Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Mfumko wa bei umegonga rekodi mpya katika nchi 19 za ukanda unaotumia sarafu ya Euro. Hali hiyo imesababishwa na ongezeko kubwa la bei ya mafuta kufuatia vita nchini Ukraine. Katika mwezi huu wa Aprili, mfumko wa bei umefikia asilimia 7.5 kiwango ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu zilipoanza kutolewa takwimu mwaka 1997. Bei za mafuta zimepanda na kupindukia asilimia 38, hali ambayo inadhihirishwa namna ambavyo vita vimeathiri bei ya nishati duniani na kusababisha hali mbaya kwa wakaazi milioni 343 wa kanda inayotumia sarafu ya Euro. Khofu kwamba vita vya Urusi nchini Ukraine huenda vikasababisha kukatizwa usambazaji wa mafuta au gesi kutoka Urusi imechochea bei za mafuta na gesi asilia kupanda zaidi.
Note.Nchi mmoja inasababisha mgogoro wa kiuchumi katika Nchi tajiri zaidi Duniani,na Ulimwengu kwa ujumla-halafu anatokea Mtanzania wa Kigurunyembe anakwambia Urusi sio chochote-khaaa.
# Urusi sio Lesotho!