Mfanyakazi wa NMG apatikana akiwa amekufa

Mfanyakazi wa NMG apatikana akiwa amekufa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mfanyakazi wa shirika la NMG aliyetoweka akielekea hospitalini apatikana City Mortuary akiwa maiti huku
Rekodi za hospitali zikionesha kuwa Akinyi hakuhudumiwa kwenye hospitali hiyo.

Mwili wa Mildred Akinyi Odira ambaye ni mfanyakazi katika shirika la utangazaji la Nation Media Group ulipatikana na familia yake Jumatatu Februari 4, katika kituo cha kuhifadhi wafu cha City Mortuary.

Akinyi alionekana mara ya mwisho na mlinzi wa makazi yake ambapo alimuomba amuitie dereva wa teksi ampeleke katika hospitali ya Ruaraka Uhai Neema Jumanne Januari 29.

Kulingana na dadake Maureen Anyango, Akinyi alikuwa akisumbuliwa ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na ugonjwa wa kisukari.

" Mwanawe Akinyi alikuja kwangu na nikashangaa mbona hajaenda shuleni siku hiyo, aliniambia kuwa mamake hakuwa nyumbani kwani alitoka mapema bila ya kumjulisha alikokuwa akielekea, hapo ndio tulijawa na wasiwasi na kuanza kumtafuta," Maureen alisema.

"Tulienda kwa nyumba yake na tukampata mlinzi kwenye lango aliyetuarifu kuwa Akinyi alichukua texsi akaenda katika hospitali ya Ruaraka Uhai Neema," Maureen aliongezea.

Maureen alienda hadi katika hospitali hiyo ila hakumpata na rekodi zilionyesha kwamba hakuhudumiwa katika hospitali hiyo.

Dereva wa teksi aliyembeba alisema alimfikisha Akinyi hospitalini humo na akaondoa dakika 20 baadaye, hata hivyo rekodi za hospitali hiyo zilionyesha kuwa alikawia katika hospitali hiyo kwa saa moja na dakika 27.

Dereva huyo alikamatwa na maafisa wa polisi na anasaidia katika uchunguzi ili kubaini kilichosababisha kifo cha Akinyi.


TukoNews
 
miss zomboko huu uandishi wa chini ya kiwango umeanza lini? Mara nyingi unaleta habari zimeshiba na kujitosheleza, wachache sana wataweza kubaini hili tukio limetokea nchi gani na huyo mhusika ni nani hasa licha ya kumtaja kama mfanyakazi wa NMG.

Jitahidi kuendeleza kazi nzuri unayoifanya na kuboresha zaidi weledi.

cc beth
 
miss zomboko huu uandishi wa chini ya kiwango umeanza lini? Mara nyingi unaleta habari zimeshiba na kujitosheleza, wachache sana wataweza kubaini hili tukio limetokea nchi gani na huyo mhusika ni nani hasa licha ya kumtaja kama mfanyakazi wa NMG.

Jitahidi kuendeleza kazi nzuri unayoifanya na kuboresha zaidi weledi.

cc beth
Hata mimi naona mapichapicha, sijaelewa kabisa tukio ni la Nchi gani na marehemu ni nani hadi aandikwe humu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari haieleweki sijui hawajui kiswahili au ndo wanavyoelewana wao kwa wao!!
 
Back
Top Bottom