Mo mzalendo
New Member
- Nov 10, 2021
- 1
- 1
Elimu ni nyenzo kuu ya kukuza ujuzi na ubunifu kwa vijana katika taifa na dunia kwa ujumla.Ili taifa liendelee linatakiwa kuwa na vijana wenye ujuzi wa hali ya juu katika kutatua changamoto mbalimbali na kuchagiza mabadiliko katika nyanja za uchumi, siasa, utamaduni,kijamii,sayansi,telnolojia na nyanja zote za maisha ya mwanadamu.Tanzania ni taifa lenye maono chanya katika maendeleo lakini limesahau umuhimu wa elimu katika kukuza maendeleo ya nchi yetu.
Mfumo wa elimu wa Tanzania umeoteshwa mizizi ya mfumo wa ukoloni na kuzidi kumea.Elimu kwa Tanzania ya sasa inamjenga kijana kuwa tegemezi zaidi kuliko kujitegemea kama ilivyokuwa kipindi cha ukoloni kwani serikali haiwaandalii vijana mazingira mazuri ya kuwawezesha vijana waliopata elimu kuwa wabunifu na kukuza bunifu zao. Sera ya elimu nchini ipo kufikisha elimu kifikra na sio kiutendaji jambo ambalo linadidimiza taifa katika kukuza ujuzi wa utendaji kwa vijana. Mfano kijana anasoma kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu darasani kwa kuhusisha mafunzo machache sana ya vitendo ambayo mengi yao hayamuandai kijana kujikwamua yeye mwenyewe bali yanamuandaa kutafuta ajira ya yeye kutumikia alichofunzwa.
Utegemezi wa wasomi wa mataifa mengine unadidimiza ubunifu na ujuzi wa vijana wasomi wa taifa letu.Serikali imekua ikihimiza wanafunzi wengi kusoma masomo ya sayansi na teknolojia jambo ambalo limejenga fikra za uwepo wa fursa za ajira katika kozi za masomo ya sayansi.katika mfano halisi tunaona vijana wengi wakiwa wanasoma kozi za sayansi na teknolojia kama vile uhandisi lakini je kuna nafasi za wao kujiajiri au kuajiriwa? jibu ni hapana kwani tunaona wasomi wa kozi za sayansi na teknolojia kutoka mataifa kama China na Uturuki wakilihudumia taifa katika ujenzi wa taifa letu wenyewe na kukosesha ajira vijana wazawa wa taifa.
Mfumo wa elimu nchini ni kandamizi kwani vijana wanatumia muda mrefu Katika masomo Kuanzia darasa la awali hadi elimu ya juu bila tija kwa taifa na wao wenyewe kwani muda mwingi wanaotumia katika elimu uliwafaa kukuza bunifu zao na vipaji vyao. Mfano hai ni kulinganisha vijana wanaosoma nchi za magharibi na wanaosoma nchi ya Tanzania,vijana wanaosoma nchi za magharibi hawatumii muda mrefu katika masomo yao na hivyo kupata wakati mzuri wa kukuza vipaji vyao tofauti na vijana wa taifa letu.
ATHARI ZINAZOPATIKANA KWENYE MFUMO WETU WA ELIMU.
Baadhi ya Athari ni za wazi kutokana na mfumo wetu kandamizi wa Elimu.
I. Kutumia muda mrefu kujifunza vitu ambavyo having tija kwa mwanafunzi,kuanzia darasa la chekechea mpaka kidato cha sita ni takriban miaka 15 ambayo kijana anajifunza mambo mengi ambayo kimsingi haji kuyatumia katika maisha yake ya kila siku.
ii. Kukosa ubunifu na ujuzi ambao utamsaidia kuendeleza maisha yake,ndani ya takriban miaka 15 ya kuwepo darasani kwa masikitiko kijana anaweza kumaliza kidato cha sita bila ya kuwa na ujuzi wala ubunifu ambao utamsaidia hii ni kutokana na kukaririshwa vitu vingi ambavyo having msaada wa moja kwa moja.
iii. Urudiaji wa mada(repetition of topics) wakati wa kujifunza,bado mfumo wetu unaruhusu upotevu wa mda kwa kuruhusu mada rejea kwa mfano kweny somo la hisabati kijana akiwa darasa la tano atasoma algebra akifika la sita atasoma tena algebra akiingia kidato cha pili atasoma tena algebra na kidato cha tano pia atarudia algebra, kadhalika kwenye somo la tehama darasa la sita utasoma "Introduction of Computer and input and output devices" lakini utazisoma tena hizo mada utapokuwa kidato cha kwanza na pia kidato cha tano.
iv. Mmomonyoko wa Maadili na mila za kitanzania,Elimu yetu inamfanya mtoto kutojali maadili na kutojua mila zake,hii ni kutokana na mda mwingi ambao atakaa darasani bila kukumbushwa juu ya maadili jambo ambalo mzaz anatakiwa awajibike kwa kiasi kikubwa ila kutokana na mwingi wa kuwepo darasani mzazi anakosa hiyo fursa.
MABORESHO YANAYOPASWA KUFANYWA KWENYE MFUMO WETU WA ELIMU
Serikali inapaswa kuhakikisha mikakati na utekelezaji mzuri kama vile:-
I. Kupunguza Muda wa kukaa darasani ili kuhakikisha mtoto anapata mda mzuri wa kupata maarifa ya ziada katika maisha,muda wa miaka 15 darasani ni mkubwa sana hivyo serikali inapaswa kuweka muda kiasi cha miaka 10 tu kukamilisha elimu ya shule.
ii. Kuweka mikakati ya kumjenga kijana kuwa mbunifu na mwenye ujuzi ili kufikia Tanzania tunayoitaka kwa kuweka elimu ya ufundi aina zote kuanzia ngazi ya awali.
iii. Kutokuwepo urudiaji wa mada kila mwaka,hii itasaidia kupunguza wingi wa madarasa na hivyo kumuwezesha kijana kupata mda sahihi wa kupata ujuzi na kuwa mbunifu.
iv. Kulinda mila na desturi zetu, hii ni kutokana na kumuwezesha kijana kumaliza shule akiwa na umri mdogo jambo ambalo litamsaidia mzazi kupata mda wa kutosha kumfundisha.mtoto mambo ya msingi kwenye mila, desturi na maadili.
Ili kuifanya Tanzania miongon mwa nchi zitakazo endlea kwa kasi basi serikali inaweza kuleta Maboresho ili kumfanya kukuwa katika misingi ya ujuzi ili kupunguza wimbi la malalamiko ya ajira na hili linawezekana kwan kama serikali imeweza kuwainua watoto wadogo kwenye siasa(CHIPUKIZI) basi pia inaweza kwenye suala zima la kukuza vijana kwenye mfumo wa teknolojia.
Mwisho niiombe serikali pamoja na watu binafsi hususani vijana kupambania mfumo mpya wa elimu usiofuata nyayo za kikoloni kwani mfumo ulokuwepo ni mfumo wa zamani ambao unaendana na katiba ilokuwepo, hivyo niwatake vijana wenzangu kudai mfumo mpya wa elimu kabla ya katiba mpya kwani Elimu ndiyo msingi wa maisha

Upvote
5