DOKEZO Mfumo wa malipo ya Parking wa TeRMIS bado una harufu ya ujanja wa upigaji fedha

DOKEZO Mfumo wa malipo ya Parking wa TeRMIS bado una harufu ya ujanja wa upigaji fedha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hizi "Parking Fee" zimekuwa na Upigaji ambao haueleweki.

Nimejaribu tu kuingia katika TeRMIS (termis.tamisemi) nikaweka namba yangu ya gari ambayo nimeagiza na imesajiliwa Tarehe 6 mwezi wa 2, 2025 lakini nilishtushwa kuona nadaiwa Pesa ya Parking Mwaka 2024 Mwezi wa 12 na Januari 2025, ambapo inasema maeneo ni Lumumba.

Sijawahi fika huko Lumumba na najiuliza gari ina usajili wa Mwezi wa 2, 2025 lakini deni ni la Mwaka 2024. Mawakala wa Parking wamekuwa na Upigaji ambao ni utakatishaji Fedha.

Gari yangu nyingine inadaiwa Tsh. 86,000 na ambayo maeneo ulipoandikiwa sijawahi kufika.

Tunaomba Mamlaka husika iingilie kati hili ili kuepusha kupotea imani ya walipa kodi. Maana huu ni kama utapeli

1000591983.jpg
 
Mkuu hawa jamaa ni hatari kupita hatari yenyewe yaani kwa ufupi ni ukizubaa umeliwa
 
Mimi mwenyewe nimelipia parking wakati ule mwaka jana 50,000/= malipo ya mwezi na bado nikaskaniwa na deni likafikia 75,000/= juu ya kuwa nimelipa, lau nisingeulizia naona lingefika hadi laki na ushee, hilo deni mpaka leo lipo na mini sililipi kwa kuwa risiti ninayo na nikienda ofisini kwao eti na wao wanasema hawajui ni lazima nilipe, yaani ni wizi wa mchana kweupeeeeeee
 
Kumbe unafanya kazi Kuna siku nikiangalia nadaiwa Ila sikujali nikajua wamekosea tu...NI mfumo wa kishenzi
 
Back
Top Bottom