Mfumo wa kutahini wa NBAA utazamwe upya

Mfumo wa kutahini wa NBAA utazamwe upya

Joined
Aug 10, 2011
Posts
35
Reaction score
13
MFUMO WA KUTAHINI WA NBAA UTAZAMWE UPYA
Naishangaa sana NBAA. Wakati nchi nyingine za muungano wa jumuia ya Afrika Mashariki zikifanya kila juhudi kuhakikisha wananchi wake hawaachwi nyuma kielimu,NBAA yenyewe inafanya kila juhudi za kupunguza watu wenye CPA hapa Tanzania.

Wakati nchi kama Kenya sasa hivi imeanza kuwapa kila mtoto wa darasa la kwanza Laptop yake huku Tanzania hata Yule wa Chuo kikuu haijulikani atapewa Laptop lini.

Jumuia ya Afrika Mashariki inakaribia kuanza shughuli zake zote kama jumuia.Ikiwemo watu kusafiri nchi moja hadi nyingine bila ya kikwazo chochote yaani itakuwa hakuna kudaiwa passport wala kibali cha kusafiria kutoka nchi moja kwenda nyingine, tunachokiona hapa ni kwamba jumuia ya Afrika Mashariki ikianza shughuli zake bila kikwazo basi Watanzania wengi watapoteza ajira zao. Kwa sababu watanzania wengi hawana vyeti vya kazi wanazozifanya sasa.Utakuta mtu anajiita Mhasibu Mkuu wa idara au wizara au kampuni fulani lakini CPA hana.Kwa nini hana ? Alishafanya sana mitihani ya CPA lakini hakufaulu kutokana na ugumu wa mitihani hiyo.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba serikali itafute namna nyingine ya kuongeza ufaulu kwa watahiniwa wa mitihani ya NBAA , la sivyo jumuia ya Afrika Mashariki ikianza rasmi , kazi zote za masuala ya uhasibu na ukaguzi wa mahesabu zitachukuliwa na wakenya na waganda kutokana na ukweli kwamba huku Tanzania watu wenye CPA ni wachache sana kutokana na ufaulu mdogo sana wa watahiniwa wa mitihani ya NBAA.

Mpaka sasa hapa Tanzania watu wenye CPA wapo elfu tano na hiyo idadi imefikiwa kuanzia tangu mwaka 1972 ambapo hiyo NBAA ilipoanza kutahini mitihani ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu.Kati ya hao elfu tano wenye CPA , wapo ambao tayari wameshakufa siku nyingi,wapo ambao wana CPA lakini hawazitumii kufanya kazi za uhasibu(kwa mfano ma-lecturer), wapo ambao wana CPA lakini wameshaondoka hapa nchini siku nyingi.

Tunaiomba serikali iitazame upya utungaji,ufanyaji ,usahihishaji na upangaji wa matokeo wa hii bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu-NBAA la sivyo milango ya jumuia ya Afrika Mashariki ikifunguliwa, basi watanzania wengi watapoteza ajira zao zinazohusiana na uhasibu na ukaguzi wa mahesabu kutokana na kukosa CPA .
 
Back
Top Bottom