Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
MFUMO WA USAGAJI CHAKULA (DIGESTIVE SYSTEM)
Tunakula aina mbali mbali za vyakula ambavyo ndani yake vina kabohaiedreti (wanga), protini, mafuta (fats). Chakula tunachokula huvunjwa vunjwa na kuwa chembe chembe ndogo, ambazo zinaweza kufyonzwa na mwili. Hii harakati yote ya kuvunjwa vunjwa chakula ili kuweza kufyonzwa.
Mwili una viungo kadhaa vinavohusika kwa pamoja na harakati za usagaji chakula navyo ni:-
i. Mdomo: Harakati za usagaji chakula huanzia mdomoni. Mdomo una meno, ulimi pamoja na maezi ya mate (salivary glands). Meno husaidia kuvunja vunja chakula kuwa vipande vidogo vidogo zaidi. Matezi hutoa mate ambayo husaidia katika usagaji wa chakula kiwe kilaini zaidi baada kuvunjwa vunjwa, pia hukitia unyevunyevu zaidi vyakula vya wanga kiasi kwamba kiweze kumezwa kwa urahisi zaidi. Ulimi hukichanganya chakula kwa mate na tena hukiviringisha chakula kuwa matonge madogo madogo na kuyasukumiza kwenye koo.
ii. Umio (Oespoghagus): Hili ni bomba la chakula. Kutoka mdomoni chakula huchukuliwa hado kwenye tumbo kupitia tyubu hii (tube)
iii. Tumbo (Stomach): Huu ni mfuko wa misuli. Chakula hukaa katika tumbo takriban masaa manne. Kuta za tumbo hutoka maji (gastric juice) kuta hizo ni misuli ambayo hutanuka na kusinyaa ili kukichanganya chakula kwa maji, ambayo sehemu husaga protini.
iv. Utumbo mdogo (Small intestine): Utumbo mdogo ni mwembamba, mrefu na ni tyubu iliyovirigishwa ugiligili (fluid) kutoka tumboni polepole huingia katika utumbo kwa mafungu madogo madogo. Na usagaji wa chakula huendelea kufanyika. Ini na kongosho (pancrease) huingiza ndani mnyunyizo wao. Nyongo kutoka katika ini huanza kufanyia kazi mafuta wakati maji ya kongosho (pancreatic juice) kutoka kwenye kongosho husaga sehemu ya protini na wanga ambayo haukusagwa. Kuta za utumbo pia hutoa maji ambayo husaidia kukamilisha usagaji wa wanga, protini na mafuta. Chakula kilichosagwa hufyonzwa kwenye damu, na damu hukipeleka chakula hicho katika sehemu zote za mwili.
v. Utumbo mpana (Large intestine): Chakula kilichobaki amacho hakijasagwa na hakikufyozwa huingi katika utumbo mpana pole pole kwa mafungu madogo. Utumbo mpana ni mfupi zaidi ya utumbo mdogo lakini utumbo mpana hufyonzwa sehemu kubwa ya maji na kuyapeleka katika damu. Chakula ambacho hakikusagwa huhifadhiwa na utumbo mpana na kuwa uchafu (faeces) na baadae hutolewa. Ufyozanji wa chakula huaanza muda mfupi tu chakula kinapoyeyuka ndani ya maji kwahio ni muhimu sana kunywa maji mengi sana kila siku.
CHAKULA KUTOSAGIKA TUMBONI
Dalili za kutosagika chakula tumboni:
Kusikia maumivu tumboni
Kiungulia (maumivu yachomayo nyuma ya mfupa wa kidari)
Kujihisi mgonjwa au kutapika
Kupiga miayo au kutoa upepo
Kuleta ladha ya uchachu mdomoni baada ya kula.
Kama baada ya kula na kupata dalili yoyote miongoni mwa hizo tutaiita hali hiyo ni kutosagika kwa chakula (Indigestion). Watabibu huiita " Dyspepsia" dalili hizo hutokeza kama kuna kitu kinaleta matatizo katika koo au tumboni.