Mfano wa Serikali kama mfugaji na wafanyabiashara kama mifugo

Anganile1

Senior Member
Joined
May 15, 2014
Posts
148
Reaction score
4
Nitatumia mfano ili nieleweke. Serikali ni kama mfugaji, sekta binafsi (wafanyabiashara) ni kama mifugo, (mfano Ng'ombe) na fani ya ufugani iwe kama aina ya uchumi wa soko tuliochagua kuufuata. Mfugaji hawezi kuishi kama mfugaji bila kuwa na mifugo, na mifugo haiwezi kuishi bila mchungaji au mfugaji.
Kwa mchungaji anayejua kazi yake atahakikisha mifugo yake inapata chakula bora, maji, madawa, na banda bora ili aweze kukamua maziwa mengi na hata akiuza, auze bei nzuri yenye faida. Ni wendawazimu kutegemea kukamua maziwa mengi na kuuza bei nzuri mifugo ambayo haijapata huduma nzuri.

Serikali ni lazima iilee vema sekta binafsi. Ni muhimu zaidi kuwalea wafanyabiashara wadogo, wakishanyanyuka ndipo serikali iingie kukamua kodi yake (maziwa). Ni jambo la ajabu sana kuambiwa ulipe kodi hata kabla ya kuanza biashara. kama tukiendelea hivi, ni ngumu sana kwa mfanya biashara mdogo kupenyeza na kuwa mfanyabiashara mkubwa na kuwa Tajiri.
Sasa hivi tuna wimbo mtamu sana wa viwanda. Serikali isikae ikafurahia uwekezaji wa viwanda vikubwa unaofanywa na wageni. Mapinduzi ya viwanda yanafanywa na wazawa, sio wageni. Maana mgeni huja na kuondoka. uwekezaji wa mzawa huanza na viwanda vidogo vidogo, tunaendelea kuviboresha hivyo viwanda vidogo mpaka tunakuwa na viwanda vikubwa.

Mfano, Kama serikali ikaamua kuwajengea uwezo vijana wazawa vikaanzishwa viwanda vidogo 500. vijana hao wakasimamiwa hatua kwa hatua kuhakikisha malengo waliyowekewa yanatimia. Naamini baada ya miaka 10 tutakuwa na viwanda vikubwa sio chini ya 200 kati ya 500 vidogo vilivyoanzishwa. Tukifikia hapo Hatutakuwa na haja ya kuwaomba wawekezaji waje kujenga viwanda from zero. tutahitaji waje kununua shares ili tukuze mitaji ya viwanda vyetu.
Huu ni mtazamo wangu tu....
 
Huu Uzi mzuri, lakini cha kushangaza vijana wengi wamejazana kujadili maswala ya siasa na maswala ya uchumi wengi atujui hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…