Mfanyabiashara: Royal Tour italeta mapinduzi ya kiuchumi Tanzania

Mfanyabiashara: Royal Tour italeta mapinduzi ya kiuchumi Tanzania

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Mfanyabiashara, Nathan Kimaro na mkazi wa jiji la Arusha amepongeza ujio wa Filamu ya Royal Tour ambayo imezinduliwa hivi karibuni hapa nchini akisema imekuja kufungua Uchumi wa Taifa kupitia sekta ya Utalii na kuwataka vijana kuchangamkia fursa za ajira .

Akiongea na vyombo vya habari jijini hapa, amesema Filamu hiyo inaonesha jinsi Tanzania ilivyobarikiwa na rasilimali nyingi pamoja na vivutio lukuki yakiwemo madini adimu duniani ya Tanzanite pamoja na wanyama asilia.

Kimaro ambaye pia ni Kada maarufu wa CCM jijini hapa,alimpongeza Rais Samia Suluhu kwa kuicheza vizuri filamu hiyo kwani alijitoa kuwatumikia watanzania ili kuionesha dunia ukarimu wa watanzania pamoja na vivutio mbalimbali vinavyopatikana hapa nchini.

Alisema Mara ya kwanz filamu ya Royal Tour lizinduliwa jijini Arusha na baadaye Zanzibar na Dar es Salaam ambapo watanzania wameipokea vizuri na wamekuwa nanimaji kubwa kuwa Utalii utakuwa mkubwa na kuongeza idadi ya watalii wanaoingia hapa nchini jambo litakaloongeza ajira kwa wananchi.

IMG-20220509-WA0239.jpg
 
Angekuwa Hana hela ningesema Hana akili, ila kada mfanyabiashara kusifia RT siyo ajabu.
 
Back
Top Bottom