SoC04 Mfumo wa elimu barabara iendayo Tanzania tuitakayo

SoC04 Mfumo wa elimu barabara iendayo Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ndemela Jr

New Member
Joined
Jun 25, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Naam.

Ni wasaa mwingine ambao tupo kusoma dira vizuri ili tusipotee katika mwelekeo wa safari yetu kuitafuta TANZANIA Bora Zaidi.

Bila kupoteza muda niende Moja Kwa moja nikibainisha wazi ya kwamba ili tuipate hio Tanzania tuitakayo ipo mbegu Moja kuu ambayo ni lazima tuipande chini iote ndipo tupate matunda yake ambayo Kwa hakika ndio hasa TANZANIA TUITAKAYO, Mbegu hio ni ELIMU.

ELIMU ni nini, Kwa ujumla wake ELIMU ni mkusanyiko wa taarifa sahihi kuhusu jambo au kitu Fulani ambazo hizi taarifa zinakusaidia kuyaweza mazingira.

Hivo basi hapa tunaona ELIMU Ina vitu viwili vikuu .

1. Ni mkusanyiko wa taarifa: ambapo sasa huu ndio ufahamu wote tunaowapa wanafunzi wetu na watakapoukamilisha ndipo hutunukiwa cheti Cha kukubalika kama wabobevu katika ufahamu husika.

2. Ili kuyaweza mazingira; hili ni DHUMUNI LA ELIMU. ELIMU sio mtindo wa maisha au maonyesho Fulani ilimu ipo Kwa makusudi maalumu, ya kumsaidia mtu kuyaweza mazingira, kuisaidia TANZANIA kupiga hatua ili tuifikie TANZANIA TUITAKAYO Kwa kipindi Fulani Cha Muda.

Kwa muda mrefu sana Tanzania tunayo ELIMU watu husoma hapa na kuhitimu. Lakini Leo nasimama kukosoa mfumo mzima wa ELIMU na ELIMU inayoendelea kutolewa nchini kuwa imepitwa na wakati na haitupeleki mbele Tena ila inatuvuta turudi nyuma.

Ni Kwa sababu gani basi: sababu hasa ni hizi,

1. Kwanza ELIMU hii itolewayo nchini ni ELIMU ya kikoloni (Colonial education) ELIMU hii ilikuwa na lengo la kumunufaisha Zaidi mkoloni kuliko mtanzania.

ELIMU hio ilikuwa na lengo la kuua ubunifu, stadi na tamaduni za kitanzania ili kurahisisha namna ya huitawala Afrika si kuisaidia.

ELIMU hii ilianzishwa mahususi ili kuzalisha wasomi wenye uwezo wa kusimamia mipango kazi Fulani tu ila sio wasomi wenye uwezo wa kuzalisha maona makubwa na kuyafanyia kazi

ELIMU hii ililenga kuzalisha waajiriwa tu, sio wabunifu wenye kutengeneza ajira zaidi,

Ndio maana hata viwanda na miradi mingi iliyoachwa na wakoloni ilikufa Leo Haipo Kwa sababu ELIMU ya kikoloni haikuwa inatengeneza watu wakutoa mipango kazi Bali wasimamizi tu.

2. ELIMU hii ililenga kuwagawa watanzania ikawekwa kwenye mfumo wa mche pia (pyramid shaped education) Hii iliwagawa watanzania wa awali mpaka tinaoisoma sasa.

Hivyo Kwa kweli kwa kutizama mambo haya machache tu unaona ELIMU hii si msaada Tena Kwa Taifa letu. Zamani kweli tulihitaji kujua kusoma na kuhesabu tu ndipo tujikomboe. Lakini mahitaji ya sasa ni tofauti sana. ELIMU itolewayo nchini haikizi kuyaweza mazingira. Mfano;

* Tumeshindwa kutengeneza dira ya nguzo kuu ya uchumi mchini,

* Tumeshindwa kuwa na dira ya teknolojia ya ujenzi na uchukuzi, tenda zote za ujenzi na usafirishaji tumeita watu watufanyie, hatuwezi kuifikia TANZANIA TUITAKAYO Kwa kuendelea kupata ELIMU dhaifu kiasi hiki. ELIMU hii imelifanya taifa lisijiamini, mfano katika mkataba wa ubinafisishaji wa Bandari za Tanzania bara, ni kukosa kujiamini Kwa viongozi ambapo nnaamini hata wangepewa watanzania wazalendo wangeweza kuongeza tija Zaid wangeongeza uzoefu na maarifa ya jinsi ya kuitumikia nchi Kwa tija Zaidi. ELIMU hii inatutia upofu tuachane nayo.

Sasa basi ni kipi lifanyike:
1. Mfumo wa ELIMU uhuishwe pamoja na maudhui yake (content)
Maudhui ya ELIMU yawe yenye dira na uelekeo wa ubunifu. Uwe na mlengo wa kubuni bidhaa huduma na teknolojia ili kupunguza utegemezi wa taifa Kwa miaka 25 ijayo.

Sambamba na mihula ya ufundishaji pamoja na upimaji wa wanafunzi wanafunzi wapimwe Kwa maendeleo ya Kila siku sio mitihani ya mwisho.

Pia mafunzo yawe ya vitendo Zaidi kuliko nadharia, na uwezo wao utazamwe huko kwenye utendaji wao. Hii itasaidia kuondoa hata tatizo la Ajira nchini Kwa 100%.

2. Iundwe Sera Bora ya malezi, Sera hii ya malezi ilenge kuwajenga watoto wa kitanzania kujitegemea wao kama wao bila kutarajia msaada mahali pengine. Hii itasaidia baada ya miaka 25 kuwa na taifa lenye mshikamano na kujiamini kama taifa bila kuangalia misaada mahali pengine.

3. Majukwaa kama JamiiForums na mengine yanayokusanya na kuibua mawazo mapya yakilenga kujenga nchi yetu vizuri yaangalie uwepo wa kufikisha mawazo hayo Kwa serikali ili yaweze kufanyiwa kazi. Maana ninyi ni kama njiti za viberiti tunazotarajia kama taifa kuwasha moto wa kuitafuta TANZANIA TUITAKAYO.

Mwisho
Naushukuru uongozi wa JF Kwa wazo hili la kuanzisha jukwaa hili. Matumaini yangu ni kwamba kupitia ninyi kizalendo na Kwa umoja tunalijenga taifa letu.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom