A
Anonymous
Guest
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanatuangusha Watanzania kwenye huu mfumo wao wa TANCIS ulioboreshwa tangu wamezindua Jumatatu imekuwa inasumbua sana hasa kwa Mawakala wa Forodha kwenye uondoshaji wa mizigo ya Wateja Bandarini.
Tunaomba werekebishe kuokoa muda na fedha za Watanzania.
Pia soma ~ TRA: Tumepokea maoni kuhusu changamoto za Mfumo wa TANCIS, yanafanyiwa kazi
================================
Tujikumbushe Uzinduzi wa TANCIS ulivyokuwa Januari 20, 2025
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua Tovuti mpya na mfumo wa TANCIS ulioboreshwa utakaosaidia kurahisisha uondoshaji wa shehena Bandarini, katika Viwanja vya Ndege pamoja na mipakani.
Akizindua mfumo huo leo tarehe 20.01.2025 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya TRA Bw. Mussa Abas Uledi amesema mfumo wa TANCIS utapunguza kuonana kwa watu baina ya TRA na Walipakodi ambapo shughuli zote zitafanyika mtandaoni huku Tovuti mpya nayo ikirahisisha upatikanaji wa taarifa.
Bw. Uledi amesema mfumo wa TANCIS ulioboreshwa utasaidia kuongeza mapato ya TRA kwa upande wa Forodha kutokana na shughuli zote za ukadiriaji wa Kodi utafanywa na mfumo kwa usawa.
Amesema mfumo huo umeunganishwa na mifumo 36 ya taasisi nyingine na kuzitaka taasisi zilizounganishwa na mfumo huo kuhakikisha mifumo hiyo inasomana kiutendaji.
Amebainisha kuwa kumekuwa na changamoto kadhaa na malalamiko ya wadau kupitia utolewaji huduma kwa kuonana hivyo uwepo wa mfumo utafanya watu wasionane na kuzifanya Bandari za Tanzania na vituo vya Mipakani viwe bora katika kutoa huduma kwenye ukanda huu na hili litachagizwa na mfumo wa TANCIS.
Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesem mfumo wa TANCIS ulioboreshwa unakwenda kujibu matakwa ya watumiaji wa mfumo huo na kuboresha utendaji kazi wa TRA kwa upande wa Forodha.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema mfumo huo utasaidia sana kupunguza muda wa kufuatilia mizigo inayoingizwa nchini kutoka sehemu mbalimbali maana mfanyabiashara ataweza kuzifikia taasisi nyingi kwa wakati mmoja kwa kutumia mfumo bila kutoka Ofisini kwake na kuwafuata.
Kamishna Mkuu Mwenda amesema mfumo wa TANCIS utaleta usawa katika kulipa Kodi ambapo kila mmoja ataweza kujua anapaswa kulipa kiasi gani kwa kutumia mfumo jambo ambalo litaongeza ukusanyaji wa Kodi.
Amesema mfumo wa TANCIS umegharimu zaidi ya Sh. Bilioni 100 katika ujenzi wake lakini faida zake ni kubwa sana kuliko gharama iliyotumika maana utaleta mapinduzi ya kiutendaji.
Kuhusu Tovuti mpya ya TRA Bw. Mwenda amesema Walipakodi wataweza kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na TRA na kupatiwa majibu kwa mambo watakayouliza.