HALI ILIVYO NA MAMBO YA KUANGAZIA:
Bado kuna ombwe kubwa la kutofautiana katika ujuzi na maarifa miongoni mwa baadhi ya wahitimu wa vyuo tofauti waliosomea shahada zinazoshabihiana.
Aidha wanafunzi wengi wa vyuo vikuu na wahitimu wa vyuo hivyo wamechagua au wamesomea shahada za fani wasizozijua, wasizozipenda wala kuwa na malengo ya kuzifanyia kazi binafsi baadae maishani mwao. Hili linatajwa kusababishwa na sababu mbalimbali kama vile umasikini wa kipato katika familia wanazotoka, kozi vipaumbele kupewa mkopo wa elimu ya juu, ufaulu duni n.k.
Licha ya baadhi ya fani kama ualimu, sheria na baadhi ya fani za afya kuwa na mafunzo ya vitendo (field training), kwa kiasi kikubwa elimu ya vyuo vikuu bado inatolewa kwa nadharia.
SULUHISHO:
Wizara ya elimu ishirikiane na TCU kuaandae mtaala utakao ziunganisha pamoja shahada zote zinazoshabihiana kutoka vyuo mbalimbali, ziwe na mlengo mmoja na content inayofanana. Hii itasaidia kuondoa hata kile kinacho semwa miongoni mwa wahitimu kuwa “digrii ya chuo flani ni balaa, ukisoma pale wewe mkali”. Hivyo upekee wa chuo flani kuwa kinatoa digrii bora kuliko nyingine utabakia kwenye umahiri wa mwanafunzi husika.
Kwa mfano, October 30 mwaka 2023 Serikali kupitia Wizara ya elimu ilitangaza kuoanisha mitaala ya elimu ya ualimu kwa ngazi ya stashahada na shahada kuwa na mshabihiano kwenye kile kilicho kuwa kinatajwa kama utofauti wa mbinu nyingi za ufundishaji wanazofunzwa wahitimu wa stashahada dhidi ya chache za wahitimu wa shahada. chanzo: Serikali kuoanisha mitaala ya ualimu stashada na shahada
Napendekeza mfumo wa elimu ya juu ubadilishwe na kuwa wa vitendo zaidi kwa degree programmes zote. Asilimia zisizopungua 70 ya University curriculumns ziwe ni vitendo vinavyo mtaka mwanafunzi kufanya Critical thinking and Augumentation, Literature reviews, library and laboratory investigations, kuandaa customer care experience and feedback reports, business communications and interaction reports, kubuni vitu, kuanzisha miradi, n.k. Aidha vyuo vitengeze utaratibu mzuri wa kuwapima na kuwatathmini wakiwa field, kisha wapewe grades kulingana na utendaji kazi au ushiriki wao kwenye field practical training.
Hili linaweza kufanyika kwa utaratibu ufuatao;
Wahitimu wa kidato cha sita wakishafanya maombi ya mikopo, Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) ichakate na itoe Means Testing kwa kila mwanafunzi husika.
Tarehe za kufungua vyuo zikifika wanafunzi wote waripoti kwenye vyuo wanavyopenda wenyewe na kwa hatua hii wanafunzi wasajiliwe na kupewa vitambulisho vya vyuo husika bila kujali cut-off points zake za ufaulu.
Baada ya usajili wanafunzi wapewe semina ya muongozo na utambuzi kuhusiana na degree programmes zinazotolewa na chuo husika. Katika hatua hii wanafunzi waelezwe maarifa wanayotakiwa kuwa nayo ili kusoma kozi flani, waelezwe na kuoneshwa umuhimu wa kuchagua kusomea kile wanachokipenda na kutamani kukifanyia kazi maishani, waletewe wataalamu waliobobea na kufanikiwa katika kila kozi au fani husika, wapewe uzoefu wa kweli wa kiutendaji kulingana na kile atakachosomea.
Haya yafanyike wiki ya “Orientation” ambayo mara nyingi imekuwa haitumiki ipasavyo japokuwa ipo kwenye “almanac” ya vyuo ya kila mwaka. Hii itasaidiaa wanafunzi kuchagua na kusomea fani wanayoipenda kwakuwa wana taaarifa za kutosha baada ya kuelezwa na kuona mifano halisi ya wafugaji, wanasheria, wataalamu wa saloon na urembo, wahandisi wanahudumu wa afya n.k.
Baada ya Orientation wanafunzi wapewe barua maalum na vyuo vyao zitakazo mtambulisha kila mwanafunzi na kuufahamisha umma na mamlaka mbalimbali kwamba huyu ni mwanafunzi na yuko field kwa ajili ya “intensive practical training” hivyo asaidiwe kwa hali na mali kufanikisha kile atakachokuwa anakifanya. Kila mwanafunzi atapewa uhuru wa kwenda katika kiwanda, ofisi, sehemu za biashara, mashambani, migodini, vikosi vya majeshi, usafirishaji n.k.
Iwapo mwanafunzi ataenda field katika sekta aisizo rasmi (yaani zisizo na utaratibu rasmi wa kiofisi) kama mkulima mdogo au mjasiriamali wa kibanda kidogo cha kuuza mahitaji yatumikayo nyumbani kila siku, asizuiliwe wala kutengwa. Hilo litakuwa jukumu la chuo chake, TCU, na Wizara ya elimu kutengeneza utaratibu bora wa kumpima na kutathmini kile anachokifanya kama kina tija kwake, jamii yake na taifa kwa ujumla, na apewe grades zitakazoonekana kwenye cheti chake cha kuhitimu elimu ya chuo kikuu.
Kwa hatua hii HESLB itaendelea kuwapa mikopo na “Boom” wanafunzi kulingana na Means Testing zao na pesa za field ziwe kiwango sawa na lazima kwa wanafunzi wote. Aidha ili kuongeza ufanisi na ubunifu kwa wanafunzi wawapo field na kuwapa utayari wa kukabiliana na changamoto mpya, vyuo na TCU vitaweka utaratibu iwapo itakuwa sawa kwa mwanafunzi kurudia kufanya field pale alipofanyia awali au aende sehemu mpya.
Baada ya muda wa field kuisha wanafunzi watarudi vyuoni na hapo ndipo mwanafunzi atadahiliwa katika kozi inayoshabihiana na kile alichokuwa anakifanya field kwa kuangalia iwapo grade alizozipata field zimefikia “pass mark” zilizowekwa na chuo au TCU ili kudailiwa kwenye kozi husika. Hapa wanafunzi watashauriwa aidha kurudia field kwa bidi na ubunifu zaidi, kufikiria kitu kingine wanachokipenda Zaidi, au kutafuta chuo kingine. Aidha HESLB haitachukulia hii kama “Discontinue” itaendelea kumhesabia kile ilichompatia awali kama sehemu ya mkopo na atakilipa.
Kwa uendelelevu wa utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, nashauri HESLB iweke ukomo wa ukopeshaji wanafunzi kulingana na mahitaji ya fani mbalimbali, mfano B.com Entrepreneurship anaweza kukopeshwa hadi Tsh. Milioni 9, hii ni kwa sababu baadhi ya fani kama hii watakuwa wanazalisha wakiwa field na kujiingizia kipato ambacho kinaweza kuwasaidia kujigharamia baadhi ya mahitaji ya chuo kikuu kama malazi, chakula, usafiri, vitabu, machapisho na “madesa.”
Vyuo vikuu vinaweza kuwa na idadi ukomo ya wanafunzi vinaoweza kuwadahili kwa mwaka kulingana na miundombinu yake. Niwatoe hofu ya kuzidiwa na idadi ya wanafunzi, kwani kwa mfumo huu tunategemea wanafunzi hawatakuwa na masomo mengi ya theory kuwahitaji wakae vyuoni muda mwingi kwa ajili ya lecture. Napendekeza mfumo uwe kama ifuatavyo;
Jedwali: Mfano wa mfumo wa elimu kwa shahada ya miaka mitatu
WITO:
Serikali ipokee na iyafanyie kazi mawazo mapya ya kibunifu hata kama inahisi hayawezekani kutekelezeka isiyapuuzie bila kuyafanyia majaribio, kwani njia aliyoitumia aliyetutangulia kutatua tatizo hilihili inaweza isiwe sahihi kwa wakati huu na mazingira haya tukizingatia uwezo wetu wa kiuchumi.

YEAR OF STUDY | SEMESTER | MODE OF INSTRUCTION |
1 | I | Industrial/Field Practical Training (Full Time) |
1 | II | Lecture discussions (Full Time) |
2 | I | Industrial/Field Practical Training (Full Time) |
2 | II | Lecture discussions (Full Time) |
3 | I | Industrial/Field Practical Training (Full Time) |
3 | II | Industrial/Field Practical Training (Full Time) |

Upvote
1