alikuwa kama mungu....
Dhana nyengine ya kihistoria inasema Enoko /enuch alifundishwa na malaika mambo mbali mbali ya kuendeleza ulimwengu huu kabla ya gharika na nakala zake waandishi wanasema Musa alikuwa nazo kuvuka nazo mpaka nchi ya ahadi ,kama malaika walikuwa na uwezo huo wa kufundisha watu pia, pia fikiria na upande na malaika waasi walifanya nini kuenda kinyume na matakwa ya muumbaji!?..mpaka Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu aje atawale viumbe vyote vilivyopo!!?? Hii haina maana kulikuwa na viumbe vilivyoletwa na hao waasi kuangamiza mipango ya Muumbaji!??Nadhani biblia inadhumuni lake sio kukupa kila kitu cha kwenye historia ..nadhani isingebebeka kama kila kitu kingewekwa...Tuzidi kujifunza tu...
Kuna mwandishi wa nakala moja hivi jina limenitoka kidogo anasema alipokuwa chuo alifanya research moja alivyoenda kupresent kwa panel akakataliwa research yake maana nilikuwa ni deep sana na inahusu ndugu wa Mungu aliyeumba ulimwengu na miungu mengine ilikubalianaje kuumba dunia na kwasababu IPI(huku ndiko kuna chanzo cha familia ya Rothschild na Rockefeller ilipotokea ilikwepo kwa sababu maalum na utajiri wao hautafutika kamwe mpaka mwisho wa dahari/nikijipanga fresh nitakuja kuelezea kwa kina)na anasema dunia kabla ya binadamu kulikuwa na viumbe vilikuwa vinaishi na kwenye uislam wanaamini kabla ya binadamu kulikuwa na majini yanaishi..na hao viumbe kutaka kwa huyo mwandishi wa nakala anasema kiumbe alichokuwa akikihoji kilimwambia sisi sio jamii ya kwanza kuumbwa na Mungu wanasema walishuhudia Muumbaji aliumba jamii tofauti tofauti zenye miili ya kushangaza na kufutwa /kuangamizwa mpaka jamii aina ya sokwe pia (nadhani darwin alipitia nakala hii) kwa maana hiyo sisi binadamu tuna matoleo mengi mpaka tukaumbwa kwa mfano wake na mpaka Leo viumbe hao wanataka kurejesha dunia yao mikononi mwao kwa kuweka watawala wenye nguvu na kutawala dunia ndio mambo ya new world order kusaidiana na hizo familia tajiri yote sababu ya hao miungu /viumbe kuwa na na bifu na muumbaji...hiyo jamaa alifukuzwa na chuo maana nilikuwa chuo cha dini (nadhani) akabidi aandike nakala hiyo..anasema reference alipata kutoka kwa kiumbe kilichoanguka na ndege kutoka safari nyengine kilichomsimulia siri zote za ulimwengu ..na kila sayari kulikuwa na kiongozi wake kazi yake maalum ..mpaka jua pia viliumbwa kwa ajili hao sio binadamu(kuna dini moja uko hapa hapa Africa hata Tanzania ya kiasili kwenye nakala zao wameweka kazi ya kila sayari/sababu ya kuwepo /nitafuatilia zaidi)

 
KAMA SAMAKI WALIKUFA WE ALIBAKIJE, MUNGU HAONGOPI ACHA PROPAGANDA JAMAA NGU
 
KAMA SAMAKI WALIKUFA WE ALIBAKIJE, MUNGU HAONGOPI ACHA PROPAGANDA JAMAA NGU
Mkuu sio propaganda mie nimecopy na kupaste kutola vitabu vya dini sijaongeza mawazo yangu.....
1. Biblia inasema milima ilifunikwa kwa mikono 15 na tunaambiwa OGU alikuwa na urefu wa zaidi ya Futi 28 ina maana akipanda mlimani maji yaliishia kiunoni??

2. Biblia inasema yeye ndio MNEFILI pekee aliyebaki na wote tunajua wanefili waliishi kabla ya gharika sasa kama hakupona gharika kivipi mnefili awepo baada ya gharika??

3. Vitabu vya dini ya kiyahudi kama Midrash na Talmud/Tanakh ambavyo ni sawa na biblia kwa wakristo vinasema Mfalme Ogu alipona gharika je inamaanisha unafahamu zaidi historia ya wayahudi kuliko wayahudi wenyewe walioandika kwenye vitabu vyao vya kiimani kuwa Ogu hakufa kwenye gharika???

4. Anyway unaweza nisaidia Ogu alitokea wapi?? Maana alikuwa mnefili na ameishi baada ya gharika sasa basi unaweza kutusaidia Ogu alikuwepo wapi kiasi akawa mnefili pekee baada ya gharika?? Kama hakuwepo kabla ya gharika je alitokea wapi ilihali wanefili wote waliuliwa kwenye gharika??

Ukijibu haya utakuwa umenisaidia kuacha propaganda, natanguliza shukrani
 
Hawa wanefili ni matokeo ya malaika kuzaa na binadamu na inasemekana waliangamia na hawapo tena
Kwanini hawa malaika waliozaa na binadamu huwa hawashuki tena duniani na kuja kuzaa na mabinti wengine baada ya gharika hadi mpaka sasa?
Nini kimewazuia
Mkuu, Goliath?....kwenye Agano la kale wametajwa kadhaa baada ya gharika.
Na ninadhani jamii nyingi kutokuwa na tabia ya kuandika habari zao, kumepelekea kupotea kwa habari nyingi za hivi.
Nilipata bahati ya kuishi pale Tarime mjini kwa kama mwaka hivi, nilisikia habari za mtu/jitu lililoishi zamani kabla ya uhuru wa Tanganyika maeneo ya Magena (au) Remagwe...
Kwa masimulizi ya wazee wa kule, huyo jamaa alikuwa mkubwa ajabu, aliweza kubeba vitu ambavyo hata wanaume hodari ishirini wasingeweza kubeba! Na wanadai kuwa mwanamke aliyekubali 'kumpa mambo' alifia kwenye eneo la tukio!
 
kuna mdau lifecoded haya mambo ameyaelezea kwenye uzi wake umo humu ya kwamba sisi ni kopi tu ya watu original, tena kwa kuongezea tu nadhani kwa waafrika si kopi bali ni kama utokeaji wetu ni kama laana fulani ilitukumba.
Labda ndiyo sababu wazungu wanafanya kila mbinu kutuangamiza kupitia viproject mbalimbali haiwezekani kila ugonjwa usiotibika reference ni kwa waafrika na hatuna maarifa yakuweza kupambana na hayo magonjwa.Sasa jiulize siye tumeumbwa kutawaliwa au nasi siku moja tutawatawala hao wazungu
 


Huyu ndo yule kaburi la kidole chake lipo bagamoyo???
 
Huyu ndo yule kaburi la kidole chake lipo bagamoyo???
Sina uhakika mkuu ingawa story zao zinafanana.... Ila kwa muktadha huu watakuwa watu wawili tofauti sababu sidhani kama huyu wa bagamoyo aliishi miaka 2000 iliyopita na kama ni hivyo basi itakuwa mmoja wao kacopy na kupaste story ya mwenzake
 
Sina uhakika mkuu ingawa story zao zinafanana.... Ila kwa muktadha huu watakuwa watu wawili tofauti sababu sidhani kama huyu wa bagamoyo aliishi miaka 2000 iliyopita na kama ni hivyo basi itakuwa mmoja wao kacopy na kupaste story ya mwenzake

Kwa stori nilizozipata huyu wa bagamoyo aliitwa UNJU BIN UNUQ, na alikuwa na kaka zake wawili, naamini wewe ni mkali wa kufatilia haya mambo, bila shaka utatupa mrejesho tukaendelea kujifunza.
 
Duh nimejaribu kuafuatilia vifungu vya bible alivyotoa hapo mtna mada anafanya upotoshaji hakuna sehemu inaonyesha aliwahi kuwako kabla ya garika.
 
Duh nimejaribu kuafuatilia vifungu vya bible alivyotoa hapo mtna mada anafanya upotoshaji hakuna sehemu inaonyesha aliwahi kuwako kabla ya garika.
Mkuu soma kwa makini wapi nimesema source ni Biblia pekee??

Kingine kwenye biblia nimejenga hija zifuatazo naomba uzijibu ili tuende sawa

1. Unaweza kunieleza kivipi huyu Ogu aliyekuwa mnefili aliweza kuwepo baada ya gharika ilihali wanefili wote walifia kwenye gharika???

2. Biblia inaposema MNEFILI PEKEE ALIYESALIA.....kwenye kitabu cha Kumb. La Torati walimaanisha nini??

3. Biblia inasema huyu mtu alikuwa ana urefu zaidi ya mikono 13 za kinefili ambazo ni sawa na mikono 26 ya mwanadamu na biblia inasema maji yalizingira hadi milima mirefu kwa mikono 15 je kivp jitu la mikono 26 lizame kwenye mikono 15??

4.Kitabu cha imani cha wayahudi yaani Talmud ndio kinachosema bila kupepesa macho kuwa Mfalme Ogu alikuwepo kabla ya gharika na alikuja kuuawa na Musa na mpaka leo wayahudi wanaongelea ushindi huo sasa ina maana wwe ndio unajua sana historia ya Israel kuliko waisrael wenyewe hadi useme napotosha???

Embu twende taratibu hapa ili tuone upotoshaji ukwapi
 
Hii dunia ina siri nyingi sana. Pole yao wale wanaoamini kwamba mambo yote ya ulimwengu yametosheleza kuandikwa kwenye kitabu kimoja au viwili..

Uzuri akili ya binadamu ina advantage ya kufikiri na kuhoji. Tuzitumie hizo ili kunufaika zaidi na taarifa za ulimwengu.

Ujumbe huu ni maalum kwa wanaojibana kwenye quran na bible pekee..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…