Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wafanya mkutano na watoa huduma za mawasiliano Dar

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wafanya mkutano na watoa huduma za mawasiliano Dar

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
969
Reaction score
1,055
Mhandisi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Bw. Shirikisho Mpunji akielezea juu ya namna ya Utekelezaji wa Miradi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo amesema Miradi hii imegawanyika katika Makundi Makuu mawili ambayo ni:

1. Miradi ya Mawasiliano ya Vijijini ambayo kimsingi Mfuko unafanya kazi kwa kushirkiana na watoa huduma za Mawasiliano kwa kupeleka na kufanikisha huduma za Mawasiliano Vijijini na Maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.

2. Miradi mingine pamoja na:
  • Mradi wa vifaa vya TEHAMA na kuunganisha shule kwa mtandao wa intaneti
  • Tiba Mtandao (Telemedicine)
  • Matangazo ya Kidigitali ya Runinga (Digital Broadcasting)
  • Mafunzo ya TEHAMA kwa walimu
  • Wasichana na TEHAMA
  • Mradi wa kuboresha matangazo ya TBC maeneo ya mipakani
Aidha Mhandisi Mpunji amesema kuwa Mfuko umeendelea kutekeleza Mradi wa kuiongezea uwezo (upgrade) Minara 77 iliyokuwa katika teknolojia ya 2G pekee ili iweze kutoa huduma ya intaneti kwa kiwango cha 3G na 4G ambapo amesema watoa huduma wameanza kutekeleza Mradi huu na unatarajiwa kukamilika Mwezi Desemba Mwaka huu 2021.

Leo Septemba 09/2021
Picha jmizungu
# SeminaUtoajiElimu
# MfukoWaMawasilianoKwaWote
# KichocheoChaUchumiWaKati
 
Visekta vingine bana vipovipo tu. Haka kamfuko hata hakajulikani kanafanya nini.

Kuna wakati Magufuli alitaka kukasambaratisha kawe kakitengo tu ndani ya TTCL, aliona hakana kazi ya kufanya.
 
Back
Top Bottom