BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Gharama za uendeshaji kwa Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) zimepungua kutoka Sh128.93 bilioni kwa mwaka 2018 hadi kufikia Sh68.83 bilioni mwaka huu sawa na asilimia 46.61. Kupungua kwa gharama hizo kunatokana na hatua ya uunganishaji wa mifuko ya pensheni minne ya PSSF, LAPF, PPF na GEPF mwaka 2018.
Hayo yamesemwa leo Jumatano Novemba 9, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo na utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23. Amesema licha kupunguza gharama uunganishaji huo, umenusuru udororaji wa mifuko na kuongeza ufanisi wa mfuko huo katika utoaji wa huduma.
“Baada ya taratibu zote kukamilika, Mfuko wa PSSSF ulianza kazi rasmi Agosti Mosi mwaka 2018. Thamani ya mfuko mwaka 2018 ilikuwa ni Sh5.86 trilioni na hadi kufikia Septemba 30, 2022 thamani ya mfuko imefikia Sh7.72 trilioni,”amesema.
Amesema mafanikio mengine pamoja na mambo mengine changamoto kubwa zilikuwa kwenye maeneo ya kulipa watumishi 10,273 waliokuwa hawajalipwa tangu kwenye mfuko mmoja wapo wa kati ya iliyounganishwa. Amesema PSSSF ililipa mafao yaliyorithiwa ya Sh1.02 trilioni ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
MWANANCHI