realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Tanzania Mpya ndani ya Miaka Mitano hadi Ishirini na tano ijayo: Kupunguza migogoro ya Ndoa na Kesi za Mirathi.
(Picha kutoka Mtandaoni)
Miaka ya hivi Karibuni katika Mitandao ya kijamii kuliandikwa visa vingi sana vikihusisha baadhi ya wanawake waliokua ndani ya ndoa kushindwa kesi zilizokua zikihusiana na Mirathi.
Cha kushangaza zaidi watu hawa walikua wamefunga ndoa huku picha zao zikiwa katika mitandao ya kijamii na wengine kufikia hatua za kuzaa na watoto.
Tatizo linakuja pale wanaume wanapofariki hasa linapokua suala la Wosia na Mirathi mambo mengi huibuka hapo.
Mambo yenyewe ni kama kabla ya kuingia kwenye ndoa mpya mtu huyu hakutalikiana na Mume au Mke wake kisheria.
Kama ilikua hivyo ilikuaje Mtumishi wa Mungu kutoka kanisa lingine akafungisha ndoa nyingine bila kujua ukweli wa mambo huku akijua kabisa anafungisha ndoa kati ya mtu mzima mwenye familia nyingine na mtu ambaye ni kama mwanae?.
Wanasheria au Mawakili wa kujitegemea na wa serikali wanq mifumo inayowatambua ili kuepukana na vishoka watakaojifanya wao ni mawakili.Wameenda mbali zaidi kuwa wakili ambae hajalipia leseni yake ataonekana kupitia mfumo huo.
Sasa Kutokana na uelewa mdogo wa Sheria zetu kwa baadhi ya wananchi ilipaswa Mfumo huo uwepo wa kumjua mwenye ndoa ikiwamo ndoa zilizo hai, walizotalikiana kisheria na ambao wako kwenye mchakato wa kuachana au kufunga ndoa.
Mfumo huu utasaidia kupunguza migogoro isiyo na ulazima kwani Kama mtu amefunga ndoa Arusha akasafiri kikazi Mkoa Mwingine akataka kufunga ndoa huko Mchungaji ataingia kwenye mfumo ili kujiridhisha kama huyu mtu kweli haba ndoa.
Kutangaza tu kanisani haitoshi kwani sasa hivi Dunia iko kiganjani lazima mfungishaji ajiridhishe.
Hii pia itapunguza utapeli wa ndoa kwa baadhi ya wanawake kupotezewa muda na baadhi ya wanaume walioko kwenye ndoa.
Italeta heshima kwenye ndoa pia.
Itapunguza kesi mahakamani zisizokua na tija.
Itapunguza msongo wa mawazo na kusaidia familia kustawi.
Familia zitajikita katika uzalishaji mali badala ya kushinda mahakamani.
Itaongeza thamani ya Ndoa.
Thamani ya vyeti vya Ndoa kuongezeka.
Mirathi pia itagawanywa kwa usawa.
Mjue Mwenye ndoa kidijitali kupunguza migogoro ya Ndoa na kupunguza kesi za mirathi ndani ya miaka mitano hadi ishirini na tano ijayo.

Upvote
1