A
Anonymous
Guest
Deadline ya lile tangazo ilikuwa Mei 16, hivyo kwa sababu za kimitandao kufeli ku-access ikawa ngumu kwa sisi wenye matamanio ya kufanya kazi za Kipolisi kwa maslahi mapana ya Taifa letu kuomba nafasi.
Serikali iliweka wazi kuwa changamoto ya kimtandao ambayo iliathiri Nchi nzima ilichangia kuathiri.
Tunashukuru Jeshi la Polisi, juzikati liliongeza siku 6 nyingine mbele hadi tarehe 21/05/2024 ili kufidia hizi siku mbazo network ilikuwa inafeli, sasa cha ajabu mpaka sasa Portal yao haiingiliki kabisa na siku zinazidi kuisha.
Nashauri watafute mbinu mbadala ya kuwasilisha maombi kwa kuwa tunaoumia ni wengi.
Sasa hivi shida sio Mtandao tena kama ilivyokuwa awali, sasa hivi ni Mfumo wao wa Portal unazingua, ndio tatizo.
Ukifungua tovuti yao ya Polisi (ajira2.tpf.go.tz) italeta sehemu ya kujaza candidate Name, Email, Password kisha unabonyeza create.
Baada ya hapo inataleta sehemu ya kujaza NIN (NIDA), ukijaza NIDA ina search kama kwa dakika 4+ kisha inakwambia “no found details check your NIN”.
Hapo ndio panashida, inaonesha kanzidata ya Police haiwezi ku-trape taarifa kutoka kwenye Kanzidata ya NIDA.
Majibu ya Polisi- Jeshi la Polisi laongeza muda wa maombi ya kazi baada ya Mfumo wa Mtandoo wao kusumbua