Mfumo wa ruzuku ya mbolea unatatiza wakulima na wafanyabiashara

Mfumo wa ruzuku ya mbolea unatatiza wakulima na wafanyabiashara

Ridomil gold

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2020
Posts
2,790
Reaction score
2,232
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema sekta hiii ipo hoi taabani sana hasa kwenye upande wa waziri na watendaji wake.

Leo tumeona wafanya biashara wanao toa ruzuku ya mbolea wamefutiwa kama 700 na kitu katika maeneo tofauti tofaut hakika hii kitu BASHE anatakiwa ajue tu kuwa wakulima wanapata tabu sana

Je, walitoa elimu kuhusu mfumo ya ruzuku kwa mawakala unavyofanya kazi au wamewafutia tu kisa wao wana nguvu vip mawakala walio kuwa na mbolea? I mean stock je wanapeleka wapi?

Na ukiwafutia leseni je utaratibu wa kurudi kwa biashara ukoje na je wakulima wao shida ya mbolea ikoje? Wafanya biashara kwanza wengi wana mikopo ya ma benk na mikopo ya mbolea kwa makampuni je inakuaje.

TFRA jitazameni na mchunguze kuwa huuu mfumo unatesa wakulima na kuwasumbua wafanya biashara na wizara hii pia BASHE HUTOSHI MKUU ANA PUNGUZA MIHEMUKO UNAUMIZA WAKULIMA NA WAFANYA BISHARA
 
Huko si ndiko kumepelekwa Bilions of Money za BBT
 
Wengi walikuwaaa wanauza mbolea kihun sana...bashe nenda na bit
 
Mimi ni mfanya biashara wa mbolea. Tuwe wakweli, serikali haijajipanga kuhusu hizo ruzuku na wanatutafutia sababu. Ukiangalia makosa waliyotuambia ni kuuza kwa kutofuata taratibu ambao hawajasema ni upi.

Serikali haina pesa kwani pesa yenyewe ya ruzuku walitegemea kupewa mkopo toka Banki ya Afrika ambayo nayo ilikuja kujitoa katika kulipa mbolea ya ruzuku na ndio maana wanatuzungusha hadi sasa kwenye malipo na hata hii kutufutia uwakala ni gheresha tu.

Mimi nina mbolea stoo kwangu na sijui nitazifanyia nini? Nimempigia Ngailo DG wa TFRA hana majibu. Mameneja wote wa TFRA hawana majibu. Kimsingi walianza kutufanyia uhuni toka mwezi wa pili kwa kushusha bei ya mbolea na kutotulipa hizo top up za mbolea. Tumefanya kazi kwa uaminifu ila kulikuwa na changamoto ya mfumo. Leo nascan namba ya mkulima, mfumo hautumii sms kwake na unakuja kutuma baada ya mwezi, mkulima analalamika hajachukua mbolea wakati alishachukua.

Usione watu wanaitwa Madr ila kichwani ni empty kabisa sawa na P3 tu.
 
Back
Top Bottom