Naona wakati tunaendelea kuchambua hoja za wabunge na fuko lao hilo la Jimbo pamoja na kwamba serikali ya CCM iliuzika rasmi ukweli na busara, hekima vilivyokuwamo ndani ya AZIMIO LA ARUSHA kupitia Azimio batili na la kihaini la Zanzibar ukweli unabakia pale pale! Tuendelee kukumbushana na hapa naomba kuwashushieni kipande kimoja toka katika AZIMIO LETU TUKUFU LA ARUSHA
Mnyonge hapigani kwa Fedha:
Lakini ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua
silaha; kwani silaha tuliyochagua ni fedha. Tunataka kuondoa
unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo
sisi wenyewe hatuna. Katika mazungumzo yetu, mawazo yetu, na
vitendo vyetu ni kama tumekata shauri kwamba bila fedha mapinduzi
yetu hayawezekani. Ni kama tumesema, "Fedha ndiyo msingi wa
maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo"!
Hii ndiyo imani yetu ya sasa. Viongozi wa TANU mawazo yao ni
kwenye fedha. Viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi,
mawazo yao na matumaini yao ni kwenye fedha. Viongozi wa
wananchi na wananchi wenyewe katika TANU, NUTA, Bunge, UWT.,
Vyama vya Ushirika, TAPA na makundi mengine ya wananchi,
mawazo yao na maombi yao na matumaini yao ni FEDHA. Ni kama
wote tumekubaliana na tunasema kwa sauti moja, "Tukipata fedha
tutaendelea, bila fedha hatutaendea"!
Mpango wetu wa maendeleo ya miaka mitano shabaha zake
kwa kifupi ni shibe zaidi, elimu zaidi na afya zaidi. Na silaha yetu
tuliyotilia mkazo sana ni fedha. Ni kama tumesema, "Katika miaka
mitano ifuatayo tunakusudia kujiongezea shibe, elimu na afya, na ili
kutimiza shabaha hizo tunatumia $ 250,000,000". Kama tumetaja na
tunapotaja vyombo vingine vya kututimizia shabaha hizo tunavitaja
kama nyongeza tu; lakini chombo kikubwa katika akili zetu, silaha
kubwa katika mawazo yetu, ni FEDHA.
Mheshimiwa Mbunge anaposema kuwa wananchi wa sehemu
yake wana shida ya maji, je Serikali ina mpango gani wa kuondoa
shida hiyo? Jibu analotaka ni kwamba: Serikali inao mpango wa
kuwapa maji wananchi wa sehemu hiyo – KWA FEDHA.
Mbunge mwingine anaposema kuwa sehemu yake haina
barabara au shule au hospitali au vyote, je, Serikali ina mpango gani?

Naye pia jibu ambalo angependa kupewa ni kuwa Serikali inao
mpango safi kabisa wa kutengeneza barabara au kujenga shule au
hospitali au vyote kwa wananchi wa sehemu ya Mbunge Mheshimiwa
huyo - kwa FEDHA.
Kiongozi wa NUTA anapoikumbusha Serikali kuwa mishahara ya
chini kwa wafanyakazi wengi bado ni midogo mno na nyumba
wanazolala si nzuri, je, Serikali inao mpango gani? Jibu apendalo
kusikia ni kuwa Serikali inao mpango maalum wa kuongeza
mishahara na kujenga majumba bora - KWA FEDHA.
Kiongozi wa TAPA anaposema kuwa wanazo shule nyingi sana
ambazo hazipati msaada wa Serikali. Je Serikali ina mpango gani wa
kuzisaidia shule hizo, jibu analopenda kusikia ni kuwa Serikali iko
tayari kabisa kesho asubuhi kuzipa shule hizo msaada unaotakiwa -
wa FEDHA!
Kiongozi wa Chama cha Ushirika akitaja shida yo yote ya
mkulima jibu apendalo kusikia ni kuwa Serikali itaondoa shida hizo za
mkulima – kwa FEDHA. Mradi kila shida inayolikabili Taifa letu
wananchi tunawaza Fedha, Fedha, Fedha!
Mwaka hata mwaka kila Wizara na kila Waziri hufanya
makadirio yake ya matumizi – yaani fedha wanazohitaji mwaka huo
kwa kazi za kawaida na mipango ya maendeleo. Waziri mmoja tu na
12
Wizara moja tu hushughulikia pia kufanya makadirio ya mapato. Ni
Waziri wa Fedha. Kila Wizara ina mipango mizuri sana ya
maendeleo. Wizara zinapoleta makaidirio yao ya matumizi huwa
zinaamini kwamba fedha zipo ila mkorofi ni Waziri wa Fedha na
Wizara yake. Na kila mwaka lazima Waziri wa Fedha na Wizara yake
awaambie Mawaziri wenzake na Wizara zao kwamba hakuna fedha.
Na kila mwaka Wizara zote huinung'unikia Wizara ya Fedha kwa
kupunguza Makadirio yao ya matumizi.
Kadhalika Wabunge na Viongozi wengine wanapodai Serikali
itimize mipango mbali mbali huwa nao wakiamini kwamba fedha zipo
ila mkorofi ni Serikali. Lakini kukataa huku kwa Wizara, na Wabunge
na Viongozi wengine hakuwezi kuondoa ukweli; nao ni kwamba
Serikali haina fedha.
Na kusema kuwa Serikali haina fedha maana yake ni nini?
Maana yake ni kuwa Wananchi wa Tanzania hawana fedha. Kiasi
walichonacho hutozwa kodi, na kodi hiyo ndiyo inayoendesha
shughuli za Serikali hivi sasa na maendeleo mengine ya nchi.
Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha
tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha
zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi.
Ukidai Serikali itumie fedha zaidi unataka izipate; na njia ya
kuzipata ni kodi. Kudai Serikali itumie fedha nyingi bila kukubali kodi
13
zaidi ni kudai Serikali ifanye miujiza; ni sawa na kudai maziwa zaidi
bila kutaka Ng'ombe akamuliwe tena. Lakini kukataa huku kukiri
kwamba tunapodai Serikali itumie fedha zaidi nia yetu ni kutaka
Serikali iongeze kodi kunaonyesha kuwa tunatambua ugumu wa
kuongeza kodi. Tunatambua kuwa ng'ombe hana maziwa zaidi;
kwamba hata ng'ombe mwenyewe angependa ayanywe maziwa hayo
au yanywewe na ndama wake au yauzwe yamfae yeye na jamaa
yake; utashi huo hauwezi kuondoa ukweli kwamba hana maziwa
zaidi.
AZIMIO LA ARUSHA 1967