Mfumo wa ufundishaji kwa vikundi umekuwa nyenzo muhimu ktk kurithisha maarifa kwa wanafunzi,hasa wale ambao wanajifunza taratibu [ slow learners ]. Tumejaribu hili hapa kibangu na tumeona matokeo mazuri tu.
Watoto wasio na viwango sawa vya kufikiri wanaweza kumudu kujiamini na kujishirikisha ,kitu ambacho kina mpa mtoto
kujitambua na kujiona sehemu ya mfumo wa kujifunza. vile vile vikundi vina jenga urafiki na kutiana moyo kitu ambacho ni sehemu ya kufanikisha uwanja wa kufikiri.