Wafundishe vitu vya msingi na wavipe kipaumbele kisha ndipo waongeze mambo ambayo siyo ya msingi lakini ni muhimu.
Mfano,kuna unaweza kumfundisha mtu jinsi ya kutengeneza gari,baadae akishajua ndipo unamfundisha fizikia ajue masuala mbali mbali kv motion,friction,heat,n.k
Ama unaweza kumfundisha mwanafunzi jinsi ya kutengeneza dawa kisha baadae mfundishe kemia,mwili wa binadamu,hisabati n.k
Kinachofanyika sasa katika elimu yetu,ni sawa na kumfundisha mtu fizikia ya baiskeli halafu ukimpa hiyo baiskeli hawezi kuiendesha na hata kuziba pancha tu.
Ila akianza kukusimulia inavyoendeshwa tena kwa kiingereza,kila mtu anaona unajua sana kumbe ubabaishaji tu