Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Taarifa iliyotolewa leo December 14,2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumane Muliro imesema "Inadaiwa siku hiyo alionekana akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni majira ya saa 6:00 mchana kuelekea Mbagala, Bandari kavu alikodai anaenda kukagua kontena la bidhaa zake baada ya kuitwa na Watu aliodai ndiyo waliokuwa wanashughulika na kutoa kontena hilo bandarini na alikuwa akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe"
"Ufuatiliaji wa taarifa hiyo unafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ndugu ili kujua na kubaini Mtu huyo yupo wapi, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa yeyote mwenye taarita kuhusiana na Mtu huyo azitoe kwenye mamlaka yoyote ya Serikali illyo karibu yake"
Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Taarifa hiyo ya Polisi imekuja saa chache baada ya Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kutoa taarifa ya kupotea kwa Ulomi ambapo amesema aliondoka Sinza kwenda Mbagala Bandari kavu alipoenda kukagua kontena lake baada ya kuitwa na Watu wa TRA kwa ajili ya ukaguzi na namba yake ya simu aliyokuwa anaitumia ni 0653630313 "Ndugu zake wamemtafuta vituo vyote vya Polisi nakupewa.