Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Wakati majirani huko na kule wanabaguana ni vema wakachungulia huku na kujifunza. Vilevile na sisi tukachungulia kule ili kuona ni vipi tusijefanya makosa kama yao.
Sifa za Makabila; (Ili uwe Kabila mara nyingi unahitaji yafuatayo)
Huenda Ndugu zetu wachagga kama wangepewa nchi yao na walivyo wengi leo hii lazima wangekuwa wanapiginia ardhi na kuangalia kama kila Ukoo / Sehemu ni kabila tofauti na hawana haki ya kuwepo sehemu husika. Na sijui ndugu zetu Wapare majirani zao nao wangekuwa nchi yao au wangekuwa Tanganyika na sijui kama wangekubali kwamba Wapare ni wa Kwetu Tanganyika na Sio Kilimanjaro. Na je ndugu zetu wa Kagera ? Uganda wangewachukua kama taifa lao iwapo wangekuwa nchi wangewezaji kumzuia Mganda bila msaada wa makabila mengine mia na zaidi ?
Kwahio binafsi naona pamoja na kazi nzuri ya Waasisi wa Taifa letu, lakini pia walikuwa na bahati (advantage) ya kwamba Tanzania ni Kubwa na hakuna mbanano hivyo wakati bado kuna wao na sisi kulikuwa na uwezekano wa wale wanaobanwa kuweza kusogea pengine na kujinafasi, bila hivyo mifarakano ingetokea
Hitimisho
Nadhani muingiliano (cohesion), ni muhimu sana na sababu tunaendelea kujaa na resources kupungua ni vema tukaendelea kuchangamana (kuingiliana) na kutengeneza machotora wa makabila tofauti tofauti ili hata siku tukishituka kwamba tumejaa na hapatoshi isiwepo uwezekano wa kusema wewe hapa sio kwako nenda kule (sababu pote patakuwa petu).

- Lugha yenu
- Ardhi / Eneo
- Utamaduni wenu, tofauti na wengine