CCM ni kama binti aliyeonja utamu wa dudu kwa maumivu kwaiyo ni nataka sitaki. Anajua akiruhusu katiba mpya mapengo aliyokua yanamfaidisha yatapungua au kuondoka kabisa, akikataa wao wenyewe wanajua hii katiba mbovu haifai kwa sababu inasababisha migogoro ambaayo hata wao inawaadhiri. Mifano ya faida na hasara za mabadiliko ya katiba kwa CCM,
FAIDA,
-mamlaka ya raisi kuteua/kutengua ikimpendeza. Hii raisi kama mwenyekiti wa chama anao uwezo kujaza makada wa chama chake kwenye nafasi mbalimbali nyeti kuhakikisha wanalinda maslahi ya chama ie majaji,polisi ata jeshini na wenyeviti wa tume mbalimbali ie uchaguzi, haki za binadabu nk
-Uwepo wa maRC na maDC Hawa kimsingi wako kutokana na asili ya katiba hii ni ya chama kimoja hivyo vyovyote vile wapo kulinda chama kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama ndio maana lazima wawe wajumbe wa kamati ya siasa ya chama kwaiyo vyeo vyao sio vya kiutendaji kwa maendeleo ya wananchi
-Muingiliano wa mihimili ya serikali, hii ili ifanye kazi inabidi kuwe na check and balance Sasa kwa katiba yetu hii raisi ni mkuu wa mihimili wa dola lakini anaonekana yupo juu ya mihimili mingine bunge na mahakana ie kuteua majaji, kuwa sehemu ya bunge ie anateua mawaziri, wabunge pia anaweza kulivunja bunge kwaiyo sio bunge wala mahakama inaweza kumuingilia raisi kifupi yeye ni mfalme au malkia
-muudo wa vyombo vya ulinzi na usalama u kwa ajili ya kulinda maslahi ya serikali zaidi ya wananchi. Kwa katiba tuliyonayo tulichukua mfumo na muundo wa hivi vyombo kutoka kwa mkoloni iliachwa hivyo wakati wa chama kimoja mpaka sasa hivyo kwa nguvu ya raisi kama mwenyekiti wa chama anao uwezo kutumia vyombo kukilinda chama chake badala ya wananchi.
Kwa upande mwingine hii katiba ni Kaa la Moto kwa ccm,
-muundo wa muungano uliopo uliunda serikali ya muungano na ya mapinduzi kwaiyo unaleta mkwamo linapokuja masuala ya bara yanashughulikiwaje na serikali ipi kifupi serikali ya muungano imevaa koti la serikali ya bara
-maadili ya viongozi na utawala bora, katiba hii ikiboreshwa wakati wa vuguvugu la ujamaa ambapo viongozi hawakutakiwa kuwa wafanyabiasha lakini sasa ccm imejaa wafanyabiasha na mabwanyeye
-umoja na mshikamano wa kitaifa, kutambua uwepo wa tunu ambazo zinatufanya uwepo wa amani na mshikamano ie lugha kiswahili
Kiujumla Tanzania ya sasa inahitaji katiba itakayotokana na maridhiano pamoja ushirikishwaji wa wananchi katika makundi yote kukidhi nahitaji ya sasa na ya badaye ili kusonga mbele kwani uwepo wa sheria mama(katiba)bora utarahisisha mahusiano uzalishaji kiuchumi, kijamii na nyanja zote