Mfikishieni salamu mkuu wa mkoa (RC) Singida

Mfikishieni salamu mkuu wa mkoa (RC) Singida

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
282
Reaction score
561
Naandika kwa masikitiko sana, Mimi ni mwenyeji wa Singida ila kishughuli naishi Dar es salaam najishughulisha na shughuli za ulinzi binafsi (bodyguard) hivyo huwa tunazunguka na wateja wangu sehemu mbalimbali (wanamuziki, wafanyabiashara, wanamichezo, wanasiasa nk).

Moja ya sehemu tunazotembelea sana ni sehemu za burudani vilabu vya usiku, kwenye na baa nk, nimesikitika sana kwa miaka hii miwili kumekuwa na idadi kubwa ya wasichana kutoka Singida ama wanyaturu ama wanyiramba wenye umri wa kuanza kidato cha kwanza wakiwa wanatoa huduma katika sehemu hizo za starehe hii inaleta tafsiri kwamba kuna genge la biashara haramu ya wasichana hao mkoa ni Singida ambalo linashawishi wazazi kuwa msichana katika umri wa Miaka 14 na kuendelea anaweza kwenda Dar na kupata ajira nasikitika mkoa wa Singida leo umekuwa kitovu cha kusambaza ma baa maid tena wenye umri wa kwenda shule.

Miaka ya nyuma nakumbuka mkoa wa Iringa ulikuwa maarufu kwa kusambaza wasichana wa ndani (house maid) hongera RC Iringa kwa kuhakikisha watoto wa kike wanaenda shule sikatai ma watoa huduma wengi kwenye baa kuwa wanasingida basi angalau wawe na miaka ya kiutu uzima na biashara ya udalali wa watoto ukomeshwe
 
Wamesambazwa zaidi maeneo gani Mheshimiwa Bodyguard ili Serikali yako sikivu iendeshe msako wa kuwabaini? Usitaje majina ya hizo Bar!! Wewe taja tu maeneo, inatosha!😇
 
Wamesambazwa zaidi maeneo gani Mheshimiwa Bodyguard ili Serikali yako sikivu iendeshe msako wa kuwabaini? Usitaje majina ya hizo Bar!! Wewe taja tu maeneo, inatosha![emoji56]
Mkuu acha atutajie walau Bar mbili tu tukamalizie w/end hapo[emoji39]
 
Baa za fukweni na zinazotoa Huduma za chakula utawatambua wanalafudhi kama ya kaskazini hivi ila maumbo yao sasa dah
 
Back
Top Bottom