KERO Mfumo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu umekuwa na changamoto wiki hii, haupokei maombi ya wahitaji kwa siku ya 9 leo

KERO Mfumo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu umekuwa na changamoto wiki hii, haupokei maombi ya wahitaji kwa siku ya 9 leo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Samwel90

Member
Joined
Jan 22, 2025
Posts
53
Reaction score
42
Napenda kuwasilisha malalamiko yangu kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania kuhusu matatizo yanayojitokeza katika mfumo wenu wa maombi ya mikopo tangu zoezi la maombi lilipofunguliwa tarehe 15 hadi leo hii tarehe 24/01/2024 Tatizo kubwa ni kwamba hakuna maombi yaliyopokelewa kutokana na changamoto katika mfumo wenu, ambazo ni pamoja na:

1. Kum-Logout Mteja Kwa Haraka: Mfumo unawatoa watumiaji (log out) ndani ya dakika moja tu baada ya kufungua. Hii inasababisha usumbufu mkubwa na inafanya kuwa vigumu kukamilisha maombi.

2. Changamoto Kwenye Sehemu ya Taarifa za Demografia: Wakati wa kujaza taarifa za uhakiki wa cheti kutoka RITA, mfumo unakataa kupokea taarifa na kuandika "error, jaribu tena baadaye." Hii imekuwa kero kubwa kwa waombaji wengi.

Binafsi, nimepiga simu mara nne hadi imekuwa kero kwa watoa huduma na wamekalili namba yangu. Jana nilipiga simu bila hata kusalimiana na mtoa huduma na kuelezea tatizo langu, yeye tayari alishajua na akanambia tatizo bado liko palepale na niendelee kuvumilia. Hadi muda huu, tatizo bado lipo ikiwa ni siku ya 9 leo.

Ombi Langu:
1. Shughulikieni Tatizo Hili Mapema: Tunaomba mamlaka zinazohusika zichukue hatua za haraka na za dharura kutatua tatizo hili. Sitaki kuamini kuwa Tanzania kuna uhaba wa wataalamu wa mfumo ambao wanaweza kutatua tatizo hili kwa muda mchache.

2. Ongezeni Muda wa Maombi: Kutokana na matatizo haya, tunaomba Bodi iongeze muda wa maombi kwani mpaka sasa zimebaki siku chache kabla ya dirisha la maombi ya mkopo kufungwa. Hii itatoa fursa kwa waombaji wote kukamilisha maombi yao bila shinikizo la muda.

Nategemea kwamba Bodi itazingatia malalamiko haya kwa uzito unaostahili na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha kwamba mfumo unafanya kazi ipasavyo na waombaji wanapata huduma bora.
Screenshot_20250124-122735.png
Asanteni.

Majibu ya Bodi, soma hapa ~ Bodi ya Mikopo: Tumepokea maoni kuhusu changamoto ya mfumo kwa waombaji wa Diploma, tunashughulikia changamoto hiyo
 
Back
Top Bottom