SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kipindi Robetinho amekuja Simba, alikuja na vibe lake la ushangiliaji. Upande wa pili wakaanza kumkejeli sana kuwa anashangilia kwa kukimbia kimbia kama kichaa. Ikafika wakati nadhani uongozi ukamshtua, akapunguza ushangiliaji wake.
Leo hii kocha wa Yanga Gamondi anashangilia vile vile kama enzi za Roberinho, tena benchi lake zima linasafishwa, hawa wanakimbia huku, wale kule kama wameingiwa na pepo, ila kimyaaa, kejeli hauzisikii tena.
Ni sawa na kejeli zilizokuwa zinasemwa za Simba kuishia robo fainali kila msimu, leo wameingia wao wanapata mzuka hadi wanazimia viwanjani.
Moja ya vitu nilivyojifunza katika mpira wa kitanzania ni kuwa Watanzania ni wanafki sana. Wanaweza kukuponda na kukupiga vita kwa jambo fulani kumbe na wao wanalitamani ila hawajalipata. Ukijichanganya ukawasikiliza waswahili ukabadili njia zako, ndio unapotea mazima. Shika hili litakusaidia sana.