Mfalme wa muziki wa Hip Hop Tanzania

herikipaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
1,198
Reaction score
1,369
Nikifatilia muziki hasa Hip Hop Bongo sasa naona kuna utofauti mkubwa, yaani kama pengo vile hawa wasanii wasasa wanashindwa kufikia swhemu ya walotangulia. Hamna maudhui ya maana kwa muziki wa sasa, kuanzia mashairi ni sifuri, kidogo mdundo Producers wanajitahidi sana, Producer ndiyo wanafanya kazi kubwa, lakini wakija kuingiza mashairi wanashindwa kulitendea haki ule mdundo, wanaishia kuharibu tu.

Nikiskiliza mashahiri ya Diplowmatz, Sugu, Gk, Professor J, John Mahundi, mfalme Hashim Dogo, naona utofauti na hawa wa sasa, wana uandishi mbovu, yaani ni upuuzi tu.

Kidogo Tamaduni Music wanajitahidi lakini hawajafika hata robo kwa niliyowataja hapo juu. Kwa bongo utungaji wa mashahiri na hata 'free style' hakuna wa kumfikia Hashim Dogo. Huyu alistahili hata tuzo ya heshima, akipewa ni vizuri tu. Ili hawa madogo wa sasa wajifunze kitu, kuwa kuna watu walifanya kazi kweli.
 
Watafute
Dizasta
Toxic
P mawenge
Unaweza pata kitu unataman kukiona
 
Tukikosa mfalme mpya tutumie tu wale wa zamani.Fid q,proffessor j,Roma,stamina,zilla.AU KWA KUWA VINATUVURUGA VITOTO.TUJITOE AKILI TUMPE HATA NAY WA MITEGO.
 
X-Plastaz wazee wa ushanta! Lord Eyez, Mr II, Langa Kileo (RIP)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…