Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Alhamisi Februari 10, 2011 Makala
Mfumo wa elimu ya sekondari unahitaji mageuzi makubwa
Imeandikwa na Neophitius Kyaruzi; Tarehe: 9th February 2011 @ 23:45 Imesomwa na watu: 22; Jumla ya maoni: 0
Wanafunzi wakijisomea chini ya miti.
Habari Zaidi:
MATOKEO ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni, yameacha maswali mengi kuhusu mustakabali wa elimu hapa nchini.
Pamoja na nia njema ya serikali ya kuhakikisha kwamba kila mtoto, anapata fursa ya kupata elimu ya sekondari kupitia mpango wa ujenzi wa shule za sekondari katika kila Kata, mkakati huo umeonekana kutozaa matunda; ambapo kiwango cha elimu kimeonekana kuporomoka kwa kasi.
Shule za serikali sasa hazitoi matumaini, kwamba zinaweza kufanya vizuri katika siku za karibuni kama zilivyo shule binafsi, kama hakutakuwapo na mkakati wa makusudi wa kuzinusuru, ikiwamo kuhakikisha zinapata walimu wa kutosha na wenye uwezo mkubwa wa kufundisha, kuzipatia nyenzo muhimu kama vile maabara na vitabu vya kutosha.
Matokeo ya mwaka huu ya shule za serikali, yanakatisha tamaa kwani shule za serikali zimeachwa mbali na shule binafsi, jambo linaloashiria kwamba kuna tatizo kubwa katika mfumo na Sera, zinazotoa mwongozo wa elimu kwa ujumla.
Kadri miaka inavyoendelea mambo yanaonekana kuharibika kwani hata shule kongwe ambazo zilikuwa zikisifika kuwa ndio za wanafunzi wenye vipaji maalumu pia hazikufanya vizuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Tunapojadili suala hili tunapaswa kwenda mbali zaidi kutazama mfumo wa elimu yetu kwa ujumla kuanzia maendeleo ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ufundi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Tukifanya hivyo tutabaini kama elimu inayotolewa inaweza kubadili maisha ya wanafunzi hapo baadaye au tunahitaji kuwa na taifa linasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi shuleni.
Kinachoonekana sasa ni kwamba mamlaka zinazosimamia shule zinaonyesha kushindwa
kuasisi mifumo endelevu ya kuinua elimu inayoendana na mahitaji ya sasa.
Kwa mfano, kutokana kukosekana ubunifu wa sera madhubuti, serikali ilidhani kuwa inatosha tu kuzipa kuongeza idadi ya shule za sekondari na kudahili idadi kubwa huku kukiwa hakuna mambo mengine ambayo yalipaswa kwenda sambamba na mpango huo.
Ili kuondokana na hali hiyo ya shule za Serikali kusuasua, lazima serikali ikubali kwamba kuna tatizo ili iweze kuchukua hatua haraka iwezekanavyo. Ukweli ni kwamba kunahitajika mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu la sivyo nchi yetuinaelekea kuwa taifa la wajinga.
Mamlaka husika zinapawa kufanya utafiti jinsi nchi nyingine zilivyofanikiwa kuendeleza elimu ambayo imeziwezesha kuzalisha wataalamu wa kutosha katika fani mbalimbali badala ya kuwa na idadi kubwa ya watu waliohudhuria shule badala ya kuelimika.
Kwa mfano, China ni taifa ambalo limepiga hatua takriban kila nyanja kutokana na kuwa mfumo bora wa elimu unaolenga kuzalisha wataalamu. Tukiangalia mfumo wa elimu ya sekondari nchini humo tunaona kuwa elimu hiyo imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni elimu ya sekondari ya juu na elimu ya sekondari ya awali.
Elimu ya sekondari ya juu inayotolewa baada ya kumaliza elimu ya sekondari ya chini. Pia kuna sekondari ya kawaida, sekondari ya ufundi na shule ya kozi maalumu. Elimu ya sekondari ya juu si ya lazima, hivyo wanafunzi wanatakiwa kulipa ada ili kuipata.
Ada hutofautiana kutokana na hali ya kiuchumi ya sehemu mbalimbali. Elimu ya sekondari ya juu nchini China huchukua miaka mitatu, ina masomo ya Kichina, hisabati, lugha za kigeni, fizikia, kemia, biolojia, upashanaji habari na kadhalika.
Sekondari nyingi za juu huendeshwa na serikali, lakini katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na sekondari za watu binafsi. China, wanafunzi wanatakiwa kufanya mtihani wa kujiunga na sekondari ya juu, na kwa mujibu wa matokeo ya mtihani na mapendekezo yao wanapokelewa na shule.
Mtihani wa kujiunga na sekondari ya juu hutolewa na idara za elimu za sehemu mbalimbali.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni, China ina sekondari za juu zaidi ya elfu 30 zenye wanafunzi milioni 30, ambao wanachukua asilimia 40 ya watoto wa rika moja.
Katika miaka ya hivi karibuni, idara za elimu za China zinajitahidi kukuza elimu ya sekondari ya juu ili kutosheleza mahitaji ya wanafunzi kujipatia elimu zaidi. Huu ni mfano mmoja tu unaoonyesha jinsi nchi hiyo ilivyo makini katika suala la elimu huku ikiwa na nia thabiti ya kuzalisha wataalamu wengi katika siku za baadaye.
Tukirejea katika matokeo ya mwaka huu ambayo zaidi ya asilimia 80 hawana vigezo vya kujiunga na kidato cha tano bna idadi kubwa kati ya hao hawana vigezo vya kuendelea na masomo kutokana na kuambulia daraja sifuri.
Hiyo inamaanisha kwamba idadi kubwa ya wanafunzi ambao wametumia miaka mine wakiwa shuleni sasa wanalazimika kubaki mitaani kutokana na mfumo wa sasa wa elimu ambao hauwapi fursa na kuendelea na masomo.
Mfumo wa elimu uliopo sasa unawahukumu wanafunzi kwa mitihani mbadala ya kuangalia mbinu ya kuwasaidia kuwajengea utaalamu unaoweza kuwanufaisha wao na taifa kwa ujumla.