kelvin bayona
Member
- Jul 18, 2022
- 16
- 8
Nchi yangu ya Tanzania kama inatamani kupiga hatua zaidi kwenye maendeleo ya tekinologia inapaswa kuangalia zaidi swala la elimu inayotolewa na vyuo haswa vya umma.
Unakuta mwanafunzi anamaliza shahada yake ya masomo akiwa anachukua masomo ya tehama lakini hakuna kitu alichotoka nacho kichwani ambacho anaweza kukifanya kwa vitendo, vyuo vingi vinafundisha kwa maneno tu nakupewa vitabu vya kwenda kupitia lakini hakuna vitendo.
Kama tunavyojua kuna wakati vyuo utoa nafasi kwa wanafunzi wake kwenda kufanya kazi kwa vitendo kile walichokisomea darasani(filidi) unakuta mwanafunzi kaletewa pale kompyuta aiunganishe labda ni mpya anashindwa pakuanzia, mimi binafsi na marafiki zangu tumepeta nafasi ya kwenda kufanya kazi kwa vitendo lakini kwenye hiyo taasisi tulipoenda kipindi chote hatukufanya kazi ya maana kwa sababu tulikuwa tunaulizwa mnaweza kufanya hiki tunajibu hapana lakini tunakumbuka mwalimu alitufundisha ubaoni na akatupa notisi zakwenda kusoma lakini hatukufanya kwa vitendo.
Hili tatizo litapelekea vyuo kukosa sifa za kuwa vyuo na vitajikuta vinatoa elimu kama wanayopata wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa sababu wanakeremishwa tu.
Siku zinavyozidi kwendelea itafika hatua hivi vyuo vikuu vitapoteza sifa za kuwa vyuo vikuu na elimu itakayokuwa inatolewa itakuwa haina utafauti na elimu inayotolewa kwenye ngazi za msingi na sekondari. Lakini pia kwa vyuo nilivyopitia na kufanya uchunguzi wangu binafsi nimeona kuanzia chuo chenyewe walimu husika na wanafunzi hawaichukulii tehema katika namna ya kipekee naona ni masomo ambayo hayana tija sana.
Changamoto ya ukosofu wa ajira nadhani inaweza ikachangia wanafunzi kutokuchukulia tehama katika hali ya upekee. Endapo serikali ikitoa kipaumbele kwenye elimu na ajiri kwenye nynja ya tehama wanafunzi wengi wataweza kujikita katika masomo hayo kama tunavyoona kwenye masomo ya sayansi tangu serikali imeewekea kipaumbele na kutoa nafasi ya kuwasomesha na kuwapeleka nje wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi wanafunzi wameongezeka sana, na mbinu hii inaweza kutumika katika tehama ninaamini mwitikio utakuwa mkubwa sana.
Mkufunzi wangu aliwahi kuniambia kwamba kuna banki hapa Tanzania mfumo wake ulipata hitirafu banki ikaanza kumtafuta mtu ambaye anaweza kurekebisha hilo tatizo ilimkosa mpaka ikaamua kumwagiza mtu kutoka kenya, sasa nikawa najiuliza kama hatuna watu wakurekebisha mifumo ambayo imekwisha kutengenezwa, je tutaweza kuwa na watu wakutengeneza hiyo mifumo kuanzia mwanzo mpaka ufanye kazi?
USHAURI KWA WANAFUNZI
1. Watu ambao wana taaluma au uelewa juu ya tehema wanahitajika kwa sasa na ni watu ambao watahitajika sana hapo mbeleni kwa sababu tekinologia inazidi kukua na kila kitu kitahitaji tekinologia ili kitendeke kwa usahihi, kwahiyo ni vema tukaliangalia hili swala la tehema kwa wakati ujao zaidi kuliko tunavolichukulia sasahivi.
2.Kuongeza bidii katika kuelewa na sio kukariri, kwasababu wanafunzi wengi wa wakatii huu tumekuwa tukisoma ili tufahuru tu, tumekuwa tunakariri ili nimalize muhura mmoja niende mwingini lakini hatumaanishi kwa kile tunachokisomea, tunasoma kana kwamba tumelazimishwa kusoma hayo masomo.
3. Kutumia mda wa ziada kutafuta na kujadiriana na wanafunzi wa vyuo vingine kuona wao kwenye mada fulani ya somo fulani wamejunza nini na wewe kitu gani hujajifunza. Kwasababu ninaamini kwa maisha ya chuo ni rahisi kupata mda wa kwenda chuo kingine na mkapata mda mrefu wa kusoma pamoja na kubadilishana mawazo
4. Kuwa na kompyuta binafsi. Hili swala ni muhimu sana kwasababu litakuwa linakuwa hata nafasi ya kuwaza kufanya mlichokisoma kwa vitendo kuliko usubiri kuazima kompyuta kutoka kwa rafiki au mpaka usubiri chuo kifunge chumba cha maabara ya kompyuta ndipo ukafanye kwa vitendo hili litakuweka nyuma sana na mwisho unajikuta umekata tamaa, lakini ukiwa na kompyuta yako ni rahisi sana kufanya ulitakalo na kwa mda wako.
USHAURI KWA SERIKALI NA VYUO VIKUU
1. Serikali ione haja ya kuanzisha vyuo vitakavyokuwa vinatoa mafundisho yanayohusu tehema tu visichanganye na masomo mengine na hivyo vyuo viwe na kila dhana mfani kompyuta, upatikanaji wa mtandao, kila mwanafunzi kuwa na compyuta yake binafsi etc, hili litasaidia mwanafunzi kuwasa swala analolisomea tu tofauti na saizi unakuta mwanafunzi anasomea tehama lakini humo humo anafundishwa masomo ya biashara humo humo anafundishwa mambo ya sheria.
2. Hili litalenga vyuo husika kuweka mitaara yake vizuri. Mfano unakuta kuna somo limegawanywa mara 2, (Networking 1 na networking 2) hapa ilo la (networking 1 ) mwanafunzi atafundishwa muhura wa kwanza, hilo la (networking 2) atakuja kufundishwa muhura wa tatu lakini ukija kuangalia haya masomo yanategemeana kwamba ulipoishia (networking 1 ) ndipo mwendelezo wa (networking 2) huyu mwanafunzi lazima aferi sababu itabidi akumbuke alipoishia (networking 1) huko muhura wa kwanza. Kwahiyo vyuo viwe vinaunganisha masomo kam hayo kwamba ukifunguq tu muhura wa pili uendeleze pale pale ulipoishia.
3. Pia kila chuo kinachotoa elimu ya tehama kuhakikisha kila madarasa maalumu kwa ajiri ya wanafunzi kusoma kwa vitendo wakati wanafundishwa au kwa mda wao wenyewe, hili litaongeza ubunifu kwa hawa wanafunzi ambao wanakuwa wanafanya kwa vitendo mara kwa mara, kwa sababu naamini masomo ya tehama hayana utafauti na masomo ya udaktari lazima mwanafunzi afundishwe kwa vitendo ndipo ataelewa kitu gana anapaswa akifanye kwa wakati gani.
4. Kuongezwa mda wa masomo kama ilivyo kwa udaktari wanasoma kwa miaka mitano, kwasababu na kuielewa tehema inahitaji mda mrefu na kutembea nayo tararibu. Siamini kama miaka mitatu inatosha mwanafunzi kuisoma tehama akailewa vizuri wakati huo huo unamwongezea masomo mengine ambayo hayahusiani na tehama, kwaiyo nadhani kwa masomo ya tehama na muhitimu kuhitimu shahada wasome walau miaka 4 alafu wa tano uwe kwa ajiri ya kusoma kwa vitendo wanapelekwa kwenye makampuni.
5. Mwanafunzi anapoanza kusoma masomo ya tehama apewe nafasi ya kuchagua kwamba yeye utahusika sana kwenye tehama ya aina gani, kwasababu tehema imegawanyika katika nyanja nyingi sana mfano watu wa (mifumo) watu wa (mitandao) watu wa (sanaa ya tehama) n.k, kama mwanafunzi wakati anaomba kusoma chuo angeorodheshewa nyanja atakayotaka ausike nayo kwa karibu ingekuwa rahisi sana yeye kuondoka naku kizuri kichwani kuliko asomo vitu vya aina tofauti kwa wakati mmoja au muhula mmoja halaf ndani ya miaka mitatu.

Upvote
2