guojr
Member
- Dec 4, 2015
- 62
- 95
Leo ningependa kuongelea kuhusu mfumo wa utambuzi unaotumika hapa nchini kwetu. Mimi binafsi nashindwa kuelewa kwanini inapofika swala la utambuzi kunakuwa na uchaguzi kadhaa za utambuzi mfano unaweza kuambiwa ulete kitambulisho cha taifa, kadi ya mpiga kura, leseni ya udereva au pasi ya kusafiria.
Ila mimi mawazo yangu yananiambia tunapaswa kuwa na nyaraka moja tu ya utambulisho ambayo ni kitambulisho cha taifa. Watu wengi walicheleweshewa au kukosa kabisa huduma fulani fulani kwasababu ya majina kukosewa au kuwa tofauti kwenye nyaraka zao zilizotolewa na mamlaka husika.
Nchi nyingi zilizoendelea zina mifumo madhuti katika kukusanya, kuhifadhi na kutumia taarifa hizi, sisi kama nchi ambayo ni sehemu ya dunia hii tunatakiwa tuendane na kasi ya ulimwengu. Kama ambavyo tunaelekea kwenye ulimwengu wa 5G, tunaambiwa kwenye teknolojia hii vitu vingi vitakua vinatumia mtandao kuanzia majokofu, viyoyozi hadi gari zetu.
Tukirudi kwenye mada sasa, haiwezekani mtu mmoja anakua na nyaraka zenye majina tofauti tofauti, unaweza kuona mtu kitambulisho cha taifa, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya shule vina majina tofauti. Kitaalam hata kama ni herufi moja tu ndio inaleta utofauti kwenye nyaraka zako basi kiutambuzi hizo nyaraka ni za watu tofauti.
Na wakati mwingine itakulazimu hata kwenda mahakani kuapa ili useme jina lako hasa ni lipi japokuwa wengi wetu tunachukulia kawaida majina kutofautiana kidogo kwenye nyaraka zetu.
Mimi nikiwa kama mtu ninaeamini katika mifumo na utaratibu, pia kama mdau wa teknolojia ningependekeza kwa serekali kufanya yafutayo ili tuweze kuendana na kasi ya maendeleo ya ulimwengu.
Moja, kila mtoto anayezaliwa apewe namba ya utambulisho ya taifa, na baadaye achuliwe alama za vidole na kupatiwa kitambulisho chake. Namba hii itakua ikiongezwa taarifa kadiri mtoto huyu anapopita kwenye hatua mbalimbali kwenye maisha, kama shule, hospitali, ajira, biashara na kadhalika. Kwamaana hiyo basi, ile namba inakua na taarifa zote kama vile amezaliwa, lini, hospitali gani, wilaya mkoa, taarifa za wazazi wake, shule alizopita kusoma, hospitali alizopita kutibiwa na taarifa za matibabu yake, ajira au biashara, taarifa za kodi hata miamala ya kifedha. Namaanisha taarifa zote zinazomhusu mtu zitapatikana kwenye namba hii.
Mbili, ili kupata taarifa hizi kwa usahihi, serekali iwekeze kwenye watu wanaochukua hizi taarifa wawe na weledi wa kutosha, wapate mafunzo ya namna ya kuchukua taarifa hizi muhimu kwasababu tumeona watu kwenye nyaraka zao muhimu kukosewa kwa majina na wengine wamebadilishwa jinsia na upoanza kufatilia kubadili hizi taarifa inakua changamoto sana.
Tatu, kuwekwe sheria maalum ya kudhibiti taarifa hizi nyeti na kila ofisi mtu atakapotembelea kwa ajili ya kupata huduma basi ofisi hizo ziwe na uwezo wa kuona taarifa zinazo wahusu tu. Pia mfumo utakua unaonesha nani ameangalia taarifa gani kwenye mfumo. Hii itadhibiti na kulinda raia na uvujaji wa taarifa zao binafsi.
Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya namna namba hii itakavyotumika katika utambuzi wa mambo mbalimbali katika kurahisisha huduma kwa jamii.
Umeenda hospitali, mhudumu anachukua namba yako anaweka kwenye mfumo wa hospitali, daktari anaweza kuona mara ya mwsho ulitibiwa hospitali gani na historia ya matibabu yako yote. Kwenye matibabu taarifa za nyuma ni muhimu sana kwa daktari ili iwe rahisi kuanza kukuhudumia kwa urahisi.
Kwenye ajira wanaweza kuingiza namba yako kwenye mfumo wa utambuzi wataona taarifa zako zote za taaluma na ajira kwa namna hii hutahitajika kuwa na nyaraka hata moja kama vile vyeti vya taaluma wala vitambulisho.
Kufungua akaunti benki na usajili wa huduma mbalimbali au vinavyofanana na hivyo wanaweza kuona taarifa zako binafsi ikiwa pamoja na mawasiliano, anuani ya makazi, tarehe ya kuzaliwa na kadhalika.
Kama unavyojua usajili ya huduma nyingi siku hizi bila kuwa na utambulisho wa anuani ya makazi tena unaweza kuambiwa upeleke barua ya utambulisho wakati tayari una kitambusho cha taifa inachekesha.
Kwenye huduma za mikopo wakiweka namba hii kwenye mfumo wanaweza kuona taarifa za miamala, mikopo ya nyuma na namna ulivyoilipa. Hii itarahisisha hata kwa ambao walikua hawapati fursa za huduma za mikopo kwa kutotambulika sasa wanaweza kuonekana sababu taarifa zao zote zitakua kwenye mfumo huu.
Hata kwenye manunuzi taarifa zake zinaweza kuunganishwa kwenye namba yako ya kitambulisho kitu ambacho inaweza hata kuisaidia serekali kukusanya mapata kwa urahisi. Kuna hduma nyingi sana za mitandaoni tunazikosa na pengine serekali inakosa mapato kwakutoweka sawa namna ya utambuzi. Inafikia mahali ili upate huduma fulani mtandaoni ni lazima uwe na pasi ya kusafiria, sasa unaweza kujiuliza ni wangapi wanamiliki pasi ya kusafiria?
Hata kwenye mambo ya kiusalama kama vile kudhibiti uhalifu wa kimtandao au wa aina nyingine kupitia taarifa zinazopatikana katika namba ya kitambulisho. Kama vile, kama uliwahi kuwa na kesi au kupewa adhabu kutokana na uhalifu.
Kumbuka kila eneo watakua na uwezo wa kuona taarifa zao tu, hivyo hatutegemei hospitali waone taarifa za miamala za kifedha au benki waone taarifa za matibabu.
Mwisho kabisa, kwakweli matumizi yanaweza kuwa mengi sana kadiri itakavyoonekana inafaa na inaweza kurahisha vitu vingi hasa kubebabeba makaratasi, najua hili linawezekana kabisa kufanyika bila shida yoyote ili kurahisisha utambuzi. Najua ni hoja fulani hivi nzito ila ndio hivyo tena dunia inaenda kasi sana kwahiyo nasisi tusibaki nyuma.
Sasa naomba kuwasilisha hoja.

Upvote
0