Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mfanyabiashara, Novita Shirima (49) na dereva, Justine Mbise (29) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro wakikabiliwa na mashtaka sita, ikiwemo kumiliki kemikali aina ya ethanol kinyume cha sheria, kughushi stempu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutumia nembo bandia za bidhaa za vileo.
Wakili wa Serikali, Frank Wambura, amedai mahakamani hapo kuwa Oktoba 10, 2024, Shimud alikutwa na lita 310 za ethanol, pamoja na chupa zenye nembo bandia za k-vant, konyagi, na highlife. Washtakiwa wote wamekana mashtaka hayo.
Soma Pia: Matumizi ya Kemikali ya Ethanol yanaweza kuathiri ini na kusababisha Saratani
Upande wa mashtaka uliomba washtakiwa waendelee kushikiliwa, ukidai makosa hayo hayana dhamana. Hata hivyo, mawakili wa utetezi walidai wateja wao wanastahili dhamana kisheria.
Baada ya kupitia hoja za pande zote, Hakimu Mkisi aliruhusu dhamana kwa masharti ya wadhamini wawili watumishi wa serikali, dhamana ya Sh10 milioni kwa kila mmoja, na kiwanja chenye thamani ya Sh100 milioni ndani ya Wilaya ya Moshi. Kesi hiyo itatajwa tena Machi 5, 2025.