SoC04 Mfumo na utaratibu wa urasimishaji ardhi uboreshwe ili kuongeza Ufanisi na kuepukana na migogoro na utapeli wa ardhi hapo baadae

SoC04 Mfumo na utaratibu wa urasimishaji ardhi uboreshwe ili kuongeza Ufanisi na kuepukana na migogoro na utapeli wa ardhi hapo baadae

Tanzania Tuitakayo competition threads

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
Utangulizi.
Migogoro ya ardhi nchini ni mingi sana,kinachopelekea uwepo wa migogoro hii ni utaratibu na mfumo wa urasimishaji ardhi kuwa na mapungufu mengi ambayo yanaruhusu mianya ya ulaghai kama vile kufoji hati na nyaraka nyingine za umiliki,uuzwaji holela wa viwanja.

Kuyakabili haya yafuatayo yapaswa kufanyiwa kazi,
  1. Kuwepo kwa maafisa ardhi kila kata.
  2. Maafisa ardhi kupewa vitendea kazi.
  3. Uundwe mfumo wa kidigitali kwa ajili ya masuala ya ardhi.
  4. Madalali wa kuuza viwanja na nyumba wasajiriwe na watambuliwe na mfumo.
  5. Zoezi la urasimishaji ardhi lifanywe upya.
Uwepo wa maafisa ardhi kila kata.
Wizara ya ardhi inakabiliwa na uhaba wa maafisa ardhi kuanzia ngazi ya chini,hivyo serikali haina budi kuajiri wataalamu wa ardhi angalau kuanzia ngazi ya kata ili iwe rahisi kushughurikia na kusimamia masuala yote yanayohusiana na ardhi kwa ufasaha,maafisa hawa watashirikiana na wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata ili kupata historia na miongozo kuhusu ardhi husika kwa lengo lakufanya maamuzi sahihi.

Maafisa ardhi wapewe vitendea kazi.
Baada ya kuajiri maofisa ardhi serikali kupitia wizara ya ardhi iwapatie maofisa hao vifaa vya kufanyia kazi kama vile vifaa vya kuchukulia vipimo,kompyuta mpakato ama Vishikwambi vyenye uwezo mkubwa vilivyounganishwa na intaneti kwa ajili ya kurahisisha usajiri ama uhakiki wa ardhi husika kwa njia ya kidigitali kupitia mfumo utakao undwa.

Uundwe mfumo wa kidigitali.
Mfumo huu utatumiwa kurasimisha ardhi,kuomba na kutengeneza hati,kuomba kibali cha kuwa dalali wa viwanja,kuomba kibali cha kuuza nyumba ama Kiwanja,kuripoti kero zinazohusiana na ardhi.

Mfumo huu utaunganishwa na kanzi data kwa ajili ya kutunza kumbukumbu zote za ardhi,utaunganishwa na mfumo wa GPS na TAMISEMI kitengo cha utowaji vibali vya ujenzi.

Pia utaunganishwa na wizara ya madini ili kutambua umiliki halali wa eneo ambalo mtu anakatia leseni ya umiliki wa mgodi,kwa sasa mtu anaweza kwenda kuomba leseni ya kumiliki sehemu flani ili kuchimba madini bila kumshirikisha mmiliki halali wa ardhi kitu kinachopelekea kuzuka kwa migogoro ya mara kwa Mara,kupitia mfumo huu watalamu kutoka wizara ya ardhi watakapoenda kuchukua kodineti katika eneo husika mfumo utakuwa na uwezo wa kutafuta na kuoanisha taarifa za umiliki,kama eneo hilo limesha rasimishwa zitatokea taarifa rasmi za nani ni mmiliki halali wa eneo hilo hivyo mfumo utaelekeza kuwasiliana na muhusika kupitia namba za simu zitakazo onekana katika mfumo,au watalam hao kuwasiliana na afisa ardhi waeneo husika,ili kumpata mmiliki wa ardhi ndio mchakato uendelee, kama eneo halijarasimishwa mfumo hautaruhusu kuendelea na zoezi la usajiri wa leseni mpaka mchakato wa urasimishaji utakapo kamilika,hivyo muombaji wa leseni atatakiwa kuwasiliana na afisa ardhi wa kata husika ili kumtambua mmiliki wa eneo husika kwa makubaliano ili ardhi irasimishwe ndio mchakato wa kuomba Leseni uendelee.

Mfumo utafanya kazi kwa kutambua kodineti,afisa ardhi ataingiza coordinates zilizopo kwenye hati ya umiliki wa eneo husika kisha taarifa za umiliki zitatokea na katika suala la kurasimisha ardhi kwa mmiliki,mtu anayehitaji kurasimishwa ardhi atatuma maombi yake kupitia programu ya simu ya wizara baada ya kujisajiri ,maombi hayo yatapokelewa na afisa ardhi katika kata husika kisha atawasiliana na baraza ardhi la kata ili kupata uthibitisho juu ya uhalali wa muombaji kumiliki eneo hilo baada ya kuthibitishwa ndipo afisa ardhi ataendelea na zoezi kwa kuidhinisha malipo kwa muombaji ambapo muombaji ataona kupitia programu yake ya simu nambari ya malipo ,baada ya kulipia ndipo sehemu maalumu kwa ajili ya kuingiza takwimu itaweza kufanya kazi,wakati wakuchukua kodineti kompyuta mpakato au kishikwambi cha afisa ardhi kitakuwa kina mawasiliano na kifaa cha kuchukulia kodineti ili kurahisisha vipimo kurekodiwa moja kwa moja katika mfumo,baada ya kukamilisha uchukuaji wa kodineti mmiliki wa eneo atapigwa picha na afisa kupitia mfumo na kusajiri alama zake za vidole na kuhifadhi kisha kutuma taarifa hizo ili kuhakikiwa makao makuu ya wizara ,baada ya kuhakikiwa na kuthibitishwa mfumo utatengeneza nambari ya malipo kwa ajili ya hati miliki ambayo mwenye eneo ataiona kupitia programu ya simu na kutumiwa ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu na baada ya kufanya malipo mfumo utatengeneza hati ya umiliki ikiwa na taarifa kamili ,na hati hiyo ataipata kupitia afisa ardhi wa eneo hilo baada ya mchakato kukamilika.

Kwa anayetaka kuuza ama kununua ardhi atawasiliana na dalali aliyesajiriwa ,dalali atawasiliana na afisa ardhi ambaye atasimami na kuthibitisha mchakato mzima ambapo mmiliki atatakiwa kuthibitisha uuzwaji huo kwa kusaini kwa alama za vidole na mnunuzi atasaini kwa alama za vidole na baada ya malipo kukamilika afisa ata tuma na hati ya muuzaji itafutwa katika mfumo na hati ya mnunuzi itaundwa ambapo mnunuzi atatumiwa nambari ya malipo ili kukamilisha mchakato wa kupata hati yake na katika mfumo kwa kodineti za eneo lililouzwa zitasoma taarifa za mnunuaji na sio muuzaji tena.

kila anaye miliki ardhi au nyumba atakuwa na akaunti ambayo ataisajiri kupitia kompyuta au programu ya simu na kila mwezi taarifa zake za kodi ya ardhi inayokatwa kupitia mfumo wa LUKU kama ni nyumba itaonekana na kama ni kiwanja ama shamba atatumiwa nambari ya malipo ya ardhi hiyo kulingana na utaratibu utakao wekwa na ataona katika programu ya simu.

MadalalI wa uuzaji wa viwanja na nyumba wasajiriwe.
Madalali wote wanaojihusisha na uuzaji wa nyumba na viwanja wasajiriwe kwa kupewa leseni na wizara kisha wajisajiri katika mfumo ambapo wanaweza kutafutwa katika mfumo wa wizara na wakaonekana sambamba na nambari zao za leseni,wao hawataruhusiwa kusimamia uuwaji bali ndio watakao wasiliana na afisa ardhi ilikufanikisha uuzwaji au ununuzi.

Urasimishaji wa ardhi ufanywe upya.
Kwa kuwa kuna maeneo ambayo tayari ardhi imesha rasimishwa na mfumo mpya utakuwa umeundwa basi wale wote waliorasimishwa watapaswa kuwasilisha taarifa zao kwa afisa ardhi wa eneo husika ili taarifa hizo ziingizwe kwenye mfumo kwa uthibitisho,taarifa zote zitakuwepo katika mfumo kasoro baadhi ya taarifa kama picha na saini kwa alama ya vidole,hivyo afisa ardhi ataingiza taarifa kutoka kwenye hati ya mmiliki kama ni sahihi na zile zilizopo katika mfumo picha na alama za vidole zitachukuliwa hii ni kwa wamiliki husika,kwa wale waliopoteza maisha kutakuwa na utaratibu wa ndugu kushughurikia kupitia mabaraza ya kata kwa kujadiriana na wanafamilia ili kupata muafaka ama wosia kama marehemu aliacha,mfumo utaruhusu kutambua mmiliki zaidi ya mmoja pia ambao ni ndugu.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom