ONESMO LAURENT MBILIZI
New Member
- May 3, 2024
- 2
- 5
Kwa nini kumekuwa na wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana hasa wahitimu wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla? Migogoro bungeni, wazazi kwa vijana, vijana na jamii kwa ujumla juu ya ukosefu wa ajira kwa vijana. pia utegemezi mkubwa wa bidhaa kutoka mabara ya dunia ya kwanza.
je nini kifanyike kuondoa au kupunguza hali hii?
1. Serikali iweke vipaumbele katika masomo ya kimkakati yenye muunganiko wa moja kwa moja wa masomo na ujuzi katika kazi husika ili kutimiza mahitaji ya jamii kwenye elimu katika kuhakikisha ukosefu wa ajira unapungua, kukuza teknolojia yetu na kuzalisha bidhaa zetu.
(a) Masomo hayo yatafundishwa baada ya elimu ya awali hadi ngazi ya chuo kikuuu, wanafunzi watatakiwa kupewa ujuzi katika eneo maalumu la kazi kuanzia ngazi za chini kwa mfano masomo ya uchakataji wa madini na nishat, masomo ya afya, miundombinu na tekinolojia, masomo ya kilimo na biashara.
(b) Kuwepo na somo la teknolojia na tehama linalo jitegemea pia liwe somo la lazima kwa kila mwananfunzi na kila hatua ya elimu kulingana na ujuzi wa kazi katika masomo husika.
2. Kuwepo na sera ya kupeleka vijana njee ya nchi kwa ajili ya kujifunza ujuzi kwenye sekta zao kutoka mataifa yanayo fanya vizuri kwenye sekta husika.
Faida au umuihimu wa mfumo huu wa elimu.
Hivyo basi ni weajibu wa serikali kutenga bajeti toshelevu kuhakikisha misingi bora ya elimu ina anzishwa kwasababu maendeleo makubwa ya kiuchumi yatatokana na ubora katika elimu.

Hivyo basi ni ukweli usio pingika kwamba, lazima serikali na wadau mbalimbali wa kimaendeleo kujidhatiti na kutambua kwamba nyumba imara hutokana na msing imara. kuna haja kubwa ya kufanya mageuzi makubwa katika secta ya elimu kwa kubadilisha mifumo iliyopo ili kuendana na uhitaji wa jamii.
Tumeona ni miaka mingi sasa imepita tangu nchi yetu imepata uhuru na inashangaza hada sasa kuona nchi yetu inategemea bidhaa nyingi hasa za kitekinolojia kutoka nje huku tukilia ukosefu wa ajira. Je nikweli sisi siyo wabunifu? Je nikweli hatuwezi zalisha bidhaa zetu? Je hatuna malighafi? Je elimu tuliyo nayo haina msaada kabisa? jibu ni hapana uwezo tunao tena mkubwa tukijidhatiti na kusimama kwa pamoja kw kurekebisha mifumo ya elimu.
Inawezekanaje nchi kama Tanzania licha ya kuwa na maliasili muhimu sana zinazo hitajika kwenye uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa mahitaji ya kawaida na mahitaji ya sekta muhimu kama vile afya, miundombinu, na tehama huku wasomi wengi walio jaa mitaani wakilia ukosefu wa ajira? Siyo makosa yao bali ni msingi wa elimu yao inayo wafunga wasiweze kufikiria zaid nje ya boksi. Hii ni kwasababu elimu walio ipata haikujikita zaidi kwenye vitendo na kutoa wasomi wenye uwezo mdogo wa kibunifu katika taaluma zao.
Kwahiyo basi nini kifanyike? Zifuatazo ni hoja za msingi kutekelezwa ili kuondokana na changamoti hii:
Tumeona ni miaka mingi sasa imepita tangu nchi yetu imepata uhuru na inashangaza hada sasa kuona nchi yetu inategemea bidhaa nyingi hasa za kitekinolojia kutoka nje huku tukilia ukosefu wa ajira. Je nikweli sisi siyo wabunifu? Je nikweli hatuwezi zalisha bidhaa zetu? Je hatuna malighafi? Je elimu tuliyo nayo haina msaada kabisa? jibu ni hapana uwezo tunao tena mkubwa tukijidhatiti na kusimama kwa pamoja kw kurekebisha mifumo ya elimu.
Inawezekanaje nchi kama Tanzania licha ya kuwa na maliasili muhimu sana zinazo hitajika kwenye uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa mahitaji ya kawaida na mahitaji ya sekta muhimu kama vile afya, miundombinu, na tehama huku wasomi wengi walio jaa mitaani wakilia ukosefu wa ajira? Siyo makosa yao bali ni msingi wa elimu yao inayo wafunga wasiweze kufikiria zaid nje ya boksi. Hii ni kwasababu elimu walio ipata haikujikita zaidi kwenye vitendo na kutoa wasomi wenye uwezo mdogo wa kibunifu katika taaluma zao.
Kwahiyo basi nini kifanyike? Zifuatazo ni hoja za msingi kutekelezwa ili kuondokana na changamoti hii:
1. Serikali iweke vipaumbele katika masomo ya kimkakati yenye muunganiko wa moja kwa moja wa masomo na ujuzi katika kazi husika ili kutimiza mahitaji ya jamii kwenye elimu katika kuhakikisha ukosefu wa ajira unapungua, kukuza teknolojia yetu na kuzalisha bidhaa zetu.
(a) Masomo hayo yatafundishwa baada ya elimu ya awali hadi ngazi ya chuo kikuuu, wanafunzi watatakiwa kupewa ujuzi katika eneo maalumu la kazi kuanzia ngazi za chini kwa mfano masomo ya uchakataji wa madini na nishat, masomo ya afya, miundombinu na tekinolojia, masomo ya kilimo na biashara.
(b) Kuwepo na somo la teknolojia na tehama linalo jitegemea pia liwe somo la lazima kwa kila mwananfunzi na kila hatua ya elimu kulingana na ujuzi wa kazi katika masomo husika.
2. Kuwepo na sera ya kupeleka vijana njee ya nchi kwa ajili ya kujifunza ujuzi kwenye sekta zao kutoka mataifa yanayo fanya vizuri kwenye sekta husika.
Faida au umuihimu wa mfumo huu wa elimu.
- Mfumo huu utasaidia kukuza ubunifu na tafiti bora; Ujuzi na utaalamu katika masomo mahususi kwenye kazi husika itasaidia kujifunza kwa undani na kuwawezesha wasomi kuwa na uwezo mkubwa wa kibunifu na kufanya tafiti zenye tija zaidi
- somo la tekmolojia kuwa somo la lazima itasaidia wataalamu kurahisisha kazi na kuongeza ufanisi mkubwa, kwani teknolojia ni muhimu kwa kila sekta.
- Itasaidia kukuza viwanda vya kati, vya chini na vya juu, kwa sababu wahitimu watakua na ujuzi mkunwa katika elimu yao kwa vitendo zaidi
- Itasaidia kuongeza fursa za kazi.

Upvote
12