Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 83
- 128
Hello, leo nakuletea enforcement mechanisms au mfumo wa utekelezaji wa haki za binadamu duniani na vyombo vinavyohusika (monitoring bodies).
Nitaanza na enforcement mechanisms chini ya Umoja wa Mataifa (UN), alafu kikanda (Regional) mfano Africa na kisha sub regional (Africa Mashariki), alafu nitamalizia na nyumbani (Tanzania).
Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke - Advocate Candidate,
zakariamaseke@gmail.com
(0754575246 WhatsApp).
Lakini kabla hatujaenda mbali, tufahamu kwanza nini maana ya Haki za Binadamu?
HUMAN RIGHTS (HAKI ZA BINADAMU) are the rights a person has simply because he or she is a human being. (Ni haki ambazo mtu anazo kwa sababu tu ni binadamu).
Ili kupata haki za binadamu, huhitaji kufanya kitu fulani maalum, zaidi tu ya kuzaliwa kama binadamu. Haki za binadamu hupatikana kiasilia (naturally), kila mtu anakuwa na haki za binadamu punde tu baada ya kuzaliwa.
Haki za binadamu hazitolewi kwa watu na serikali wala hazisubiri kuandikwa kwenye sheria, zenyewe zipo tu hata kabla ya sheria. Sheria inachokuja kufanya ni kuzitambua tu rasmi ili ziwe na nguvu kisheria.
Jaji Lugakingira aliwahi kusema, “Human rights are not gifts from the state, but are inherent in person by reason of his birth and are therefore prior to the state and law”. Kwamba haki za binadamu sio zawadi kutoka kwa dola (serikali), ila ni za asili kwa mtu kwa kuzaliwa kwake, na kwa hiyo haki za binadamu zilitangulia kuwepo kabla ya dola na kabla ya sheria.
Kisha akaendelea kusema kwamba, “Katiba za leo, mfano Katiba yetu Tanzania, zimetaja haki za binadamu kwenye vifungu vyake, lakini hiyo haimaanishi kwamba hapo ndipo haki za binadamu zimeundwa, ila (zilikuwepo tangu zamani), kule kuwekwa kwenye katiba ni ushahidi tu wa kuzitambua ili ziweze kutekelezwa (kudaiwa) Mahakamani” (Emphasis supplied). Soma kesi ya Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, 1995.
NATURE / CHARACTERISTICS OF HUMAN RIGHTS (SIFA ZA HAKI ZA BINADAMU).
1: Human Rights are inherent (ni za asili).
2: Human Rights are universal (zinafanana dunia nzima).
3: Human rights are inalienable (hazinyang’anyiki).
4: Human rights are indivisible (hazigawanyiki).
5: Interdependence & interrelated (zinategemeana na kuhusiana)
6: Human rights are recognized (zinatambuliwa).
Types/division (aina) of human rights:
1: Negative human rights.
2: Positive Human Rights.
Generation of human Rights:
1: The first generation of Human Rights (Civil & political rights)
2: Human rights of second generation (economic, social & cultural rights)
3: Human rights of the third generation (collective/solidarity rights).
Baada ya utangulizi huo mfupi, sasa tuendelee na ENFORCEMENT MECHANISMS (UTEKELEZAJI WA HAKI ZA BINADAMU
Tuanze na INTERNATIONAL LEVEL (KIMATAIFA). Tunaanza na Umoja wa Mataifa (United Nations).
THE UNITED NATIONS (UN) HUMAN RIGHTS SYSTEM:
Sheria inayoanzisha Umoja wa Mataifa (UN CHARTER), haielezi maana ya haki za binadamu ila inaweka azimio (commitment) na wajibu (obligation) kuhusu kulinda haki za binadamu na ina vifungu kadhaa vinavyohusu haki za binadamu. Ukisoma Preamble ya UN CHARTER.
Pia kwenye Article 1(3) ya sheria hiyo, inasema mojawapo ya malengo ya Umoja wa Mataifa ni kuhamasisha na kulinda haki za binadamu. Soma pia Article 13(1)(b), Article 56, 62(2) & (3) na Article 68. (Turudi kwenye enforcement).
HUMAN RIGHTS ENFORCEMENT AND MONITORING MECHANISMS UNDER UNITED NATIONS SYSTEM
Mfumo wa utekelezaji wa haki za binadamu chini ya umoja wa mataifa umegawanyika mara mbili:
(1) Mfumo wa kwanza ni UN CHARTER BASED MECHANISMS: Hizi ni njia zinazotumika ku enforce (kutekeleza( haki za binadamu ndani ya Sheria ya Umoja wa Mataifa (UN CHARTER.
Umoja wa Mataifa unatumia njia zifuatazo kushughulikia masuala ya haki za binadamu.
(i): UN HUMAN RIGHTS COUNCIL
(ii): THE UNIVERSAL PERIODIC REVIEW
(iii): THE SPECIAL PROCEDURE OF THE HUMAN RIGHTS COUNCIL
(iv): THE HUMAN RIGHTS COUNCIL COMPLAINT PROCEDURE
(i) TUANZE NA UN HUMAN RIGHTS COUNCIL:
UN Human Rights Council (Baraza la haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa) ni kitengo muhimu sana cha haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa. Baraza hili linashughulika na masuala muhimu ya Haki za Binadamu ikiwemo kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa watu binafsi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kuhusu ukiukwaji wa haki za Binadamu.
(ii) UNIVERSAL PERIODIC REVIEW (UPR):
Hii inahusu kupitia records za Haki za Binadamu za nchi wanachama wote wa Umoja wa Mataifa, kila baada ya miaka minne.
(iii): THE SPECIAL PROCEDURE OF THE HUMAN RIGHTS COUNCIL:
Special procedure ni independent human rights experts (wataalam huru wa haki za binadamu) wenye mandate (mamlaka) ya ku ripoti na kutoa ushauri juu ya haki za binadamu.
Special procedure inaweza kuhusisha mtu binafsi (individual) ambaye anaitwa special rapporteur au independent expert au linaweza kuwa kundi (a working group) linaloundwa na watu watano. Hao watu wanachaguliwa na UN Human Rights Council (Baraza la haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa) kutoka mabara mbali mbali mfano Africa, Asia, Europe, America.
Hao watu wanatembelea nchi mbalimbali na kutathimini hali (position) ya haki za binadamu kwenye nchi husika na kutoa ripoti. Kabla hawajaja nchi husika wanatuma barua kuomba waruhusiwe kuitembelea. Na wanaweza kuiandikia nchi barua kuomba wapewe maelezo ya jinsi gani nchi husika imetekeleza haki za binadamu.
(iv): THE HUMAN RIGHTS COUNCIL COMPLAINT PROCEDURE:
Huu ni mfumo wa kupokea malalamiko (addressing communications submitted by) kutoka kwa watu binafsi (individuals), makundi ya watu, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) na watu wote kiujumla ambao ni wahanga wa uvunjifu wa haki za binadamu au mtu yeyote ambaye ana taarifa sahihi (direct and reliable information) za uvunjifu wa haki za binadamu.
Malalamiko yanapelekwa Switzerland, Geneva. Lakini kuna vigezo ili taarifa au malalamiko yako yaweze kupokelewa.
CRITERIA FOR A COMMUNICATION TO BE ADMISSIBLE (VIGEZO):
(i) Taarifa yako isiwe imechochewa na ushabiki wa kisiasa (it is not manifestly politically motivated) na iwe sawasawa (consistent) na sheria ya Umoja wa Mataifa na sheria nyingine za kimataifa zinazohusu haki za binadamu.
(ii) Utoe ufafanuzi wa kina (factual description) kuhusu huo uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo haki zinazodaiwa kuvunjwa.
(iii) Usitumie lugha chafu (abusive language). Hata hivyo taarifa yako inaweza kupokelewa kama itakidhi vigezo vingine baada ya maneno mabaya kuondolewa.
(iv) Taarifa yako isiwe habari za kusikia tu kwenye media.
(v) Isiwe ni kesi ambayo tayari imefanyiwa kazi na chombo kingine cha haki za binadamu kimataifa.
(vi) Lazima uanzie kwanza kwenye mifumo ya ndani ya nchi kabla ya kuruka na kwenda huko nje (domestic remedies should have been exhausted), isipokuwa tu kama unadhani nafuu zilizopo ndani ya nchi hazitoshi au zitakuchelewesha bila sababu (unreasonably prolonged).
(Hiyo ndio UN CHARTER BASED MECHANISM).
2: Sasa tuangalie aina ya pili, UN TREATY BASED MECHANISMS: - NJIA zinazotumika ku enforce haki za binadamu NDANI YA MIKATABA MINGINE YA HAKI ZA BINADAMU KIMATAIFA).
Ukiacha ‘UN CHARTER,’ bado kuna sheria au (conventions) mikataba mingine mingi ya haki za binadamu ambayo pia imeanzishwa chini ya hao hao UN (umoja wa mataifa). Ndio maana tunaiita “UN TREATY based” mechanisms.
Hii ni mifumo ya kutekeleza haki za binadamu ambayo inapatikana ndani ya sheria za mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu ambapo muasisi wake bado ni Umoja wa Mataifa (UN), kwa hiyo sheria au mikataba hii ni kwa ajili ya dunia yote (nchi yeyote inaweza kusaini). Zifuatazo ni njia zinazotumika kutekeleza hiyo mikataba:
(i) Reporting System.
(ii) Individual complaint (communication).
(iii) Inter states complaint system.
(iv) Inquiries.
(i) REPORTING PROCEDURE:
Hapa nchi wanachama (Serikali) kwenye mkataba husika wanatakiwa kuwasilisha ripoti kila baada ya kipindi fulani kwenye kamati husika (relevant committee), kuonesha hatua walizochukua kutekeleza haki za binadamu na changamoto zozote walizokutana nazo.
Kando na ripoti ya Serikali, kamati zinaweza pia kupata ripoti kutoka kwenye vyanzo vingine kama mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), Taasisi za Umoja wa Mataifa (UN agencies), Vyombo vya habari, Taasisi za elimu n.k.
(ii) INTER STATES COMPLAINT SYSTEM:
Hii ni njia ambayo mkataba unaruhusu nchi wanachama kwenye mkataba (Convention) kupeleka malalamiko (complaint) kwenye chombo husika, kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu uliofanywa na mwanachama (nchi) nyingine. Kwa hiyo nchi inashtakiwa na nchi nyingine (mwanachama mwenzake). Soma Article 21 ya Convention against Torture (CAT), Articles 11-13 ya ICERD na Articles 41 - 43 ya ICCPR.
(iii) INQUIRIES:
Hapa kamati kwenye mkataba husika inaamua yenyewe kufanya uchunguzi, baada ya kupokea maelezo ya kuaminika (reliable information) yanayoashiria kwamba kuna uvunjifu wa mkataba wa haki za binadamu kwenye nchi fulani. Uchunguzi unaweza kufanywa kwenye nchi wanachama tu (States Parties).
(iv) INDIVIDUAL COMPLAINT (COMMUNICATION) SYSTEM:
Hii ni kwamba, mtu binafsi (individual) anaruhusiwa kupeleka moja kwa moja malalamiko yake kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu kwenye kamati za kimataifa. Kila mkataba una kamati yake inayopokea na kusikiliza malalamiko. Sasa itategemea na haki ambazo wewe unasema zimevunjwa ni za Mkataba au Convention ipi, kwa sababu pia sio mikataba yote inaruhusu mtu kufanya hivyo.
WHO CAN COMPLAIN (NANI ANAWEZA KULALAMIKA)?
Anayeweza kulalamika, ni mtu yeyote (any individual) ambaye anadai kwamba haki zake kwenye mkataba fulani wa haki za binadamu zimevunjwa na nchi ambayo ni mwanachama kwenye huo mkataba. Pia unaweza kumtuma mtu mwingine tofauti na wewe (third party) akalalamike kwa niaba yako.
VIGEZO NA MASHARTI:
Ili kamati husika iweze kupokea malalamiko yako, lazima ukidhi vigezo vifuatavyo:
(i) Ridhaa ya mhusika (consent of the victim). Kama umepeleka malalamiko kwa niaba ya mtu mwingine basi uoneshe ridhaa yake.
(ii) Lazima uoneshe kwamba wewe binafsi umedhurika na huo uvunjifu wa haki za binadamu. (Being a victim of the alleged violation).
(iii) Uvunjifu unaodaiwa kufanyika uwe unaendana na haki zilizoko kwenye Mkataba. (Compatibility with the provisions of the treaty).
(iv) Malalamiko yasiwe yamechochewa na nia ovu (ill motive) au ushabiki wa kisiasa.
(v) Timing of the violation (suala la muda). Lazima huo uvunjifu uwe umetokea baada ya sheria husika kutungwa na sio kabla. Isipokuwa (unless) kama ni uvunjifu endelevu, kwamba ulikuwepo kabla ya mkataba husika na umeendelea kuwepo hata baada ya mkataba.
(vi) Exhaustion of local remedies. (Lazima uanze kwanza kwa kutafuta nafuu zote zilizopo ndani ya nchi yako kabla ya kuruka kwenda huko nje).
(vii) The claim should not be abuse of complaint process. Usitumie vibaya mfumo uliopo mfano kurudia rudia kesi ile ile, labda (unless) kama walalamikaji wawe ni tofauti n.k.
(viii) Hakikisha kesi yako haijafunguliwa kwenye kamati au chombo kingine chochote cha kimataifa.
(ix) Hakikisha nchi unayotoka ni mwanachama kwa maana kwamba imeridhia na kusaini mkataba husika na inatambua mamlaka (competence) ya kamati husika kupokea na kusikiliza malalamiko.
(x) Sufficient evidence (uwe na ushahidi wa kutosha na sio taarifa tu za mtandaoni au vyombo vya habari).
(xi) The complaint must not be anonymous. (Malalamiko yasitoke kwa mtu asiyejulikana). Lazima utaje jina lako hata kama hutaki kujulikana bado utatakiwa kutaja jina lako ila utaomba liwe siri.
(xii) Time limit for lodging complaints (muda wa kupeleleka malalamiko). Baada ya kumalizana na Mahakama za ndani unatakiwa kulalamika ndani ya miezi sita.
(xiii) Jurisdiction (mamlaka kisheria). Ili kamati husika iwe na mamlaka ya kukusikiliza, inatakiwa uwe ulikuwepo ndani ya mipaka ya nchi husika wakati uvunjifu wa hizo haki unatokea. Ingawa kuna mazingira hata ukiwa nchi nyingine, bado Kamati itakuwa na mamlaka ya kukusikiliza. Mfano kama huo uvujinfu wa haki umefanywa huko nje dhidi ya Watanzania lakini na mamlaka au kiongozi wa nchi ya Tanzania, mfano ofisi za Ubalozi wa Tanzania, huo uvunjifu bado uko ndani ya jurisdiction.
Ndugu msomaji hizo ndizo baadhi ya njia ambazo zinatumika kutekeleza haki za binadamu kwenye mikataba ya haki za binadamu duniani (kimataifa).
Sasa tuangalie vyombo au mamlaka zinazohusika kutekeleza hizo haki ndani ya mikataba ya haki za binadamu.
INTERNATIONAL (UN) HUMAN RIGHTS MONITORING BODIES:
Utekelezaji wa sheria au mikataba hii mara nyingi husimamiwa na kamati huru au Mahakama zilizoanzishwa ndani ya mkataba/sheria husika (Human rights treaty bodies). Nikisema Kamati, kwa hapa namaanisha chombo maalum ambacho kimeundwa na mkataba husika wa haki za binadamu kutekeleza vifungu vya huo mkataba.
Kuna mikataba (sheria) nyingi na kila mkataba una kamati (committee) yake au monitoring body yake (kwa pamoja ndo tunaziita TREATY BODIES). Soma hapa chini baadhi ya Mikataba na kamati zinazosimamia mikataba hiyo.
(i) The International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR), 1966. Kamati husika kwenye huu mkataba inaitwa the “Human Rights Committee (CCPR).”
(ii) The International Covenant on Economic, Social and Cultural Rights (ICESCR), 1966. Kamati yake inaitwa the “Committee on Economic, Social and Cultural Rights (CESCR).”
(iii) The United Nations Convention on the Rights of Persons with Disabilities (CRPD), 2006. Kamati yake inaitwa the “Committee on the Rights of Persons with Disabilities (CRPD).”
(iv) The Convention against Torture and Other Cruel, Inhuman or Degrading Treatment, 1984. Kamati yake inaitwa the “Committee Against Torture (CAT).”
(v) The United Nations Convention on the Rights of the Child (CRC), 1989. Kamati yake inaitwa “the Committee on the Rights of the Child (CRC)”.
(vi) The United Nations Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination against Women (CEDAW). Kamati yake inaitwa “Committee on the Elimination of Discrimination against Women (CEDAW).”
(vii) The International Convention on the Elimination of All forms of Racial Discrimination, 1965. Kamati yake inaitwa the “Committee on the Elimination of All forms of Racial Discrimination (CERD).
(viii) Na kadhalika.
Mpaka hapo tumemaliza MFUMO WA UTEKELEZAJI WA HAKI ZA BINADAMU (DUNIANI), na vyombo vinavyohusika kuzitekeleza (MONITORING BODIES), KWENYE SHERIA YA UMOJA WA MATAIFA NA MIKATABA MINGINE.
Sasa tuje kwenye upande wa ukanda (Regional) au mabara moja moja kama vile Africa, Ulaya, na sub regional kama Africa mashariki na mwisho tutamalizia na nyumbani Tanzania.
REGIONAL HUMAN RIGHTS SYSTEM (MFUMO WA HAKI ZA BINADAMU KIKANDA)
Kwa upande wa Kanda (Regional Human Rights system) kuna mifumo mikuu mitatu:
1: The Council of Europe ambayo inahusika na haki za binadamu Ulaya (European Union human rights system).
2: Organization for American States (OAS) ambayo inahusika na haki za binadamu Marekani (Inter America human rights system)
3: African Union (AU) ambayo inahusika na haki za binadamu kwa Africa (Africa Human Rights System).
Kasoro Asia tu, mabara mengine yana mfumo maalum wa haki za binadamu (Asia does not have a defined human rights protection system).
Lengo la regional human rights laws ni ku supplement international human rights mechanisms (kuziongezea nguvu sheria za kimataifa). Kwa ajili ya muda sitaongelea hayo mabara mengine, twende moja kwa moja Africa.
AFRICAN HUMAN RIGHTS SYSTEM:
Mkataba wa haki za binadamu Africa nzima unaitwa, “THE AFRICAN CHARTER ON HUMAN AND PEOPLE’S RIGHTS” kwa kifupi tunaita, “AFRICAN CHARTER.” Huu ndio Mkataba mkuu wa Haki za Binadamu Afrika.
Mkutano wa kuuandaa (draft) ulifanyika nchi ya Gambia, mji wa Banjul na ndio maana African Charter pia inaitwa “Banjul Charter”, kwa sababu ya historia yake.
Sheria hii au mkataba huu ulipitishwa (kuwa adopted) rasmi na baraza kuu (Assembly) la UMOJA WA AFRICA (the Organization of Africa Unity) (OAU) ambayo kwa sasa inaitwa African Union (AU), tarehe 28 June, 1981 nchini Kenya (Nairobi). Na baada ya kusainiwa na nchi nyingi Africa, sheria hii ikaanza kazi (came into force) tarehe 21, October 1986. Kufikia mwaka 1999, mkataba huu ulikuwa umesainiwa na nchi zote za umoja wa Africa (AU).
Kando na African Charter, kuna mikataba mingine midogo midogo ambayo imetengenezwa kufafanua au ku supplement vifungu vya mkataba huo, mfano;
(i) The African Charter on the rights and welfare of the child:
Huu mkataba unahusu haki za watoto. Ulikuwa adopted mwaka 1990 na ukaanza kufanya kazi (came into force) November 29, 1999. Mkataba huu umeanzisha kamati kwa ajili ya kulinda na kutetea haki za watoto Africa. Kamati hiyo inaitwa “The African Committee of Experts on the Rights and Welfare of the Child (African Children’s Rights Committee). Makao yake Makuu ni Addis Ababa, Ethiopia.
Kamati hii ina mamlaka ya kupokea, kusikiliza na kuamua malalamiko (communications) kutoka kwa watu binafsi (individuals), NGO’s, na nchi wanachama. Pia nchi wanachama (States Parties) wanatakiwa kupeleka ripoti zinazoonesha hatua walizochukua kutekeleza sheria au mkataba huo.
(ii) Protocol on the African Human and People’s Rights Court. Ilikuwa adopted Ouagadougou, Burkina Faso, tarehe 9, June 1998 na kuanza kutumika rasmi tarehe 25, January 2004. Hii inaanzisha Mahakama ya Haki za binadamu Africa.
(iii) Protocol to the African Charter on the Rights of Women in Africa (Women's Protocol). Huu mkataba unahusu haki za wanawake. Ulikuwa adopted Maputo, Mozambique, tarehe 11 July 2003 na kuanza kazi tarehe 25, November 2005.
Ziko na sheria au mikataba mingine mingi sana Africa, kama vile the Constitutive Act of the AU 2000, Protocol on the Pan-African Parliament 2001, Protocol on the Peace and Security Council 2002, Statute of the Economic, Social and Cultural Council 2004, Convention on the Prevention and Combating of Terrorism 1999, Convention on the Conservation of Nature and Natural Resources 2003, Convention on the Prevention and Combating Corruption 2003, African Charter on Democracy, Elections and Governance 2007, the Convention for the Protection and Assistance of Internally Displaced Persons 2009 na kadhalika.
Sitajadili sheria zote hizo, turudi kwenye mkataba mkuu (main), “THE AFRICAN CHARTER ON HUMAN AND PEOPLE’S RIGHTS” kwa kifupi tunaita, “AFRICAN CHARTER”* na jina lingine “BANJUL CHARTER.”
SIFA ZA MKATABA HUU:
Huu mkataba ndugu msomaji umewashangaza hata wazungu, una sifa za kipekee (unique features) ambazo hata mikataba mingine yote ya haki za binadamu duniani haina. Na hii ni kwa sababu mkataba huu ulitungwa kwa kuzingatia mazingira ya nyumbani (it was drafted taking into account African Culture) na ulilenga kushughulikia mahitaji ya Waafrika (was specifically directed towards African needs).
(i) The Charter contain collective rights (haki zote pamoja). Tunaiita holistic approach.
Tofauti na mikataba mingine utakuta civil and political rights zina mkataba wake (mfano ICCPR), na economic, social and cultural rights zina mkataba wake (mfano ICESCR), lakini mkataba wa haki za binadamu Africa umezichanganya zote ndani ya sheria moja (within the single instrument). Kwa Africa, hii ina maana kwamba aina zote za haki ni indivisible (hazigawanyiki).
(ii) The concept of People's Rights (group rights). African Charter ndio mkataba pekee wa haki za binadamu ambao una haki za jumla kwa watu wote (Rights of the African masses), tunaziita third generation rights au rights of solidarity. Kama vile haki ya maendeleo (people's right to development), free disposal of natural resources, self determination n.k. (Soma Article 19 - 24 ya African Charter).
(iii) Individual duties. African Charter ndio mkataba pekee wa haki za binadamu ambao pia unampa mtu wajibu katika nyanja ya kimataifa (duties are imposed to individuals as a matter of international obligation). Ni haki na wajibu, kwa pande zote mbili, serikali na mtu binafsi. Mfano paragraph sita (6) ya preamble (utangulizi).
(iv) No derogation is allowed (African Charter does not contain a derogation clause). Mkataba huu hautoi mwanya au nafasi yoyote ya kukiuka haki zilizomo haijalishi ni dharura au mazingira gani. Kuna sababu moja tu - Article 27(2).
AFRICAN HUMAN RIGHTS ENFORCEMENT & MONITORING BODIES:
Sasa tuangalie jinsi haki za binadamu zinavyotekelezwa Africa, tutajikita zaidi kwenye sheria kuu ya African Charter. Je, ni njia gani zinatumika na ni mamlaka gani zinafanya hiyo kazi kwa maana ya monitoring bodies.
Vifuatavyo ni vyombo au mamlaka zinazohusika kutekeleza haki za binadamu kwenye African Charter:
(i) African Commission on human and people's rights.
(ii) The African Court on Human and People's Rights.
(iii) African Court of Justice and human Rights
(i) AFRICAN COMMISSION ON HUMAN AND PEOPLE'S RIGHTS:
Commission (Tume) hii imeanzishwa chini ya Article (Ibara) ya 30 ya African Charter. Majukumu yake yapo Article 45 ya sheria hiyo hiyo. Mojawapo ni kupokea malalamiko (communications / complaints) yanayohusu haki za binadamu Africa.
NJIA ZA ZINAZOTUMIWA NA AFRICAN COMMISSION
(i) State Reporting Mehanism.
Nchi wanachama kwenye African Charter wana wajibu wa kupeleka ripoti kwenye Commission jinsi ambavyo wametekeleza haki zilizomo kwenye mkataba huo. Article 62.
(ii) Inter state procedure.
Kama nchi moja inaamini kwamba nchi nyingine ambayo pia ni mwanachama wa African Charter imevunja vifungu vya African Charter, basi inaweza kuiarifu hiyo nchi au kuishtaki moja kwa moja kwenye Commission. Article 47.
(iii) Lodging a complaint (communication).
Commission inapokea malalamiko kutoka kwa mtu binafsi, NGO au nchi. Articles 47 - 54 of the African Charter.
Vigezo na masharti (admissibility criteria) vipo Article 56, mfano utaje jina la mlalamikaji, usitumie lugha za kutukana, isiwe ni mambo ya kusikia kwenye vyombo vya habari pekee, hakikisha umeanzia na kumalizana na Mahakama za ndani kwanza (exhaustion of local remedies) ingawa kuna mazingira unaweza kusikilizwa hata kama hujaanzia nyumbani, pia hakikisha uko ndani ya muda n.k.
Commission inaishia kutoa mapendekezo tu (recommendation), kwamba inatoa uamuzi, ila uamuzi huo hauibani nchi husika (Commission does not have binding decision), ila itapeleka huo uamuzi (mapendekezo) kwenye Baraza la wakuu wa nchi za Africa (to the Assembly of African Heads of States and Governments) kwa ajili ya uamuzi wa mwisho. Na hii ndo inahafifisha ulinzi wa haki za binadamu kwenye Sheria hiyo, maana inategemea good will of political leaders.
(ii) MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU AFRICA (THE AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLE'S RIGHTS):
Imeanzishwa na Additional Protocol to the Banjul Charter ya tarehe 9 June, 1998 ambayo ilianza kutumika 25 January 2004. Makao yake makuu yako Arusha, Tanzania. Mahakama hii inaisaidia Commission kulinda haki za binadamu Africa.
Utofauti wake na tume (Commission) ni kwamba, hii Mahakama ina uwezo wa kutoa uamuzi wa mwisho na ambao ni binding decisions (unaoibana au kuifunga Serikali). Mahakama ya Africa inapokea kesi kutoka kwa Tume (African Commission) na nchi wanachama. Soma Article 5.
Pia inapokea kesi kutoka kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) na watu binafsi wanaweza kwenda moja kwa moja kufungua kesi kama nchi unayoshtaki inatambua mamlaka ya Mahakama kupokea kesi kutoka kwa mtu binafsi (has made declaration to accept the competence of the Court to receive complaint from individuals and NGO’s) under Article 34(6) of the Protocol. Hii pia inahafifisha utekelezaji wa haki za binadamu kwenye Sheria hiyo, maana ni nchi chache sana zimekubali hicho kitu. (Tanzania na Rwanda zimejiondoa kwenye mfumo huo).
Raia wa nchi ambayo imesaini na kukubali mamlaka ya hii Mahakama wana uwezo wa kunyoosha moja kwa moja kwenda kuishtaki Serikali kwenye Mahakama ya Africa hata bila kupitia kwanza kwenye Commission.
Nchi ambayo imesaini tu Protocol lakini haitambui mamlaka ya hii Mahakama ya Africa (yaani haijafanya declaration) chini ya Article 34(6), au imejitoa, raia wake lazima waanzie kwenye Commission kwanza na Commission ndo inaweza baadae kuipeleka hiyo kesi Mahakama ya Africa.
Na nchi ambayo hata kusaini hiyo Protocol tu haijsaini, raia wake wanaweza kusikilizwa na Commission tu.
(iii) AFRICAN COURT OF JUSTICE AND HUMAN RIGHTS:
Hii imeanzishwa na Protocol on the Statute of the African Court of Justice and Human Rights, July 2008. Haijaanza kufanya kazi maana kulikua na nchi tatu tu zilizosaini.
REGIONAL HUMAN RIGHTS AND RIGHTS:
Sasa tumebakiza UKANDA WA AFRICA MASHARIKI (EAC HUMAN RIGHTS SYSTEM) na Tanzania.
Hapa nitakutajia sheria tu ukasome.
Kwa Afrika Mashariki soma The Treaty for the Establishment of the East African Community na kwa Tanzania soma sheria zifuatazo Katiba (ya Tanzania na ya Zanzibar), soma the Basic Rights and Duties Enforcement Act (BRADEA) na kanuni (rules) zake. Kuna mambo mengi sana hapa mazuri na kesi za kutosha zinazovutia. Kama unapenda haki za binadamu utasoma.
-----MWISHO----
Natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili. Unaruhusiwa tu kusambaza lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.
Disclaimer: Lengo la hii makala ni kutoa elimu kwa jamii. Huu sio ushauri wa kisheria kwa mtu yeyote. Ikiwa utaamua kufanya chochote kwa kufata haya maelezo na ukapata hasara, mwandishi wa maelezo haya hatawajibika kwa vyovyote vile. Kama unahitaji ushauri wa kisheria wasiliana na Mawakili.
(Nakaribisha maoni na nyongeza, ikiwa kuna sehemu hujaelewa omba ufafanuzi au uliza swali, kuuliza ni bure kabisa).
Imeandaliwa na kuletwa kwako nami, Zakaria Maseke,
Advocate Candidate,
(0754575246 - WhatsApp).
zakariamaseke@gmail.com.