Mfumuko wa bei nchini Tanzania umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 ya mwezi Oktoba, 2019

Mfumuko wa bei nchini Tanzania umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 ya mwezi Oktoba, 2019

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Imeripotiwa kuwa Mfumuko wa bei nchini Tanzania kwa mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 ya mwezi Oktoba, 2019.

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii wa ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja ameyasema hayo leo Jumanne Desemba 10, 2019 mjini Dodoma.

Amefafanua kuwa hali hiyo inaashiria kuongezeka kwa kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi Novemba 2019.

746D2AF5-2A09-42B4-B98D-41806447D139.png


"Kuongeza kwa mfumuko wa bei kumechangia na kuongeza kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Novemba 2019, "amesema.

Ametaja baadhi ya vyakula vilivyoongezeka bei kuwa ni mchele kwa asilimia 6.6, unga wa mihogo (7.8), nyama (2.6), mafuta ya kupikia (7.2), maharage (8.6), mbogamboga (6.0) na mihogo kwa asilimia 5.8.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Novemba 2019 ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, mkaa (4.4), samani (3.1), huduma ya malazi kwa wageni (5.0) na mazulia kwa asilimia 6.3.


Chanzo: Mwananchi
 
Na hapo ni baada ya kuchakachuliwa sasa jiulize data halisi zikoje!!?
 
Mfumuko wa bei nchini Tanzania KWA mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 ya mwezi Oktoba, 2019.
 
Watu wamesoma takwimu lkn wanajiondoa ufahamu. Nyama ya ng'ombe imepanda toka 6500 mpaka 7000 eti imepanda kwa asilikia2. 6. Hesabu za wapi hizo????
 
Fyatueni tu madawati yamechongwa msiwe na wasi wasi.
 
Miezi kama hii ni kawaida bei za vyakula kupanda,.
Na bei kama mahindi ilisemwa ijipange yenyewe. Kama vipi lima mahindi yako
 
Back
Top Bottom