SoC03 Mfumo wetu wa elimu ndo kilio chetu

SoC03 Mfumo wetu wa elimu ndo kilio chetu

Stories of Change - 2023 Competition

Miltony

Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
32
Reaction score
211
Kwanini Watanzania tunapotea katika elimu shuleni? Na kwanini tunasoma na mwisho wa siku tunakaa bila ajira? Ni kwa sababu zifuatazo

KISIASA: Kisiasa elimu inachukuliwa kama chama tu ambacho kinajitegemea na kinajiweza kwa kila kitu kana kwamba chenyewe hakiitaji nguvu ya ziada kusukumwa na kutazamwa mapungufu na ubora wake na ndo mwisho wa siku utakuta icho chama kinanyonywa tu na kupotea bila kujua kimepotelea wapi na kikipotea lazima na watu walio ndani ya chama watapotea watabaki wale wenyewe mawasiliano ma chama fulani chenye nguvu na ilo ndilo tatizo ni sawa na elimu kwa maana ya shule , haiangaliwi kwa umakini nini mazao yake na nini kinazalishwa apo shuleni na ni kina kazi gani baada ya kuzalishwa apo ndo utakuja kukuta wengi tumesoma bila kujua tulisoma ili kuzalisha nini na mwishowe tunashindwa maisha kwa sababu hatukuambiwa mapema icho tunachokisoma tutakipeleka wapi na tutakitumia vipi na wanabaki wachache tu wenye mtandao mkubwa ndo utawasikia wizarani.

2.KIJAMII : Kijamii elimu inajengewa taswira ya kusoma ili mda uende na uwe unakua na ukishamaliza tujue ni kitu gani cha kufanya kwa maana iyo elimu inawekwa pembeni na utafanya kitu tofauti ambacho hujasomea na kimerahisishiwa jina na kuitwa (kujiajili) lakini mda uo uo tukiwa tunasoma tunaaminishwa ukimuona juma anafanya kazi kwenye mgahawa jua ni mshamba hana elimu sasa ni kijana yupi atataka aonekane hana elimu ?? Na kasoma mpaka degree na arudi kule jamii ilikomuonesha kuwa ukifanya kazi hotelini au ukifanya kazi Bar ni ukosefu wa elimu au ni matumizi mabaya ya elimu mwishowe anaishia mawazo na kujiunga na makundi mabaya na madawa ya kulevya ni wapi tutapata kijana mkomavu kwa mfumo huu wa shule zetu??

3. KIUCHUMI:Elimu imejengewa taswira ya asiyesoma ndo mwenye pesa na aliyesoma anapoteza mda wake tu shule na akimaliza atakuta yule ambae hajasoma ana mali na yeye anajiona hana kitu hii inaharibu hata mtu anayesoma aone kama anapoteza tu mda na kuishusha ile thamani ya elimu na iyo inapelekea hata akimaliza aone wenzake wamemzidi ata kama mtu anafanya kazi gani anamuona tiyari kamzidi kiwango lakini ukiangalia mda uo yeye ana degree aliyoitafuta kwa mamilion ya fedha lakini bado haiwezi msaidia.

Ni kwanini yote haya? Ni mfumo duni wa elimu tulio nao zamani wazee wetu walisoma ili kuondoa ujinga kwa maana walikuwa na mali na pia waliridhika ila sisi saivi tunasoma ili kuipata pesa ni tunawekeza sio kusoma tu ni sawa na biashara.

Nini kifanyike?

Ni mengi ya kufanyika kiasi kwamba yote siwezi yaandika apa ila ntaelezea machache yanayo ona ni muhimu sana

1. MFUMO HURU KWA MWANAFUNZI, hii ni moja ya vitu ambavyo mwanafunzi anavikosa akiwa shule kwa asilimia kubwa anachokisoma shule ni kile ambacho serikali inataka sio mwanafunzi anachokitaka na unakuja kugundua tangu darasa la kwanza hadi form 6 yeye kajifunza kuandika , kuhesabu na kusoma hakuna kingine na baada ya apo chuo anaenda kufanya nini? Ndo labda anaanza kidogo kuamka yaani anaona kama ndo anaanza maisha , kwaio serikali kwa kushirikiana taasisi ya elimu waweke mfumo huru utakaomuwezesha mwanafunzi kusoma kitu ambacho anakiweza na sio kukiweza tu akipende pia hakuna raha kama kusomea na kufanya kitu unachokipenda tena tangu utotoni utakuwa mbali sana angaalau kuanzia darasa la nne.

2.ELIMU KWA VITENDO: tusi ishie kwenye kusoma na kuandika tu kuna mda tunaitaji vitendo zaidi mfano eti hadi mtoto anakuja kusoma ufundi wa umeme akiwa na miaka 23 (vyuoni) mda wote kasoma history ya lazima usiku kucha na wakati angesoma kwa vitendo labda angejua hata njia mbadala zaidi ya kufanya kazi na kupata kipato sisi tunaishia kukomaa na vitabu badala ya kujua jinsi ya kulima kwa trekta tunakomalia majembe na yenyewe kwa adhabu sio kujenga zaidi na wakati tupo katika ulimwengu wa teknolojia ambao mashin zinatumika kuliko mikono yetu serikali iliangalie ilo.

3.KIPAUMBELE : Serikali iweke kipaumbele kwa elimu kabla ya kuiangalia siasa kwa maana ya kwamba fedha inayowekezwa katika siasa mara mikutano ya apa na pale mara semina ambazo inafaidi asilimia ndogo sana ya watanzania iwekezwe katika sekta ya elimu kwa kufanya mambo yanayoonekana , mwalimu hawezi fundisha vyema akiwa na mawazo nyumbani watoto wanalala njaa hali duni unahisi nini wanafunzi watajifunza kutoka katika elimu wakati walimu ni maskini?

Ina maana apo kazi ya elimu itakuwa inapotea maana msomi mwenyewe inaonekana hana maisha sasa kwanini namimi nitie nia ya kusoma kama yeye na hana?? Serikali iweke macho zaidi ya sana pia na katika uboreshaji wa mazingira na miundombinu ya shule pamoja na vifaaa hii itasaidia achilia mbali maswala ya elimu bure mkiboresha elimu ina maana kila mzazi mbeleni atakuwa na maisha bomba ataweza kulipa ada kwa sababu anajua alichovuna shule.
Yote hayo yaliyoorodheshwa kwa juu yakifanyika nini kitabadilika

1. Kwanza mwanafunzi hatakuwa na uelewa wa kusoma na kuandika na kutumia akili katika karatasi bali atakuwa ana uwezo wa kutumia akili yake kubuni kitu kipya zaidi ya kile alichosoma na pia itamuwia rahisi yeye kujiajili kwa sababu anajua ni nini anafanya kwa asilimia zote akisoma kuanzia darasana la nne elimu ya vitendo .

2. Itafuta utaratibu wa kwenda maofisini na kuambiwa kwamba ni lazima kujitolea ili tujue kama una uzoefu kwa sababu mwanafunzi atatoa vyeti vyake tangu nyuma na alichokipambania na ataonesha kafaulu wapi hadi kuna apo ofisini sio mambo ya uzoefu na kujitolea yote ayo yatawezekana kama kweli Serikali itaweka mfumo huru wa kusoma kwa mwanafunzi, itatoa kipaumbele kwa mwanafunzi na pia kama itatoa elimu kwa Vitendo Tanzania itaenda mbali zaidi kuliko mfumo wa sasa wa kukaa na kukariri kisga chuo tunapitia tukija mtaaani tunaambiwa hatuna uzoefu tujitolee kwanza na badi hupati ajira , mfumo unakazia kwenye kukariri na kuandika na sio utafutaji wa pesa.

ELIMU YA SAIVI NI KUWEKEZA SIO TENA KUSOMA KUONDOA UJINGA NI SAWA NA BIASHARA TUNATEGEMEA FAIDA
Kijana mwandishi
Tonny
 
Upvote 36
Hongera umenena.elimu ya Sasa sio yakuondoa ujinga elimu ni maisha elimu ni mtaji elimu ni pesa.sasa mtoto anasoma kwa mamilion ya pesa na hko kapeza muda n ujinga.mitaala zibadilishwe watoto wafundishwe ujuzi wakajiajiri.Hii y Sasa ni upuuzi mtupu.watoto wanaffundishwa mtambuka.

Elimu mtambuka ni elimu ambayo mtu yeyote anaweza PATA bila kwemda darasani ndo maana wasomi wetu wanadharaulika.leo hii ambaye hajasoma na anauwezo anathaminika kuliko msomi.
 
Hongera umenena.elimu ya Sasa sio yakuondoa ujinga elimu ni maisha elimu ni mtaji elimu ni pesa.sasa mtoto anasoma kwa mamilion ya pesa na hko kapeza muda n ujinga.mitaala zibadilishwe watoto wafundishwe ujuzi wakajiajiri.Hii y Sasa ni upuuzi mtupu.watoto wanaffundishwa mtambuka.elimu mtambuka ni elimu ambayo mtu yeyote anaweza PATA bila kwemda darasani ndo maana wasomi wetu wanadharaulika.leo hii ambaye hajasoma na anauwezo anathaminika kuliko msomi.
 
Hongera umenena.elimu ya Sasa sio yakuondoa ujinga elimu ni maisha elimu ni mtaji elimu ni pesa.sasa mtoto anasoma kwa mamilion ya pesa na hko kapeza muda n ujinga.mitaala zibadilishwe watoto wafundishwe ujuzi wakajiajiri.Hii y Sasa ni upuuzi mtupu.watoto wanaffundishwa mtambuka.elimu mtambuka ni elimu ambayo mtu yeyote anaweza PATA bila kwemda darasani ndo maana wasomi wetu wanadharaulika.leo hii ambaye hajasoma na anauwezo anathaminika kuliko msomi.
Ee boss tunawekeza ila tunaambulia kukaaa bila chochote
 
Hii ntaisoma jumamosi halafu niletee a critical analysis
Sawa boss ila cha muhimu tunaona vijana wengi wamesoma ila mwishowe elimu yao ni ya karatasi sio vitendo je ni wapi utapeleka makaratasi bila ufanisi wa vitendo ueleweke? Kwaio ni lazima elimu ya vitendo ipewe kipaumbele kuliko makaratasi mtu hata akifail ila angalau ana chochote kitu cha kuanzia mkuu
 
Kwanini Watanzania tunapotea katika elimu shuleni?? Na kwanini tunasoma arafu mwisho wa siku tunakaa bila ajira?? Ni kwa sababu zifuatazo
Mkuu hapo ulipoandika "ARAFU" pamenikata stimu ya kuendelea kusoma, badilisha ili niweze kurudi kusoma niweze kupiga kura kihalali.
 
Back
Top Bottom