Jerry Farms
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 202
- 167
Kwa mujibu wa ripoti ya Tasisi ya Utafiti na Kupunguza umaskini Tanzania(REPOA) ya 2019, wasomi milioni moja huzalishwa kwa mwaka alhali idadi ya ajira zinazozalishwa serikalini na katika sekta binafsi ni 250000.
Nayo taarifa ya muenendo wa ajira toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaonesha hali ya ajira ikiendelea kuzorota siku hadi siku mfano kwa mwaka 2019 asilimia 9.6 ya wananchi hawakua na ajira, 2020 asilimia 9.5 na 2021 asilimia 9.0.
Hali hii haiko Tanzania tu bali ni tatizo la kidunia mfano Kenya asilimia 4.9 ya vijana haikua na ajira kwa mwaka 2019, (Ripoti ya Tume ya taifa ya Takwimu Kenya,2019).
Tatizo la ukosefu wa ajira limechagizwa na mambo mengi ikiwemo; mifumo mibovu ya kielimu, ukuaji wa teknolojia, kuyumba kwa uchumi, rushwa na ufisadi, mabadiliko ya tabia nchi na kadharika. Licha ya jitihada mbalimbali kufanyika tatizo hili bado lingalipo.
Sasa imefikia wakati muafaka kwa wazazi na walezi kuachana na kasumba mbaya waliyokua wamejijengea kwa muda mrefu ya kuwa wakisomesha watoto wao basi matokeo yatakua ni kwa wao kuajiriwa! Zoea hili halina budi kufanyiwa mapinduzi makubwa haswa.
Tatizo la ajira ni mtambuka, ni muda sasa wazazi wajikite katika kuweka mazingira ya wao kua ndio waajiri wakuu wa wasomi ambao ni watoto wao. Hili litawezekana tu kama patatokea badiliko la kifikra kwa wazazi wenyewe juu ya dhima nzima ya Elimu na ajira.
Ni kwa vipi sasa mzazi anaweza kuwa muajiri mkuu?
Wazazi wajikite katika uwekezaji wa rasilimali fedha katika Elimu mazingira( Elimu ya ujuzi na stadi za maisha).
Elimu mazingira ni elimu ile inayoendana na mahitaji ya soko na hali halisi ya kimaisha aliyoko mzazi na mwanae.
Hapa hatumaanishi mzazi apuuze Elimu, la hasha! Bali mzazi awekeze katika elimu yenye manufaa kwa mwanae.
Mfano mzazi aliyeko mazingira ya ufugaji/kilimo basi jitihada zake kubwa ziwe katika kumuelimisha mtoto ajikite katika kuzisoma na kuzitatua changamoto zilizomo katika sekta ajiri iliyopo katika mazingira wanayoishi.
Mzazi kujenga zoea la kutunza akiba kwa ajili ya mtaji kwa mwanae.
Somo la utunzaji wa akiba lina umuhimu mkubwa kutolewa kwa wazazi na walezi. Zoea la wazazi kusomesha mtoto katika shule za gharama kubwa linapaswa kubadirishwa na msukumo mkubwa kupelekwa katika kufanya maandalizi ya mitaji kwa watoto.
Imekuwa ni zoea kwa mzazi kuwa radhi alipe mamilioni kusomesha mtoto lakini ni mzazi huyo huyo hayuko tayari kutoa kiasi japo nusu ya hicho kama mtaji kwa mwanae. Waswahili wanamsemo wa "Akiba haiozi" shime kwa wazazi kuzingatia hilo.
Mzazi kuanzisha na kuwa msimamizi mkuu wa shughuli aliyomuajiri mwanae.
Pendekezo hili liwekwe katika mtazamo wa mzazi kuwekeza katika mradi A na kumuajiri kijana wake. Hapa wazo la uwekezaji katika mradi huo inabidi liwe limejumuisha mawazo ya wanafamilia.
Ushirikishwaji wa vijana kabla ya kuwekwa kwa fedha katika mradi kutawafanya vijana hao wapende na kujikitakwa moyo katika mradi husika.
Ajira ni chache na wasomi ni wengi, ni jitihada binafsi za wazazi, walezi na vijana ndizo zitakazo komboa chumi za familia na taifa kwa ujumla.

Upvote
2