Mfumo Wa Vyama Vingi Kufutika Duniani

Bess

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
547
Reaction score
656
Baada ya dunia kushuhudia anguko LA mfumo wa kijamaa baada ya vita baridi, sasa ni wakati wa kuona anguko lingine LA mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi.

Baba wa demokrasia hii, US ameonekana kutingishwa na kwa kweli ameyumba baada ya kugundua pasi na shaka kwamba Russia ili- temper na documents muhimu sana ndani ya chama cha democrat wakati wa uteuz wa mgombea wao., walifanikiwa kukimega hiki chama kabla hata ya uchaguz, wakimlenga kummaliza Clinton aliyekuwa na Sera wasizozipenda.

Mashirika ya kiusalama wa mitandao zaid ya 10 nchiniwao walithibitisha kuhusika kwa Russia.

Haikuwa tu ndani ya chama, bali mifumo ya mashine zinazohusika moja kwa moja na kura vilionekana vidole vya mbabe Russia. Kukua kwa teknolojia na hasa kuanza matumiz ya AI(Artificial intelligence) ni tishio namba moja LA demokrasia ya vyama.,

Usishangae kura zikapigwa na watu ambao hawako na zikahesabiwa kura. Huyu ni anayejiita baba wa demokrasia.

Kutoaminika mfumo huu utaongeza kiu ya viongoz wengine kuanza kufikir mfumo mbadala wa kuongoza serikali.

Hata hivyo, bila kuhusisha maendeleo ya teknolojia ni kama vile mfumo wa vyama vingi unaonekana ama kudharauliwa au kuchokwa. Tupitie kidogo nchi zinazogonga vichwa vya habarr kimataifa. Tuanze Afrika;

Kenya kwa kweli hakukuwa na uchaguz huru na wa haki Bali ilikuwa tu kumthibitisha Kenyata kuongoza katika awamu ya pili. Uganda ni sawa na kusema jamaa ni Rais wa maisha. Rwanda itakuwa ndoto ya mchana KG kuachia nchi., Burundi kijana wetu ni Rais wa maisha tayar. DRC hamna haja ya kuuliza kilicho kwenye kichwa cha Rais wa sasa.

Zimbabwe imechukuliwa na MTU mwenye mawazo ya Mugabe, kichwani mwake Hamna msamiati wa demokrasia.

Nje ya Africa tunamuona Putin alivyo neutralize nguvu ya wapinzani pendwa wa wananch kisha akajishindanisha na vilaza wengine kisiasa. China ni hivi majuz tu chama tawala kimeondoa ukomo wa Urais...

Kwa kweli kutumia tu akili ya kawaida, nchi tambulishi kidunia zinapoyumba katika mfumo Fulani tujue kabisa ni mwanzo wa huo mfumo kufutika kabisa

Mfumo ulio anguka baada ya vita baridi na hasa baada ya kuanguka kwa kiongoz wao USSR wanaungana sasa kuangamiza na kuufuta kabisa mfumo ulio uti wa mgongo wa nchi za magharibi

Ni juz tu katibu mkuu NATO ametoa tahadhar ya nchi wanachama kushambuliwa na Russia kimtandao nyakati za uchaguzi., ikiwa na maana dalili ya mashambuliz Tayar IPO.

Hakuna MTU aliyeshangaa kusikia ile kura ya UK kujitenga na EU, Russia ilihusika kwa kiwango Fulani kusababisha matokeo positive ya BREXIT.

Demokrasia ya mfumo wa vyama vingi uko ICU
 
Nikweli.Hata mfumo wa kila nchi kuwa na serikali yake utafikia mwisho.
 
Dah....demokrasia ya mini wakati tuna vilaza 25% [emoji13] [emoji13]
 
Mmm,historia inatengenezwa na mwanadamu pengini kwa njia zisizo wazi,zilizo wazi au kutokana na mazingira yaliyopo.msuguwano huu utalete makundi makubwa mawili yaliyo na nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…