Mfumo wa Lechantre vs Masoud Djuma upi ni bora zaidi?

Last emperor

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
10,351
Reaction score
9,855
Salaam wakurugenzi, Nimekuwa nikifatilia kwa makini ligi ya vpl toka ianze,hususani timu ya simba. Toka ligi ianze timu ya simba ilianza kufundishwa na Omog, chini ya Omog timu ilicheza mpira wa kasi na pasi fupifupi.Tatizo likaonekana kuwa timu haishindi kwa goli nyingi,ushindi unakuwa wa tabu na mashaka.Viongozi wakaona wafanye mabadiliko ya benchi la ufundi,wakamleta Masoud Djuma ili aweze kama msaidizi wa kocha mpaka atakapopatikana kocha mkuu. Kipindi kifupi timu ipo chini ya Masoud timu ilikuwa inashambulia zaidi na timu ikawa inaadhibu timu pinzani 4g kila wanapokutana nazo,tatizo tu ikawa upande wa beki sio imara zinaweza kurudi kama tulivyoona kwa Stand United. Akaletwa Lechantre, tukaanza kuona timu imekuwa imara kwenye beki na viungo,lakini inashinda kwa tabu, kagoli kamoja kamoja tu.Tumerudi kule kule.Naomba kuuliza mfumo wa Lechantre vs Masoud upi ni bora kwa Simba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…