Mfano wa Kuigwa: Mkusanyiko wa Makabila uliotengeneza Taifa Moja (Watanzania)

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Wakati majirani huko na kule wanabaguana ni vema wakachungulia huku na kujifunza. Vilevile na sisi tukachungulia kule ili kuona ni vipi tusijefanya makosa kama yao.

Sifa za Makabila; (Ili uwe Kabila mara nyingi unahitaji yafuatayo)
  • Lugha yenu
  • Ardhi / Eneo
  • Utamaduni wenu, tofauti na wengine
Mifarakano Mingi imekuwa ikitokea Iwapo Resources (Ardhi n.k) inaanza kuwa Chache (Kugombaniwa)
Huenda Ndugu zetu wachagga kama wangepewa nchi yao na walivyo wengi leo hii lazima wangekuwa wanapiginia ardhi na kuangalia kama kila Ukoo / Sehemu ni kabila tofauti na hawana haki ya kuwepo sehemu husika. Na sijui ndugu zetu Wapare majirani zao nao wangekuwa nchi yao au wangekuwa Tanganyika na sijui kama wangekubali kwamba Wapare ni wa Kwetu Tanganyika na Sio Kilimanjaro. Na je ndugu zetu wa Kagera ? Uganda wangewachukua kama taifa lao iwapo wangekuwa nchi wangewezaji kumzuia Mganda bila msaada wa makabila mengine mia na zaidi ?

Kwahio binafsi naona pamoja na kazi nzuri ya Waasisi wa Taifa letu, lakini pia walikuwa na bahati (advantage) ya kwamba Tanzania ni Kubwa na hakuna mbanano hivyo wakati bado kuna wao na sisi kulikuwa na uwezekano wa wale wanaobanwa kuweza kusogea pengine na kujinafasi, bila hivyo mifarakano ingetokea

Hitimisho
Nadhani muingiliano (cohesion), ni muhimu sana na sababu tunaendelea kujaa na resources kupungua ni vema tukaendelea kuchangamana (kuingiliana) na kutengeneza machotora wa makabila tofauti tofauti ili hata siku tukishituka kwamba tumejaa na hapatoshi isiwepo uwezekano wa kusema wewe hapa sio kwako nenda kule (sababu pote patakuwa petu).
 
Uoga wetu tu ndio unatusitiri bro
If that is the case bora dunia nzima wangekuwa waoga..., Mfano Watusi na Wahutu wangekuwa waoga (kama unavyosema) leo hii ndugu zao malaki kwa malaki wangekuwa hai wanasaidiana kujenga nchi yao bila makovu (instead ya leo wengine ni mafuvu katika museum)
 
Ubaguzi upo milele ila sio tabia nzuri ,kawaida ya ubaguzi kama wanaansa level ya ukabila basi hata koo ndani ya kabila moja zinabaguana ,mpaka level ya familia watu wanabaguana.

Tanzania ni washamba wachache bado wana hizo habari ila wengine tulishaachana nazo ,hamna ulazima wa kujua kabila la mtu ..Mtanzania anaweza kuishi popote ndani ya Tz kikubwa afuate taratibu wa kupata ardhi kihalali.
 
Kiini au chanzo kikuu cha kuwepo kwa Migogoro mingi Sana ya kibinadamu husababishwa na kukosekana kwa HAKI na kuwepo kwa DHULUMA na Uonevu.
Suala la Ukabila,, Ukanda, Udini, Ubaguzi, tofaufi za mitazamo ya Itikadi za Kisiasa, Nepotism, n.k ni factors saidizi tu katika vigezo vya kuweza kuwadhulumu Watu wengine Haki zao stahiki au kutoa Haki kwa Watu ambao hawastahili.
 
Hiyo level ya kuondowa ukabila kabisa miongoni mwa watanzania bado hatujafikia,kwa sababu watu baadhi hawawezi kumchaguwa mtu awe kiongozi mahali fulani kwa sababu tu siyo mzaliwa wa eneo hilo. Kwa hiyo kunahitajika Elimu zaidi
 
Huwa nawashangaa sana watu wanaomnanga Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, leo hii watanzania tuko tulivyo kwasababu tulichanganywa tukachangamana tukawa kama ndugu wa damu hatuna vita za kikabila
 
Na resources zinapokuwa chache watu wanaanza kutafuta sababu na ku justify kwanini wao wapate zaidi ya wengine yaani kwanini mimi nina haki kuliko wewe (all animals are equal but some are more equal than others); Mfano utumwa usingekwisha kama isingekuwa industrial revolution, sababu wachache wangetafuta moral grounds za kuwafanyisha kazi wengine ili wao wawanyonye...

Now kama tunatengana kwa Kipato (at least unaweza ukasema na mimi ninaweza kupata kipato) ila kama tunatengana kwa kitu ambacho sina uwezo wa kukibadilisha hapo ni kwamba mtu anakuwa hana hope maisha yake yote (unless awe brainwashed kwamba yeye yupo pale kutumikia wengine) basi lazima kitawaka....
 
Vipi kuhusu ubaguzi wa kisiasa??
 
Vipi kuhusu ubaguzi wa kiuchumi/kipato??
 
Hiyo level ya kuondowa ukabila kabisa miongoni mwa watanzania bado hatujafikia,
Kabila zibaki tu kama identity na uniqueness na watu kutaniana hapa na pale (hakuna ubaya wa utofauti) ndio maana hata maua yakiwa mengi sehemu yanafanana yakuwa sio maua bali magugu.., ila kuanza kuona kwamba tumpe mtu kitu / wafidha sababu ni kabila langu hivyo mwenzangu na yule sio mwenzangu ni upuuzi
kwa sababu watu baadhi hawawezi kumchaguwa mtu awe kiongozi mahali fulani kwa sababu tu siyo mzaliwa wa eneo hilo. Kwa hiyo kunahitajika Elimu zaidi
Naam huko ni kupotoka na wenzetu wakenya hii inawatafuna hadi kwenye Katiba yao yaani wanataka hata labda viongozi (mawaziri nao wawe kwenye makabila tofauti) yaani unaona kwamba kwanini wasukuma hatuna basi hata kama kipindi hicho kuna mazezeta unaamua kuweka mazezeta ili mradi tu namba zifike. Na kwenye hii topic hata usawa wa Jinsia sijui 50/50 kwenye uongozi naona ndio yale yale tu...
 
Vipi kuhusu ubaguzi wa kiuchumi/kipato??
Hapo inabidi kuwe na Haki yaani mtu asimyonye mwingine na Keki ya Taifa igawanywe kwa Haki yaani mtu apate atleast ujira wa kumuwezesha kuishi na kwenye hilo takupa points mbili moja kutoka kwenye Hotuba ya Mwalimu na nyingine Uzi wangu kuhusu Mwananchi ambavyo hatendewi haki...

  • CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake. Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA.
 
Huwa nawashangaa sana watu wanaomnanga Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, leo hii watanzania tuko tulivyo kwasababu tulichanganywa tukachangamana tukawa kama ndugu wa damu hatuna vita za kikabila
Naam msingi ulijengwa sasa kama tunashindwa kuweka kuta na madirisha tusilaumu waliojenga msingi; shortcoming zetu ni sababu yetu sasa hivi..., na kumbuka hawa waasisi hawakufuja mali hivyo walituachia urithi intact...

Kwahio ni kama unalaumu Babu yako kwa kuwa na vitukuu vyenye Chogo sababu alimuoa Bibi yako mwenye Chogo wakati wewe ulikuwa na uwezo wa kuoa mke kwenye Kichwa Bapa ili upunguze Chogo....
 
Vipi kuhusu ubaguzi wa kisiasa??
Suala la Politics binafsi naona lishakuwa Kama Simba na Yanga; Hivyo hata kama wao wanabaguana bado wanawabagua kina Pamba na Lipuli..., that said mimi kila siku nasema asset ya Tanzania ni Watanzania (Wananchi) na sio wanasiasa wala viongozi / walamba asali; if anything they are the ones letting us down..

Ndio maana kuna siku nilisema hata katika kujaribu kupata Habari / Madudu tusiwategemee bali tutafute alternative...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…