Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Wakati dunia ikianza kupata afueni kutokana na Covid, ghafla inaingia vita ya Russia VS Ukraine na mataifa makubwa ya magharibi yanaungana pamoja kuiwekea vikwazo Urusi. Tofauti na mataifa mengine yanayowekewa vikwazo, Urusi ni namba mbili kwa uzalishaji wa nishati duniani huku mteja wake mkubwa akiwa bara Ulaya.
Mfumuko wa bei Marekani umefika 7.9 kikiwa kiwango cha juu kwa miaka 40 sasa huku vita na vikwazo vyake vikiwa havina dalili ya kupoa. Tanzania ni mtegemezi mkubwa wa mafuta katika uchumi wake hasa sekta ya usafirishaji ambayo ina mchango mkubwa katika mabadiliko ya bei.
Angalau kwenye nishati ya umeme utegemezi wa gesi ya kusini mwa nchi unapunguza haya maumivu. China kaamua kufunga mkataba mpya wa nishati na Saudi Arabia kuyakabili yajayo.
Kama Taifa tumejiaandaje na yajayo yanayoonekana hayafurahishi kama suluhu isipopatika mapema Ukraine.