SoC02 Mfumo dume kuisha,labda ibilisi ajitokeze Posta akila dafu

SoC02 Mfumo dume kuisha,labda ibilisi ajitokeze Posta akila dafu

Stories of Change - 2022 Competition

Bosi Kalewa

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
7
Reaction score
4
MFUMO DUME KUISHA LABDA IBILISI AJITOKEZE POSTA AKILA DAFU

Kikao cha mama zetu kina Gatrude kule Beijing. Hawakuchonga funguo ya ukatili dhidi ya watoto wa kiume. Lengo lilikuwa jema juu ya kumuinua mwanamke.

Lakini leo mtazamo ni hasi kwenye mchakato wa kumuinua mtoto wa kike. Kwa makusudi tunamtenga wa kiume ili wa kike ainuke. Hapa kama jamii tunakosea.

Tunapoujengea ubora wa upande wa kike, tuisibomoe ubora wa upande wa kiume. Wote wasitirike na ni haki yao wote waheshimike. Ubora wa Malkia ni uimara wake Mfalme.

Kikeni jiamini, jiheshimuni, ongezeni na utii. Kiumeni wajibikeni, lindeni na upendo zidishenii. Jamii kwa ujumla (Afrika) kuna pahala tulichomoa betri ya fikra kitambo.

Wa kiume akiwa na wapenzi wengi ni sifa kwa pande zote kama rijali. Wa kike akiwa hivyo atapewa sifa mbaya na pande zote kama malaya. Hii ipo kiasili na siyo bahati mbaya.

Mfumo dume upo duniani miaka tele. Toka enzi za Manabii. Siyo kazi rahisi kuumaliza kwa karne moja haraka. Tunapoenda haraka ndipo tunajikuta tukiua ubora wa mtoto wa kiume.

Matokeo wa kiume kakosa uangalizi. Dunia ipo na wa kike zaidi, wa kiume ni kama mgeni wa dunia ambayo ipo makini na ujenzi wa ubora wa kikeni.

Ni kweli mke si chombo cha starehe ya mume. Lakini pia tuachene na kauli za "Wanawake ni dhaifu. Sijui ni jeshi kubwa, ana moyo wa kiume nk." Hizi ni lugha baguzi zenye nadharia ya sifa njema.

Kaka akimtuma dada kwa mpenzi wake haina shida. Lakini kaka akijua tu kuwa dada ana mpenzi ni shida kubwa kwa dada na mtu wake.

Wahudumu wa kiume hawavai sare za vifua wazi. Ila wa kike huvalishwa vivazi vya kuvutia wateja. Hufanya kazi mbili kwa mshahara mmoja.
Kuhudumia na kuvutia wateja.

Wakike wakijiuza hupewa jina baya. Wateja wao wa kiume hawaguswi.
Ndoa ikivunjika jamii ya pande zote husema mke kaachika. Hata kama mume ndo kaachwa.

Viti maalum kwa wa kike bungeni. Ni dhahiri serikali zinahalalisha dhaifu wa mtoto wa kike kimuundo. Kuwa hawezi kujipambania bila kushikwa na wa kiume.

Hata majumbani, mtoto wa kike atapewa chumba jirani na wazazi wake. Lakini wa kiume atatengwa mbali ama kupewa chumba nje ya nyuma.

Matokeo yake ni wa kike kutambua nafasi yake kupitia ukaribu wake na wazazi. Na wa kiume kujikuza holela bila kutambua nafasi yake kwa kukaa mbali na wazazi.

Ndo chanzo cha 'umarioo', kutojua wajibu wao kifamilia. Wakijikuza bila kujua jinsi yake iwajibike vipi katika familia. Wanakaa mbali na kioo cha kujitazamia ambao ni baba zao.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom