Mfumo wa sasa wa uchumi haumsaidii mfanyabiashara wa kati Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Mfumo wa sasa wa uchumi haumsaidii mfanyabiashara wa kati Tanzania. Wafanyabiashara wa kati ni wale ambao wanaitaji msaada wa Bank ili kuweza kukuza biashara zao. Mfumo wa sasa ni mzuri kwa billionea ambao hawahitaji pesa za bank za Tanzania kuendesha biashara zao na wafanyabiashara wa chini sana kama machinga au bodaboda ambao hawalipi kodi wala kufuata sheria.

Kama tunataka uchumi ukuwe na biashara zikue ni lazima tuwasaidie wafanyabiashara wa kati kwasababu wenyewe ndiyo wanatoa ajira nyingi mfano wauza maduka, gas stations, wenye mabasi ya dalala, maduka ya vifaa, wenye taxi, nyumba za kupanga, daladala, maduka ya nguo, vinyago, wauzo nafaka, wenye malori na magari ya mizigo. Hapa naongelea wenye magari, nyumba chache.

Je shioda gani wanazipata

1. Mikopo ya bank ni ya 15%-25% na ni lazima ulipe hii ni ngumu sana kwasababu mkopo unapanda hata kama huna faida
2. Tax: Tax ya Tanzania iko juu sana na hawa hawawezi kukwepa kama machinga na mabilionea wanaogopeka hivyo TRA wanategemea hii group.
3. Serikali: Kunyanyaswa na kuwa na vibali vingi ambavyo vinaongeza gharama, kodi ambazo haziishi


Hivyo salamu zangu kwa mawaziri ni kufanya jitihada kupunguza riba na kupunguza gharama zisizo za msingi. Nitatoa jinsi ya kupunguza riba.
 
Hilo la mkopo sijui, lakini TAX?

Kama hauna faida haulipi TAX. Kumbuka hilo.
 

Umenyimwa mkopo na bank fulani? hao wafanyabiashara wa kati waliowatangulia ndio walioharibu so bank zinwaogopa wafanyabishara wa kati.

Elimu ya mikopo ina hitajika

wateja wakukopa hawapo ndio maana unaona benki ya biashara inakuwa benki ya mikopo ya nyumba, n.k
 
Mimi nimewahi kufanya biashara ya dada dala na maduka Tanzania. Kodi hata kama una faida utalipishwa kwasababu Tanzania sio kama huku wanaenda na makadirio ukiwapa kitabu chenye hasara watu wa TRA hawatakubali hata kidogo watakuwekea vi charge vya kijinga mpaka utalipa.Sisi tulikuwa na CPA lakini bado tulikuwa tunasumbuliwa waulize wenye maduka wanavyosumbuliwa Tanzania. Kuhusu mikopo sio swala la elimu mkopo wa bank wa 20% ni biashara ya magendo unayofanya italipa huo mkopo? Na ndiyo maana hawakopi na Mabilionea wengi wanakopa nchi za nje ambako mikopo ni chini ya 10%. Huwezi kuwa na system ya capitalism wakati mfumo wa capital ni mbovu
 

Unajua rushwa ina tokana na luck of information, if your well informed utalipa TAX ile unayostahili kulipa?

Watu wa TRA by nature sio Whasibu(Accountants) or Auditors ni revenue collectors kwa kukariri, na iwapo wewe unajua kodi zako zote na zinalipwa kwa wakati gani hawatoweza kukutoza kodi kijingajinga.

Ndio maana wenzetu wahindi, hawalalamiki kama sisi, wanachofanya ni compaliance(i.e) anajua yeye kama mfanya biashara ni kodi gani anatakiwa kulipa na kwa wakati gani? ana lipa kiduchu mradi awe na risti ambayo itamonyesha ana comply?

Mfano wewe ukiwa na hasara kwenye bisahara(na mind you kodi haikokotolwi to kwenye turn over hata kama ni mabilioni). ukakutwa kwamba hukulipa paye or withholiding tax kwenye mkataba wa pango(kama biashara umekodi duka/ofisi) watakutaka ulipe ndipo utaanza kusema nimepata hasara lakini, bado kuna vitu vidogo vidog bado wamenitaka nilipe?

Elimu bado inahitajika..... ya kodi/mikopo na biashara yenywe unafikiri Mkapa angesubiri tufundishwe wakati ndipo privatazation ije watu wa nje wasinge nunua kitu?
 
Nahisi una jambo jema la kufundisha wajasiriamali,ingekuwa vyema uje na uzi wako kabisa kutolea ufafanuzi zaidi coz hapa ni kwa kifupi sana kiasi ni ngumu kidogo kuelewa kwa undani.p
 
Watu Je wewe ni mfanya biashara maana kuongea na kutenda ni tofauti sana. Mimi vilevile najua nacho nina degree ya Finance na ingawa niko kwenye makampuni makubwa sasa najua accounting vizuri na kampuni nayofanya ina revenue $80B kwa mwaka. Tunajaribu kutoa ushauri tu kwamba hiyo mikopo ya 20% huwezi kukuza wafanyabiashara wa kati. Nitatoa sababu hapa ambazo ni ngumu kidogo kuzielewa lakini ndiyo sababu kubwa ya riba kuwa kubwa.
 
Hii niliandika ipo technical kidogo kwasababu ni corporate finance lakini sijapata njia rahisi ya kueleza


Naona badala ya kuongea siasa kila wakati tunaweza kuelimishana kwenye mammbo muhimu hapa.Hii topic nilishawahi kuituma.

Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi. Moja la tatizo kubwa linalokwamisha sana maendeleo ni hakuna utaratibu mzuri wa bank kusaidia uchumi kama ulivyo kwenye nchi zenye uchumi mkubwa. Mikopo ni migumu kupata na riba ipo juu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa wafanyabiashara wa kawaida kupata mikopo. Bank za Tanzania hazisaidii uchumi kama inavyotegemewa tena ukizingatia pesa karibu zote zimewekewa riba na bank kuu kwa kupitia serikali. Serikali na Bank kuu zinatakiwa kufanya yafuatayo
1. Vitambulisho: Serikali inatakiwa kuwa na vitambulisho vya uhakika ili watoa mikopo wa wapokea mikopo wajuane. Hii vilevile itasaidia kujua historia za watu za mikopo.
2. Historia ya mikopo au (Credit Rating System): Serikali bank kuu na wizara husika zinatakiwa ziweke utaratibu wa kuwa na hifathi (database) ambayo inaonyesha historia za watu kuchukua na kulipa mikopo.
3.Riba za T-Bills/T-Bond za serikali ziwe chini: Serikali inachukua pesa kwa wananchi na mashirika kwa njia hizi mbili. Serikali ikichukua hii mikopo inatoa vitu viwili muhimu (a) muda wa kuwalipa mikopo (b) riba ya mikopo. Riba ya hii mikopo ya serikali ambayo mara nyingi ni lazima ilipwe ni kubwa sana 7%-8% ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zina 2%-5%. Hii ni muhimu sana kwani bank ikitoa mikopo inatoa kutokana na riba hizi. Riba za bank ni lazima ziwe juu kuliko za serikali hivyo kama riba zao ni 5% na serikali ni 7% wanakupa riba ya 12%. Hii ni kwasababu watu ambao wanatoa pesa za mikopo ya bank hawawezi kuwekeza kwenye mikopo ya bank wakati mikopo ya serikali inauhakika wa kulipwa (Risk Fee rate). Kwa bank kupata wawekezaji ni lazima waweke kiwango cha juu zaidi.


 
My 2014 topic bado ipo valid baada ya miaka mitatu!
 

Well said mkuu.. Tatizo lingine ni kuweka kipaumbele kny kuongeza makusanyo ya kodi toka kny biashara "zinazosinyaa" badala ya kuzisaidia kukua
 
Na ifike mahali tuangalie tunawezaje kutatua changamoto zinazotukabali tukiachana na malalamiko kwa serikali, (conflict of interest) serikali inaangalia kwa upande wake ni kwa jinsi gani wanaweza kukusanya mapato kwawingi kutoka kwa wafanyabiashara hvyo kwa wafanyabiashara wanamkakati gani juu ya hli
 
kitu kikubwa kinachonshangaza wafanyabiashara wazawa wakubwa ni walewale miaka yote hawa wengne watainuka lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…