Mfumo wa elimu ubadilishwe. Je, unataka uweje?

Mfumo wa elimu ubadilishwe. Je, unataka uweje?

Joined
Jul 5, 2024
Posts
20
Reaction score
58
Kila kona ya nchi watu wanalalamikia mfumo wetu wa elimu. Kama ni elimu ya vitendo hata VETA ipo.

Je, wewe ungepewa nafasi ya kubadilisha mfumo wa elimu ungefanya nini?ungeboresha nini?

Weka hoja ya msingi tafadhali.
 
Wafundishe vitu vya msingi na wavipe kipaumbele kisha ndipo waongeze mambo ambayo siyo ya msingi lakini ni muhimu.

Mfano,kuna unaweza kumfundisha mtu jinsi ya kutengeneza gari,baadae akishajua ndipo unamfundisha fizikia ajue masuala mbali mbali kv motion,friction,heat,n.k

Ama unaweza kumfundisha mwanafunzi jinsi ya kutengeneza dawa kisha baadae mfundishe kemia,mwili wa binadamu,hisabati n.k

Kinachofanyika sasa katika elimu yetu,ni sawa na kumfundisha mtu fizikia ya baiskeli halafu ukimpa hiyo baiskeli hawezi kuiendesha na hata kuziba pancha tu.
Ila akianza kukusimulia inavyoendeshwa tena kwa kiingereza,kila mtu anaona unajua sana kumbe ubabaishaji tu
 
Muda wa masomo rasmi wa darasani ufupishwe mpaka saa Saba hivi, baada ya hapo mtaala usio rasmi uendelee.
Na huu ujinga wa watoto kushindishwa shule mwaka mzima - hakuna likizo, week end ufe.
 
Mimi mchango wangu;
1. Tuongeze Vyuo vya veta wanafunzi wakimaliza kidato cha sita wote waingie VETA kwa mwaka mmoja ndio wajiunge vyuo
2. Wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne wale ambao hawajapata nafasi kuingia kidato cha tano au Vyuo rasmi, wote waingie VETA walau mwaka mmoja na kuendelea kwa wale watakaofaulu vizuri
Hii itafanya wahitimu wa ngazi mbalimbali wawe na pa kuanzia kwa kuwa wana ujuzi

3. Mitihani ya form four iwe compulsory kusoma kuanzia masomo manne tu +English kwa wale wa saiyansi
mfano:
Phy, Chem, Biol, Hesabu na English
au History, Geography, kiswahili na English
Chemistry, Biology, Geography na English

Nategemea kwa kufanya hivyo tutakuwa na wanafunzi wabobevu kuanzia huku chini kwa kusoma masomo machache
 
Wenzetu Nigeria tayari washafanikiwa kuurekebisha mfumo wao wa elimu kuanzia Primary watoto watakuwa wana somo la fani kwa nadharia na vitendo.
Hicho ndicho kinachotakiwa kifanyike.
Ukisema elimu ya vitendo iko veta si kila Mhitimu atapata nafasi ya kwenda kusoma Veta kwa sababu mbalimbali maana huko Veta hiyo huduma haitolewi bure.
 
Attachments

  • Screenshot_20241119_073023_LinkedIn.jpg
    Screenshot_20241119_073023_LinkedIn.jpg
    193.4 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241119_073023_LinkedIn.jpg
    Screenshot_20241119_073023_LinkedIn.jpg
    193.4 KB · Views: 4
Wafundishe vitu vya msingi na wavipe kipaumbele kisha ndipo waongeze mambo ambayo siyo ya msingi lakini ni muhimu.

Mfano,kuna unaweza kumfundisha mtu jinsi ya kutengeneza gari,baadae akishajua ndipo unamfundisha fizikia ajue masuala mbali mbali kv motion,friction,heat,n.k

Ama unaweza kumfundisha mwanafunzi jinsi ya kutengeneza dawa kisha baadae mfundishe kemia,mwili wa binadamu,hisabati n.k

Kinachofanyika sasa katika elimu yetu,ni sawa na kumfundisha mtu fizikia ya baiskeli halafu ukimpa hiyo baiskeli hawezi kuiendesha na hata kuziba pancha tu.
Ila akianza kukusimulia inavyoendeshwa tena kwa kiingereza,kila mtu anaona unajua sana kumbe ubabaishaji tu
hahahaha true
 
Kinachovuruga elimu ya Tanzania ni lugha ya kiswahili.Hii lugha haifai kabisa Kwa elimu.Inapelekea kuwanyima fursa watz kimataifa
 
Back
Top Bottom